Kampeni ya Kuirudisha UDA mikononi mwa wananchi; Haja ya Mfumo Bora wa Usafiri Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni ya Kuirudisha UDA mikononi mwa wananchi; Haja ya Mfumo Bora wa Usafiri Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 13, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  udacampaign_phixr.png
  Utangulizi
  Tulipoanza kampeni ya kurudisha kampuni ya Kiwira mikononi mwa serikali watu hawakuamini kama inawezekana. Kwa wanaokumbuka kampuni hiyo ya makaa ya mawe ambayo kuendelezwa kwake kungesaidia sana kupunguza tatizo la nishati ya umeme nchini iliuzwa kinyemela kwa viongozi wa serikali miongoni mwao ni familia ya Rais Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini Bw. Daniel Yona.

  Tulipoanza kampeni ya kuidai Kiwira irudishwe watu wengi wanafikiri tulikuwa tunafanya utani. Tulianza kampeni hiyo mwaka 2007 na niliandika makala kwenye gazeti la Kulikoni wakati ule isemanyo “Mkapa, Yona wanyang’anywe Kiwira”. Hii ilikuwa ni kabla wabunge hawajaanza kupigia kelele Bungeni kutaka Kiwira irudishwe serikalini. Ilituchukua muda na wengine walidhani tunafanya utani au ilikuwa ni jitihada ya bure lakini pole pole watu walianza kuamini tunachogombania siyo utajiri wa Mkapa au Yona bali urithi wetu na ule wa watoto wetu. Hatukutaka kuona mali ya wananchi wa Tanzania inapigwa rehani.

  Kutokana na suala hilo tulijifunza vitu kadha wa kadha mojawapo ni kuwa sera yao ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma japo kinadharia ilikuwa nzuri lakini imetengeneza mabepari waporaji ambao hawataki kuingiza uwezo na fedha zao katika kuanzisha miradi yao bali wako tayari kama kupe kudandia miradi ya watanzania! Tulitambua kuwa ubepari ambao tuliukataa toka mwanzo wa taifa letu umerudi kwa nguvu kwa jina la “uwekezaji” na safari hii siyo kutoka kwa watu kutoka ng’ambo bali kutoka kwa watu wetu wenyewe!

  Tukagundua kuwa bila kuwakataliwa watawala wetu wanaweza kuuza kitu chochote na kwa sababu yoyote. Na ndio maana naamini kuwa endapo Watanzania wataamua kukaa pembeni na kupiga makofi tu bila kuhoji au hata kukataa wanaweza kujikuta wanaamka siku moja kama waliokuwa kwenye usingizi mzito wakiulizana ni lini taifa lao liliuzwa jumla?

  Sakata la UDA ni suala la namna hiyo. Bila ya mgogoro wa fedha uliojitokeza kati ya wahusika na mchakato, UDA ingeuzwa kinyemela na wananchi wasingejua zaidi ya kusikia tu shirikia “limebinafsishwa”. Hakuna wa kuhoji hakuna wa kulalamika. Kama wahenga walivyosema mchawi hawi mchawi hadi mtoto wa kwake aliwe! Baada ya wahusika kuanza kuzungukana ndio tumegundua kuwa wachawi wengine hawatoki nje, ni sisi wenyewe.

  Hivyo basi, kampeni hii ina kusudio moja tu la kwanza nalo ni kurudisha UDA mikononi mwa wananchi na kutoka hapo kufikiria namna gani shirika hilo na lile la Mabasi Yaendayo kasi yataweza kuunganishwa ili kutengeneza mfumo wa kisasa wa usafiri wa mabasi ya umma jijini Dar na yawezekana kuigwa katika mikoa mingine vile vile.
   

  Attached Files:

 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Aug 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe lakini itakaporudi mikononi mwa wananchi ni nani atakabidhiwa dhamana ya kuiendesha?
  Wasiwasi wangu ni aina ya viongozi wa jiji tulionao
   
 3. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,834
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  MMJ Nafurahia sana kwa Upambanaji wako Dhidi ya Madhalimu wa Hii nchi ambao wanakula hata bila kunawa!! Ni uporaji na kufuru Nyingi zimetawala!! Kuirudisha UDA Mikononi mwa wananchi mimi naona bado sio kazi Ngumu, Kwani tunaweza kufanya new Evaluation na kujua Thamani Halisi ya Shirika kwa kutumia independent Valuers!! Then Tuseme thamani halisi ya kampuni itakuwa 30billions!! (Tujue Kampuni ilishajenga jina kwa Muda mrefu hiyo ni additive Value!!) Then Tunawatambua hawa wawekezaji Uchwara simon, kama watu waliowekeza kama Wabia wa kampuni, say ownership yao kwa hizo 285 million (Kama zipo kwenye account za uda) Waweze kupewa hisa Zao kwa Gharama walizolipia (Say 2%)!! Then hisa Nyingine Zinauzwa kwa wawekezaji wengine!! That is Simple hakuna Haja ya kuwapeleka Mahakamani we will be wasting time and Money!! Ifahamike kwa dar es Sasa tunatakiwa tuwe na kitu cha Kujivunia!! Say Reliable Transport na sio adha iliyopindukia!! Najua hatuna barabara ijapokuwa watu wachache waliochoka kufikiri wanasema ni wingi wa magari kitu ambacho sio kweli!! Ningependelea Tuanzishe Ring road system ambazo magari haya yatakuwa yanapita, Then wawekezaji wawezi kujitokeza na kuwekeza!!
   
 4. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi kupitia maandishi yako ndugu yangu Mwanakijiji, huwa unanipa fursa ya kuiona Tanzania kama Taifa kubwa na imara, lenye watu wenye kuwaza makubwa juu ya mustakabali wao!
  ALUTA........
   
 5. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  This is a good movement! Ila wasiwasi wangu ni kama wa mchangiaji Bishop Hiluka kuhusu watu watakaopewa dhamana ya kulisimamia hilo shirika.Nadhani watakuwa ni wale wale ambao wamelifikisha hapo lilipo.
   
 6. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Big up mwanakijij!!! ile ngoma ya BOGOTA imenikumbusha enzi zile za kumbakumba (ikarus).
   
 7. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #7
  Aug 13, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  iwe kuirudisha mikononi mwa wananchi lakini iongozwe na viongozi wenye maadili, vinginevyo yatakuwa yale yale!!!!!............mashirika kibao ya umma yamekufa mikononi mwa hao hao wananchi! hata wanyama mbugani watapenda wajilinde dhidi ya uzalimu wa binadam lakini kuwawekea simba kuwa mlinzi wao hujawasaidia swala katika kujilinda.
   
 8. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Uda,uda,uda.,je linatusaidiaje sisi watu wa dar?
   
 9. M

  Mr.Right JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 408
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kidogo napinga hiyo hoja. UDA inatakiwa ibinafsishwe siyo kwa asilimia zote. Serikali inatakiwa iuze stake yake at least 60%, halafu serikali imiliki only 40% ili kuongeza ufanisi.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ninaamini kuwa Tanzanua ina wati wenye uwezo wa kufikiri na kutataua changamoto zilizopo mbele yao. Uwezo huu yanapotokea mauzauza kama ya UDA kwa kweli unahojiwa. ninayo mapendekezo ya jinsi ya kuliendesha shiriki hili kwa ufanisi, weledi na jwa muda mfupi kuondoa daladala na kuingiza mabasi ya kisasa.

  Lakini tufanye ya kwanza kwanza and in this case to reverse the privatization of UDA.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,204
  Trophy Points: 280
  Asante MMKJJ, safari ni hatua, 'moja shika sii kumi nenda rudi', hivyo kwanza tuishike, ndipo tuijadili tuiendeshaje.
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  sidhani kama inahitaji kuendeshwa na viongozi wa jiji! iundwe bodi upya yenye wataalam watakaoshauri na kuismamia. na uongozi uwe on competency base. kama wakihitaji wanaweza kuajiri mkurugenzi expert awapeleke puta hadi kieleweke,na profit iwe realised!
   
