Kampeni ya Ghana yatafuna bil 2/-

M

MegaPyne

Guest
WAZIRI wa Habari Utamaduni na Michezo, Muhammed Seif Khatib, amesema serikali imeridhishwa na uongozi bora wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linaloongozwa na Rais Leodgar Tenga.

Akizungumza katika hafla maalum iliyoandaliwa na TFF kuwashukuru Watanzania kwa kuiunga mkono timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, kwenye Ukumbi wa Crystal, uliopo New Africa Hotel, Khatib alisema serikali imeridhishwa na utendaji mzima wa TFF.


Alisema ni taasisi chache nchini, zinazoweza kuthubutu kufanya kama TFF, kuweka wazi mahesabu ya mapato ya fedha, na mchanganuo wake na imeonyesha ni jinsi gani ilivyo na dhamira ya dhati ya kukuza soka.


“Niwapongeze TFF, kwa sababu hili la kutangaza mapato ya fedha hadharani ni jambo gumu, ni watu wachache sana wanaoweza kufanya hivi na TFF mmekuwa mfano, tunawapongeza,” alisema na kuongeza:


“Nilipokwenda kumuomba ruhusa Waziri Mkuu, ili kuhudhuria hafla hii, aliniruhusu kwa sababu ya ukubwa wa tukio lenyewe na inaonyesha jinsi viongozi wa ngazi za juu wanavyoridhishwa na uongozi wa TFF,” alisema Khatib.


Alisema umakini na uwazi wa Tenga, unamfanya akumbuke miaka ya 1975-78, wakati huo wakiwa wote Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kanali mstaafu, Idd Kipingu, walipokuwa wakilala bweni moja, na hakutarajia kama siku moja wangeweza kukutana katika tukio kama hilo.


Aidha, Waziri Khatib alizionya klabu kongwe za Simba na Yanga, kuacha mara moja kuwa vinara katika kukwaza maendeleo ya soka nchini, kwa kukumbatia migogoro isiyokwisha.


“Serikali inakereka kwelikweli kwa migogoro isiyokwisha ya klabu zetu, hasa hizi kongwe, Simba na Yanga, wamekumbatia migogoro kila kukicha, viongozi wanagombana wao kwa wao,” alisema Khatib.


Alisema inashangaza kuona klabu zetu zingali zinakumbatia ushirikina, ambao hauna nafasi yoyote katika karne hii, ya sayansi na teknolojia.


Aidha, alielezea kukerwa kwake na tabia za viongozi kuwanyanyasa wachezaji, ikiwemo kuwapa adhabu kubwa pindi wanapokosa bila kuangalia, chanzo cha makosa hayo.
“Hivi inzi, unampiga nyundo ili kumuua, hii ni sawa?” alihoji Khatib.


Alisema kwa hakika klabu hizo zimekuwa zikikwaza na kukwamisha jitihada za TFF, katika kukuza soka, pamoja na jitihada za Rais Jakaya Kikwete, na serikali yake kuleta makocha kutoka nje ya nchi.


Alisema ujio wa Mbrazil, Marcio Maximo, hautasaidia kitu kama klabu kubwa zitaendelea kung’angania migogoro, na anazishangaa klabu hizo kwa kutotaka kuanzisha timu za vijana, ambazo ndizo zitakazowaletea mafanikio katika soka, siku zijazo.


Khatib alimtaka Maximo kutokata tamaa, kwa vijana wake kushindwa kwenda Ghana, kwani kwa mafanikio waliyoyaonyesha, anaamini siku moja itapata tiketi ya fainali hizo kubwa Afrika.


Aliwataka wachezaji walioteuliwa kuunda timu ya taifa bara, watambue kuwa wamebeba dhamana kubwa ya Watanzania, na wanachokihitaji kutoka kwao ni ushindi, ndiyo maana wako tayari kutoa mamilioni yao ya fedha kuisaidia Stars.


Awali, kabla ya kumkaribisha waziri, Rais wa TFF, Tenga, alisema kwamba nia ya kuandaa hafla hiyo, ni kutaka kuwashukuru wote waliochangia kwa namna moja au nyingine, kusaidia Stars kufikia hapo ilipo.


“Kikubwa kilichotufanya tuwaalike hapa leo (juzi) ni kuja kusema asante kwa wote, waliotuwezesha kufanikisha safari yetu ya miezi 18 ya kusaka tiketi ya kwenda Ghana ambayo tumeikosa,” alisema Tenga.


Alisema amelazimika kufanya hivyo kwa sababu si jambo dogo watu kukubali kutoa mamilioni ya shilingi, kwa ajili ya kuidhamini Stars.


“Kwanza ni serikali, imefanya jambo kubwa sana, mbali ya msaada wa fedha, lakini imewaleta makocha, ambao pia ina dhamana ya kuwalipa mishahara na posho hadi sasa,” alisema Tenga.


Mbali ya serikali, Tenga alitoa shukrani kwa mdhamini mkuu, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Benki ya NMB, Mohammed Enterprises na wote waliotoa michango yao, sambamba na Watanzania waliojitolea kuingia mipirani, wakati wa mechi za Stars.


Alisema michango hiyo, iliyotolewa kwa nyakati tofauti, imeisaidia Tanzania kupiga hatua kisoka licha ya kwamba haikubahatika kukata tiketi ya kwenda Ghana, katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.


Alisema kwa ujumla misaada ya serikali, wadhamini na wafadhili wengine ilifikia kiasi cha sh bil 1.9 wakati viingilio ni sh bil 1.1 huku matumizi yakiwa sh bil 2 na milioni 26 na kusema, wangeweza kuwa na akiba, lakini wakatumia kuandaa timu nyingine.


Alifafanua kuwa, walitakiwa kuziandaa timu za vijana chini ya miaka 23 na 17 na ile ya wanawake, ambazo zilikuwa zikikabiliwa na mashindano na sasa wanasubiri bili za umeme na maji vilivyotumika kwenye uwanja mpya, pamoja na posho za mafundi wa Kichina waliofanikisha mechi hizo.
 

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,144
707
What is 2 bil. Tshs in promotiong our national pride? Do we know how much other countries invest in their national teams? How much money is misused in curruption?

Stil feel 2 Bil. Tshs is not much- it is 0.03% of our annual budget!
 

Mtaalam

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
1,364
205
naah nadhani watu wanaona hilo jus kwa vile imetumika kwenye mpira..they aint see wats behind the mpira and national teams..though yawezekana kuna fungu limeingia kwenye mifuko ya watu lakini i support huyo aonaye bil.2 is kidogo mno..
je tujiulize ni fungu gani ambalo huyo mtalii na vijakazi wake wanalitumia out of the budget?yaan haieleweki fedha zajaje na zatumikaje??lakin wanaweza tumia kwa jus 1day if not siku 3??
can we compare them na hii bil.2 ambayo imetumika kwa more than 100 pipo kwa muda mrefuuu??
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom