Kampeni ya chanjo kwa watoto

Tsidekenu

Senior Member
May 7, 2009
141
41
Bandugu,

Naomba mwenye uelewa anisaidie, mtoto wangu ana mwaka na miezi sita na hivyo alishapata chanjo zote hizi za surua, polio vit a na bcg wakati nampeleka clinic. sasa je anatakiwa kumpeleka tena kwenye chanjo hizi? maana naona kama ni zile zile tu.
 
Bandugu,

Naomba mwenye uelewa anisaidie, mtoto wangu ana mwaka na miezi sita na hivyo alishapata chanjo zote hizi za surua, polio vit a na bcg wakati nampeleka clinic. sasa je anatakiwa kumpeleka tena kwenye chanjo hizi? maana naona kama ni zile zile tu.

nenda nae uwaulize wataalamu palepale
 
Kuwa makini Best! Hawa mapapa wa nchi yetu ni sumu,hayo ni maagano. Be care Best! Achana hiyo biashara!
 
Achana kabisa na hii kitu!...Surua hii imepandikizwa Ngorongoro Umasaini ili watu wakubali kudungwa masindano hayo wanayoita chanjo!...I beg you..kuwa makini...Naamini unaipenda familia yako!
 
Tafadhali mpeleke mwanao pamoja na kuwa alishapata chanjo hizo zote kama ulivyosema. Kama nilivyoelewa mimi ni watoto wote kuanzia miezi Tisa hadi miaka mitano. hayakutolewa maelezo kuwa aliyekwisha pata chanjo hiyo hatakiwi kupelekwa kwa chanjo. Ni "heri uamini hapa duniani kuwa Mungu yuko na ukienda huko ukakuta hayuko hutakuwa umepoteza kitu, lakini ukiamua kusema kuwa hakuna Mungu, na ukienda huko mbinguni ukamkuta kweli yupo na ukiwa hapa duniani ulitenda mabaya kinyume na matakwa ya mwenyezi Mungu utakuwa umeumia kwa kuwa nafasi ya kujiweka sawa ili uishi milele hutaipata" Mpeleke mtoto kwa kuwa imeelekezwa.
 
Nakushauri uende naye utapata maelekezo huko huko kwenye matone. Sithani kama wana nia mbaya na watoto kwa sababu hivi vitu vimekuwa vikitolewa tangu nchi inapata uhuru mpaka, ndio maana vifo vya watoto wachanga vimepungu na idadi ya watu kuongezeka kutoka milinioni 8 mwaka 1961 mpaka 40 m mwaka 2011.
 
Nenda Mkuu. Mimi niko ZNZ na tayari nimempeleka mwanangu. Usiache kwenda. Acha kusikiliza hadithi za mitaani.
 
thanks wote kwa comment zenu, i am just curious you know as whats the loggic ya kuwachanja watoto tena kama walishachanjwa? does that mean zile zinazotolewa clinic sio sawa? na kama ziko sawa kwa nini nimsubject mtoto wangu kwa maumivu tena au hawachomwi sindando ni matone tu? kwa nini wizara ya afya haijazungumzia chochote kuhusu ambao wameshachanjwa tayari wakati wanajua kabisa watoto huwa wanapata hizi chanjo clinic.
 
KAMA UNATAKA WATOTO WAKO WAPUMBAE NA WAPUNGUE UWEZO WA KUFIKIRI WAPELEKE TENA..... CHANJO ZA AWALI ZINATOSHA HIZO NYINGINE NI HASARA TU.... UNAMUHARIBU MTOTO:decision::decision::flame::flame:
 
Je unajua anaenda kupata chanjo gani?
usichanganye hapa fact za chanjo na siasa za mtaani kaka aisee.

chanjo mtu anaweza akapata na pia hata akarudiwa.. sababu za kurudiwa zipo na moja ikiwa kama mtaani kuna maambukizi ya tazizo husika hata kama amepata chanjo anaweza kurudiwa kupewa chanjo kutokana na hali iliyopo mtaani tunaita "Mass treatment"

kama kuankuwa na case nyingi katika kijiji X za mara kwa mara mfano Minyoo kinachofanyika ni kuwapatia watoto wote chanjo husika au mtibabu husika bila kujali anaumwa au haumwi kwa sababu inaonyesha ni watoto fulani wapo katika hatari ya kupata tatizo Hilo.

nakushauri nenda ukapate chanjo, mtoto wa miezi 6 bado bado mdogo sana hata kinga yake haijawa imara kupambana na magonjwa husika.

watoto wote walio katika umri wa chini ya miaka 5 wapo katika hatari zaidi ya kupata magonjwa.
Mpeleke akapate chanjo kwa ustawi wa maisha yake.
 
Back
Top Bottom