Kampeni: Wito kususia biashara za mafisadi

Jamani kimbieni Tanzania nchi inashikiliwa na mafisadi, hamieni sijui wapi?
 
Wandugu tumekuwa sana tukija na data za kuwahusisha wale nugu yetu hosea anasema washika uchumi wa nchi...(MAFISADI).Wengi wametoa maoni yao ..wamejaribu kutoa mawazo yao...nafikiri imefika sasa badala ya kuakaa na kuanza kuandika tuanze kufanya vitendo kwa kuukataa ufisadi wao......BASIL MRAMBA ;ROSTAM AZIZ
wamekuwa na mali nyingi sana ambazo kwa masikitiko wengine tumeendelea kuzikimbilia na hata wengine kuhakikisha wanasionga mbele;;

Pdidy

KATAA UFISADI-- KATAA BASIL MRAMBA-- KATAA PRECISSION AIR

BASIL MRAMBA amkuwa na share nyingi sana pale precission air.najua watanzania wengine watashangaa ila kwa mtazamo wangu kama tunashabikia kufikishwa mahakamani mramba na huku Tunaendelea kupanda PRECISSION AIR;tunajiumiza vichwa wenyewe.....
PESA tunazopigia kelele ndizo zimeleta ndege za precission kuwepo pale..sasa kama ni hilo ningeomba tumsaport na kijana wetu apo chini

KATAA UFISADI-- MKATAE ROSTAM AZIZ--
KATAA KUTUMIA VODACOM

It is too late now but not too late enough.. kama uko kwenye mapambano dhidi ya ufisadi na hauko tayari kusalimu amri, nakushauri kuachilia namba za simu za Vodacom ASAP. As a matter of fact, hamia "kwingine" within the next 72 hours (beginning Monday). Do it or be ready to live with the consequences.

Nilikuwepo.

M.M.

Mkuu;

Umenena. Tuko pamoja.
 
Tutapambana nao kama Nyerere alivyodai Uhuru!

AMEN NA IWE HIVYO KAMA ISAYA 7:7...AKUNA KUWAKIMBIA TENA UKIKUTANA NJIANI MWAMBIE MUNGUA KAMA NILIVYOWAONA LEO HII NISIWAONE TENA MAISHANI MWANGU MATOKEO YAKE WAO NDIPO WATAKUWA WANAKUKIMBIA.......
JINA LA BWANA LIBARIKIWE......
 
Mbona hii idea ilishakuwa conceptualized by utopian socialists kama Robert Owen na wenzake na ikafeli? Waliosoma Wajamaa wa njozi A-level nafikiri wanalijua hili.

Pia hata Mahatma Gandhi alijaribu lakini haikufanya kazi vizuri.

Kwanini mnafikiri itafanya kazi leo kwenye mazingira ya utandawazi ambapo hayo mashirika yamejichanganya mno kuliko hata zamani? Unaweza kukuta humo humo VODACOM hata pesa za maskini kupitia mifuko mbalimbali zimewekwa huko. Unaweza kukuta shirika kama hilo limekopeshwa na hiyo mifuko na likifa ni pigo kwa hata maskini. Unaweza kukuta athari kubwa kwa watu ambao ni maskini, hawana ufisadi na wanafanya kazi kwenye shirika kama hilo.

Kikawaida mashirika kama haya yanapokufa wanaopata madhara zaidi ni watu maskini maana matajiri wanakuwa wa kwanza kuhamisha pesa zao kupeleka kwingine.

Ni muhimu kusoma historia ya nyuma ili kutojiingiza kwenye makosa yale yale ambayo huko nyuma hayakusaidia.
 
Mbona hii idea ilishakuwa conceptualized by utopian socialists kama Robert Owen na wenzake na ikafeli? Waliosoma Wajamaa wa njozi A-level nafikiri wanalijua hili.

Pia hata Mahatma Gandhi alijaribu lakini haikufanya kazi vizuri.

Kwanini mnafikiri itafanya kazi leo kwenye mazingira ya utandawazi ambapo hayo mashirika yamejichanganya mno kuliko hata zamani? Unaweza kukuta humo humo VODACOM hata pesa za maskini kupitia mifuko mbalimbali zimewekwa huko. Unaweza kukuta shirika kama hilo limekopeshwa na hiyo mifuko na likifa ni pigo kwa hata maskini.

Kikawaida mashirika kama haya yanapokufa wanaopata madhara zaidi ni watu maskini maana matajiri wanakuwa wa kwanza kuhamisha pesa zao kupeleka kwingine.

Ni muhimu kusoma historia ya nyuma ili kutojiingiza kwenye makosa yale yale ambayo huko nyuma hayakusaidia.


Mkuu;

Kuna mahali pia nilisoma kuwa njia hii imefaulu sana katika zama hizi. Nitakutafutia reference na kubandika hapa.
 
