Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,796
11,959
MATOKEO - LIVE:




Wakuu,

Tunawaletea matukio na matokeo rasmi kwa nafasi ya Urais kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kama yatakavyokuwa yakitangazwa.

Orodha rasmi ya wagombea wanaowania Urais kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Kama ilivyo kwenye karatasi ya kupigia kura)

1. Chama cha Mapinduzi
Dkt. John Pombe Magufuli - Mgombea Kiti cha Rais
Bi. Samia Suluhu Hassan - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

2. ADA TADEA
Bw. John Paul Shibuda - Mgombea Kiti cha Rais
Bw. Hassan Kornely Kijogoo - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

3. SAU
Bw. Muttamwega Bhatt Mgaywa - Mgombea Kiti cha Rais
Bi. Satia Mussa Bebwa - Mgombea kiti cha Makamu wa Rais

4. NRA
Bw. Leopord Lucas Mahona - Mgombea Kiti cha Rais
Bw. Khamis Ali Hassan - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

5. Demokrasia Makini
Bi. Cecilia Augustino Mwanga - Mgombea Kiti cha Rais
Bw. Tabu Mussa Juma - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

6. NCCR Mageuzi
Bw. Yeremia Kulwa Maganja - Mgombea Kiti cha Rais
Bw. Khamis Haji Ambar - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

7. CUF
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba - Mgombea Kiti cha Rais
Bi. Hamida Huweishil Abdalla - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

8. ACT Wazalendo
Bw. Bernard Kamillius Membe - Mgombea Kiti cha Rais
Prof. Omar Fakih Hamad - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

9. UPDP
Bw. Twalib Ibrahim Kadege - Mgombea Kiti cha Rais
Bw. Ramadhan Ali Abdallah - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

10. ADC
Bi. Queen Cuthbert Sendiga - Mgombea Kiti cha Rais
Bw. Khamis Juma Shoka - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

11. DP
Bw. Philipo John Fumbo - Mgombea kiti cha Rais
Bi. Zaina Juma Khamis - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

12. CHAUMMA
Bw. Hashim Spunda Rungwe - Mgombea Kiti cha Rais
Bw. Mohammed Massoud Rashid - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

13. AAFP
Bw. Seif Maalim Seif - Mgombea Kiti cha Rais
Bw. Rashid Ligania Rai - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

14. UMD
Bw. Khalfan Mohammed Mazrui - Mgombea Kiti cha Rais
Bi. Mashavu Alawi Haji - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais

15. CHADEMA
Bw. Tundu Antiphas Lissu - Mgombea Kiti cha Rais
Bw. Salum Mwalimu Juma - Mgombea Kiti cha Makamu wa Rais


UPDATE:

SHIBUDA AGOMA KUPIGA KURA

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ADA-TADEA, John Shibuda amegoma kupiga kura hadi mawakala wake Wilayani Maswa watakaporuhusiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura baada ya kuzuiliwa kwa madai kuwa hawana barua za utambuzi.

UPDATE

DKT. MAGUFULI NA MKEWE WAPIGA KURA

Dkt. Magufuli na mkewe, Janeth Magufuli wamepiga kura kituo cha Idara ya maji kilichopo Ikulu, Chamwino.

Magufuli.jpg

MWANDISHI: Unazungumziaje taratibu za upigaji kura katika kituo chako? Mambo yanavyokwenda kwa ujumla, umeridhika?

DKT. MAGUFULI: Napenda niwapongeze watanzania wote kwa kuiona hii siku ya leo ambayo ni siku muhimu sana katika kukuza demokrasia katika Taifa letu, napenda niwapongeze pia wasimamizi wa uchaguzi katika kituo chetu cha hapa Chamwino ambacho mimi nimepiga kura pamoja na mke wangu, maandalizi yalikuwa mazuri, mstari wapiga kura wamejitokeza wengi kwa hiyo nawapongeza kwa usimamizi mzuri ambao unaendelea kufanyika hapa.

Wito wangu kwa Watanzania, tujitokeze kwa wingi katika siku hii ya leo kwenda kupiga kura, twende tukapige kura kwa ajili ya maamuzi ambayo kila mmoja atakuwa nayo katika moyo wake.

Lakini napenda nisisistize amani lazima tuendelee kuitunza kama Taifa kwa sababu kuna maisha hata baada ya uchaguzi, Mungu awabariki wapiga kura wote, Mungu aibariki Tanzania. Asanteni sana watanzania, nami nimeshapiga na kidole changu hiki hapa(Anakionesha), mke wangu nae ameshapiga, tumetimiza wajibu wetu wa kuchagua.

UPDATE
BI. QUEEN SENDIGA WA ADC Party APIGA KURA
Mgombea Urais wa Tanzania kwa Tiketi ya ADC Mhe. Queen Sendiga amepiga kura katika kituo cha UNUNIO Dar es Salaam.

Sendiga.JPG

UPDATE
HASHIM RUNGWE APIGA KURA

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha CHAUMMA Hashim Rungwe amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Ushindi Mikocheni 'B' Kawe jijini Dar es Salaam.

Rungwe.jpg

UPDATE
BERNARD MEMBE APIGA KURA

Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Bernard Membe ametimiza haki yake ya Kikatiba ya kupiga kura katika kijiji cha Chiponda, Lindi
membe.jpg

UPDATE:
PROFESA LIPUMBA APIGA KURA

Mgombea Urais kupitia CUF amepiga kura ktk kituo cha Shule ya Msingi Mtakuja, Dar. Ametoa wito akisema “Wanaosimamia Uchaguzi watende haki, kura zihesabiwe kama zilivyopigwa kusiwe na uchakachuaji

Lipumba.jpg


UPDATE
TUNDU LISSU APIGA KURA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tundu Antiphas Lissu amepiga kura katika Kituo cha Ntewa A, Shule ya Msingi Ntewa, Kata ya Ntuntu, Ikungi, Mkoani Singida

Lissu.jpg
LIC
 
Reserved: Ajili ya PICHA na video mbalimbali

TUNDU LISSU AELEKEA SINGIDA KUPIGA KURA
Lissu.jpg
Mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar es salaam tayari kuelekea Mkoani Singida kushikiri zoezi la upigaji kura.


BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA AWATAKIA KILA LA KHERI WATANZANIA
Today is the day! Kila la kheri to all Tanzanians as they head to the polls to exercise their right to vote. Providing full access to observers and party agents, along with transparent tallying, will give credibility to this process.
Baloz.jpg


IGP SIRRO APIGA KURA, ATOA NENO
 
Back
Top Bottom