 13. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  wananchi wabaki na 51% na mwekezaji 49% kama BP Umma kupewa 100% ni maumivu na siyo kwa govmt hii
   
 14. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji , unamawazo mazuri.
  Ila tatizo ni kuwa bila ruzuku ya serikali, UDa haiwezi kujiendesha kabisaa. Kurudisha UDA mikononi mwa wananchi ina maana kuwa lazima serikali iwe inatoa ruzuku kwa UDA.

  Kama Tanzania ingekuwa na Adhabu ya kifo kwa watu wote wenye kuhujumu mali za umma , hapo ningekuunga mkono UDA iwe mikoni mwa wananchi. Maana hii secta ya transort za mijini inaingiza pesa nyingi sana ila tatizo ni wizi wa pesa za umma unaofanywa na viongozi wa Idara hiyo.

  Utakuta kwanza wanajipangia mishahara mikubwa sana . Halafu vikao vya bod members haviishi. Halafu semina za nje haziishi. Njoo kwenye posho. Hose allowance. Millage allowance. Funeral expenses.

  Lakini ukiwapa watu binafsi, hizo posho ni ndotto na mishara mikubwa sana ni ndotto pia. As long as hatuna adhabu ya kifo tanzania, wewe achia tuu watu binafsi wachukue ila serikali iwabane katika kutoza nauli kbwa kama ilivyo wadhibiti wauza wese.

  Nchi za Ulaya, marekani na Israel, secta hizo za usafiri huwa zinamilikiwa na serikali. Lakini wao hutoa sana ruzuku kwa makampuni hayo ya commuter services. Halafu sheria zao za udhibiti wa pesa ni kali kama vile kuku akilinda vifanga vyake vya siku moja.
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #15
  Aug 13, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,220
  Likes Received: 7,339
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote naunga mkono hoja, kuunga mkono kunatokana na mambo kadhaa: Kwanza kabisa, usafiri wa umma ni suala nyeti na linaloigusa jamii na serikali . Katika nchi zilizoendelea hakuna mahali usafiri wa umma umetengwa na serikali na sababu ni za kiuchumi na kimaendeleo.

  Pili, watu wana wasi wasi kuwa usafiri wa umma maana yake ni umiliki wa serikali, inaweza kuwa au hapana. Kwanini watu wasijiulize inakuwaje CRDB ifanye vema katika soko la ushindani wa fedha? Tujiulize, kwa kuogopa umiliki wa umma kwanini basi tusibinafsishe halamashauri ya jiji la Dar es Salaam, kwasababu ya uzembe na kushindwa kutekeleza majukumu! na kwanini manispaa ya mji wa Moshi inaendelea kuwa na ufanisi kama manispaa zingine duniani(ni moja ya manispaa bora barani Afrika).

  Tunaposema UDA tunazungumzia shirika kama Precision Air, tofauti inakuja kwenye uongozi. UDA viongozi walitokana na mfumo mbovu wa uteuzi, kwamba mhusika anawajibika kwa mtu mmoja na si waajiri wake. Kama tulivyoona madudu ya ATC, ambapo bodi ya wakurugenzi ilimuona Mustafa Nyanganyi ana makosa na ameshindwa kuongoza shirika, wakamwandikia Rais. Rais kwa huruma, heshima au urafiki wake na Nyang'ganyi amekaa kimya shirika limekufa. Tatizo hapa si ATC ni mteuzi wa management.

  Kama tunakubali kuwa DART inaweza kuwa na ufanisi na tafiti zimeonyesha UDA inaweza kuwa mshiriki mzuri kwanini visifanye kazi pamoja!
  UDA kuwa mikononi mwa umma haina maana kuendeshwa na serikali, upo uwezekano wa kuuza share, serikali ikawa na hisa, jiji, makampuni na watu binafsi. Mimi nitatanunua shea kwa kuelewa kuwa biashara ya dala dala inalipa na uwezekano wa UDA kufanikiwa ni mkubwa.
  Uongozi utokane na shirika bila mkono wa serikali na uwajibike kwa wana hisa. Ndivyo wenzetu wanavyofanya duniani.

  Endapo shughuli za usafiri wa umma hazina umuhimu kwanini dala dala wakigoma viongozi wote wana haha kutafuta muafaka!
  Ili kuwa sehemu ya muafaka ni lazima ushiriki uwepo na ndipo tunasema kuna ruzuku na kununua shea. Ruzuku haina maana kutumbukiza pesa za bure ili zitafunwe, inaweza kuwa katika misamaha ya kodi na ujenzi wa miundo mbinu.

  Hivi hatujajifunza kitu kutoka CRDB, NMB na Manispaa ya Moshi!! japo kwa uchache.
  Kwanini tuogope kumiliki UDA na tupange foleni kuchagua uongozi wa Jiji lililoshindwa kazi kwa kigezo chochote kile duniani.
  Jiji lisiloweza kuzibua hata mtaro!!!, kwanini tusianze kubinafsisha jiji kama tunadhani ubovu wa ufanisi ni matokeo ya umiliki wa umma.

  Tusiogope vivuli vyetu, mmiliki wa dala dala 20 anawezaje kufanikiwa na wanahisa wa UDA wakashindwa!
  Kuna hofu inajengwa na wenye dala dala kuhusu hili lakini ukweli unabaki ulivyo, biashara hii inalipa na inatakiwa kuwa chini ya umma ili kuleta ufanisi, usalama na maendeleo ya wananchi.

  Hii ni sekta muhimu sana katika maendeleo ya jamii, ni kwa nchi za hovyo tu hawalioni hili.
  Tumedanganywa soko huru,lakini kule lilipoanzia New York, London, Muscat, Singapore, Beijing, Copenhagen, Vancouver, Ulan Bator, Johaness burg, Samoa, Mauritius, Fiji na Tonga soko halifanyi kazi hivyo, kwanini tuwe na soko huru tofauti na waalimu wetu kwenye usafiri wa umma?
   
 16. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  MMKJJ,
  Mnyumbuisho wako ni mzuri na ninaamini watanzania na watendaji wengi serikali kuu na serikali ya jiji wanafahamu faida za mfuno umma wa usafirishaji. Kwa kuwa Watanzania (na waafrika wengi kwa ujumla) wanamatatizo makuu mawili (hapa chini)
  1. Umaskini mkubwa na kufikiri kila ajira watayopata ipo pale kwa wao kutajirika kiasi kwamba hawafikirii tena umma bali matumbo yao kwanza
  2. Ukosefu wa huduma kwa mteja (customer service)
  basi hakutakuwa na maendeleo yoyote! Ukiangalia kwa umakini sana mkataba wa ujenzi wa mabasi yaendayo kwa kasi utagundua kuwa mradi ulipopembuliwa ulionesha faida (pesa) kubwa achilia mbali kuondoa usumbufu wa usafiri kwa umma na ajali za barabarani. Sasa wajanja wajanja (hao wanaofikiria kujikwamua ili wawe matajiri wenyewe) wakaona njia nzuri ni kulifisadi shirika la UDA ili liiingie mikononi mwao na wao wapate hio faida ya pesa tu.
  Kinadharia kampeni yako ni nzuri, hata hivyo cha kujiuliza hili shirika lilikuwa limelala wapi? Je watendaji wake wataweza kumudu kulifufua? Ama nini kifanyike kuondoa matatizo mawawili hapo juu na kulifanya lifanye kazi kama lilivyotarajiwa kufanya.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Aug 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  swali linatakiwa kuwa Je UDA itusaidieje sisi watu wa DAR tutakapoirudisha mikononi mwetu?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Aug 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  absolutely, tatizo liko wapi? mbona tunatoa ruzuku kwa vyama vya siasa kila mwezi ili watutawale au waje kututawala?
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Aug 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  tayari sekta "binafsi" inaendesha asilimia 90 ya usafiri wa watu jijini dar.. kuna ufanisi? kwanini kwa karibu miaka thelathini hatujaona hicho kinachoitwa ufanisi wa sekta binafsi ambao tuliambiwa ungekuja kutokea kwa sababu ya ushindani wa soko huru?
   
 20. Nyota Ndogo

  Nyota Ndogo Senior Member

  #20
  Aug 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  rekebisha kidogo................

  andika

  wananchi wa Tanganyika
   
Loading...