Acheni hizo. Kwanza si wengine ni brand loyal. Pili kuna ndugu(watz) zenu kibao wanafanya kazi voda. Tatu, mkitaka mfanye zengwe ili RA aporwe hisa zake, si vingine. Mbona Jenerali alifanyiwa zengwe na kuporwa hisa pale habari corp? Think twice
 
Jamani susieni bidhaa za mafisadi ila mjue hamtawaumiza wao, ni sisi ndugu zenu tunaopata riziki huku...sasa wakati mnafikiri kutufanyia unyama huo pia mfikirie namna ya kuzisaidia familia zetu pindi tutakapokosa pahali pa kupatia riziki. Ninauhakika kabisa waliotoa wito huo wengi wako MAJUU na sidhani kama wanafahamu Bongo hakuna ajira na zilizopo ni za hao Mafisadi. Huu mtazamo unafaa huko mliko sio hapa kwetu ambapo familia inaishi kwa kuunga unga na wapo wanaopitisha siku kadhaa bila kutia kitu tumboni.

Siwapingi na kampeni yenu, hata mimi ningekuwa kama nyinyi bila shaka ningekuwa wa kwanza kususia bidhaa za hao walanguzi na mibaka uchumi. Chukulia mfano kampuni kama Quality group, Vodacom, New Habari Corporation na zinginezo zinazomilikiwa na hao Mafisadi zimeajiri watanzania wangapi? Je wakitoka hapo nchi hii itatosha kweli...let's be real people, nilishasema kwenye thread ya Mzee Mwanakijiji kuwa mawazo kama hayo ni ya KIBINAFSI yanawezekana tu ukiwa na Moyo kama wa Bush Jr, Osama Bin Laden na hata waisrael kuhalalisha mauji ya mamia eti kulinda wachache ambao hata kuguswa ni shida.
 
kumbe kwengine anajiita ALLEN? makubwa haya
sasa kuna ubaya gani kutumia jina la sikuzote au noma?
 
Mada kama hii pia imeanzishwa na Mwanakijiji katika thread yake ya "Wanaharakati: Ziachieni simu za Vodacom!".

Nadhani kama jitihada hizi mnazozianzisha zikifanikiwa, mtakuwa mmefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuangamiza Taifa hili. Mtafanikiwa kuifanya Tanzania iwe na sura ya kiuchumi isiyotofautiana sana na Zimbabwe kwa sasa. Mtakuwa mmefanikiwa kuhakikisha kuwa, watoto wadogo wengi wanakufa kuliko kipindi chochote cha nyuma. Mtakuwa mmehakikisha kuwa, usalama waraia na mali zao ni suala lisilo na tiba. Mtakuwa mmefanikiwa kuhakikisha kuwa, watoto wa masikini hawapati tena elimu na wakiipata itakuwa haina maana kwao wala kwa Taifa lao.

Maana yake ni kwamba, mtakuwa mmeumaliza kabisa uchumi wa Taifa hili, na kuurekebisha itakuwa ni kazi isiyoweza kufanyika kwa muda mfupi.

Wakuu, nchi hii inahitaji uangalifu sana katika maamuzi inayochukua. Nchi iko kwenye state ambayo, kama kutatokea jitihada zozote za kudhoofisha uchumi wake, basi uchumi huo ni rahisi sana kuporomoka. Nchi inahitaji wazalendo na uzalendo mkubwa ili walau iweze kulinda maisha na ustawi wa wananchi wake.

Vita dhidi ya UFISADI inaweza kufanikiwa tu endapo itaelekezwa katika vyanzo vya ufisadi. Itakuwa ni jambo la ajabu na hatari kupigana na ugonjwa kwa kuua wagonjwa wote. UFISADI unafanywa na wengi na vyanzo/sababu zake haziongelewi kabisa. Inatakiwa kila mmoja wetu ajue nini hasa kinachosababisha hao tunaowaita mafisadi kufanikiwa kuutekeleza ufisadi wao. Baada ya kuelewa hilo, ndipo kweli tutaweza kuuangamiza ufisadi na kuhakikisha mafisadi wanalipa kutokana na ufisadi wao.

Thread hii na ile ya "Wanaharakati: Ziachieni simu za Vodacom!" zinanitisha kuwa inavyoelekea kama tusipokuwa makini, mwananchi anaeteseka kutokana na ufisadi akaangamia zaidi kwa kutumia nguvu zetu wenyewe tukidhani tunapambana na adui yetu. Tuache hayo ili kuokoa Taifa hili ambalo linaelekea kukosa mwelekeo.

Hatuwezi kuua Panya waliojaa nyumbani kwa kufyatua risasi bila kujali vichanga vilivyolala vyumbani mwetu. Kwa kuwa tu, tuna hasira sana kutokana na madhara ya panya hao.

Tuwe waangalifu zaidi, ndipo tutashinda.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom