Kampeni ya kukuza Utalii kwa kutumia wasanii wa ndani.

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
4,345
13,078
Katika kuelekea mwishoni wa mwaka jana kulikua na harakati za kutangaza utalii wa nchi yetu kutumia "celebrities" wetu wa Kitanzania. Katika kampeni wasanii wa filamu pamoja na wa Bongo fleva walihusika kwa kushirikiana na kiongozi wa Wizara husika. Mimi ni mdau wa utalii na ninajua utalii wa Tanzania kwa kiasi changu. Kwa kufanya analysis ya kampeni ile naweza kusema malengo ya kutangaza utalii kwa namna ile yanatija ndogo sana kwa utalii. Kwa sababu zifuatazo..

1. Watanzania tunafahamu hifadhi zetu
Ukiangalia ile kampeni ilikua kana kwamba watanzania hatujui vivutio vyetu kitu ambacho si kweli. Kwa maana hiyo kumtumia Ayo, Naseeb na wengineo ambao 99% ya followers ni Watanzania haina mashiko sana (poor allocation of resources) sababu tatizo la sisi si kutokujua uwepo wa Serengeti, Ngorongoro au Ruaha ila tatizo ni uwezo wa kwenda kutembelea hivyo vivutio.

2. Utalii ni ghali
Ukichukulia hifadhi zetu za taifa kitu pekee ambacho Mtanzania wa kawaida kwake ni nafuu ni Kiingilio tu cha hifadhini lakini vyote vilivyobaki si rafiki. Kuanzia gharama za malazi hadi usafiri ndani ya hifadhi.

Nini Kifanyike?

Kwa utalii wa Mbugani ili mtanzania wa kawaida aweze kufanya kuna haja ya kutatua tatizo la usafiri ndani ya hifadhi. Ambapo hifadhi inaweza kua na magari yao kama ilivyo kwa hifadhi ya Mkomazi ili kuweza watembeza watu ndani ya hifadhi. Pili kuboresha public campsites ndani ya hifadhi kwa kuweka miundo mbinu rafiki zaidi kwa watanzania kutembelea hifadhi zetu kwa gharama nafuu na usalama wa kutosha.

Baada ya kufanya hayo sasa hata Wizara ikiwatumia wasanii kutangaza utalii wa ndani na kuweza kuwajulisha upatikanaji wa huduma husika kwa gharama nafuu utalii wa ndani utakua.

****************
Zile hoteli za kitalii ndani ya hifadhi zinazotoa huduma za malazi kwa wasanii bure si kwamba wao hawakufanikiwa katika kutangaza hoteli zao, ni wamefanikiwa sana sababu target yao si wewe bali ni ile 1% ya watanzania ambayo wanaweza fanya utalii ukweli wa kuufanya. Hivyo kwa kumuona mbongo fleva/bongo movie ndani ya hoteli husika yule Mtanzania anayeweza nunua atahamasika.
 
Back
Top Bottom