Kampeni: Wito kususia biashara za mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni: Wito kususia biashara za mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Allien, May 20, 2009.

 1. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  KAMPENI: WITO KUSUSIA BIASHARA ZA MAFISADI


  Kwa: WanaJF Kwanza na Kisha Watanzania Wote

  Kutoka Kwa: Alien – Mkazi wa Sayari za Mbali

  KAMPENI YA KUSUSIA BIDHAA NA HUDUMA ZA MAFISADI

  Kwa Nini?
  Kwa kuwa Serikali na Vyombo vya Dola vimeshindwa kuwashughulikia mafisadi na Kuwachukulia hatua kali stahiki. Hukuna tena mtu wa kutusaidia. Tumepiga kelele hakuna anyetusikia. Tumelia bado wazeziba masikio. Ndugu zetu wamekufa hakuna anayetuonea huruma.

  Wanachofanya Mafisadi:
  Mafisadi ni watu wanaotumia rasilimali za taifa kwa manufaa yao binafsi. Aidha hutumia madaraka yao vibaya kwa kujinufaisha ama hutumia njia za udanganyifu kuiba pesa za umma kwa manufaa yao binafsi.

  Madhara yanayoletwa na Mafisadi:
  Wengi wamepoteza maisha yao kwa sababu ya Ufisadi. Kuna ambao wameathikika ama moja kwa moja ama kupitia sababu ambayo imesababishwa au kuchangiwa na ufisadi.

  Nini cha Kufanya:
  Inabidi sasa tujipange vema kupinga ufisadi kwani tumeachwa kama watoto yatima ambao wazazi wao walishafariki na kuchukuliwa na mlezi ambaye pia amekabidhiwa mali ya watoto lakini akaanza kujinufaisha yeye na nafsi yake.

  Kwa namna gani?
  Kwa kususia bidhaa na huduma zote zinazotolewa na makampuni yanayomilikiwa na mafisadi hata kama ina maana kwa kufanya hivyo tutaabika. Hii itawafanya watambue kuwa sasa imefika mahali hatukubali tena. Hii pia itasaidia kuvunja vunja nguvu zao za kifisadi na kiuchumi kwa kiasi fulani.

  Nini tena?
  Tubuni na mikakati mingine ambayo pia itasaidia kuhakikisha mafisadi wote wanadhibitiwa kwa nguvu ya umma.

  Tushiriki Vipi?
  Kwanza kila Mwana JF asign katika thread hii na kuonyesha kiasi gani anunchukia UFISADI. Kisha ashiriki kwa vitendo katika kususia bidhaa na huduma zote zinazotolewa na makampuni yanayomilikiwa na mafisadi.

  Nitajuaje Huduma na Bidhaa Zao?
  Kila asomaye hapa na aandike kwa Uhakika Makampuni yote Yanayomilikiwa na Mafisadi kwa Majina na Kutaja wamiliki wake na Ufisadi Uliofanywa.

  Baada ya Hapo?
  Sambaza Waraka huu kupitia barua pepe na njia nyingine zote zinazoweza kufanikisha kufikisha ujumbe huu kwa Wananchi Wote wa Tanzania.

  Kampeni Inaanza Lini?
  Natoa Mwito Kampeni hii ianze Tarehe 01-06-2009

  Mungu Ibariki Tanzania
   

  Attached Files:

  Last edited: May 20, 2009
 2. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Usemacho ni kweli hii njia kw kiasi fulani inaweza kusaidia japo wataumia baada ya muda kwani hela wanazotumia baadhi yao kama RA hategemei biashara zake zipo kama bosheni.

  MIMI NATOLEA MFANO RA anamiliki New HABARI Corporation ambayo ina magazeti kama The African, Bingwa, Rai, Mtanzania na Dimba. Mimi nilishaacha kununua magazeti yake.

  Baadaye nikasikia yuko Vodacom huko ndiyo najiandaa kutoka niende kwenye mtandao labda wa TTCL. Japo network yake haipo makini sana. Maana hawa Zain nao ni mafisadi kwa hii kampuni ilizaliwa kijanjajanja, hela zetu zimeliwa.

  Hivyo ni kweli cheche hizi zikipelekwa uswazi nafikiri tunaweza kufanikiwa kwa asimilia fulani.

  Lakini pia na wewe ungetuwekea mifano yako michache.
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tususie bidhaa za Reginald Abraham Mengi kwani yeye ndio Nyangumi wa ufisadi Tanzania
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana JF wenye majina ya kampuni za mafisadi na wamiliki wao wayaweke wazi ili kufanikisha zoezi la kususia bidhaa na huduma zao.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Tuko pamoja sana kama samaki na maji.

  Haitawaumiza sana , lakini at least watakuwa wamepata kionjo cha

  HISIA zetu. Unity is stergnth! C'mon people!
   
 6. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamaa kasema tuweke mifano ya wazi hivyo kama mengi ni nyangumi weka makampuni yake ili watu tuyajue tuyapige chini. Siyo kututajia mtu kwani wote tunamjua humu.
   
 7. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Asante Mkuu;

  Tuko pamoja. Nina namba ya Voda lakini sasa nimenunua ya TTCL. Tarehe 01-06-2009 Naachana na line ya Voda. Ila itabidi nifanye kazi ya ziada maana kampuni yangu maofisa wote wanatumia Voda.

  Bidhaa za nje mimi nilishazisusia siku nyingi mpaka iwe hakuna namna. Nanunua za Kitanzania tu ingawa ubora wakati mwingine si mzuri. Lakini kila ninapotumia najisikia kutosheka kuwa nimetimiza wajibu wangu wa Kizalendo.
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Unaishi dunia gani? kama huyajui makampuni ya Mengi then ur in the wrong forum try Michuzi au hata darhotwire!
   
 9. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Masatu; hii ni kampeni na nivizuri tuwe makini katika kuhamasishana. Ni vema ukataja makampuni, bidhaa, wamiliki na ni kwa nini unafikiri na Mafisadi.
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kindly refer to the post #8 pls...
   
 11. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Masatu;

  Ubishi na ushindani hautatusaidia kitu katika hii kampeni. Please soma thread kuu kwa makini. Si kila mtu anajua hapa biashara zote za mengi au bidhaa na huduma zake ni nini.

  Utakuwa umetenda haki kama utataja makampuni yake yanayofanya ufisadi na ni nini kisusiwe. Simple and clear. Sasa malumbano ya nini na sisi tuko katika kampeni.

  Please tusiivuruge thread. Heshimu thread kuu unless kama una argument za msingi za ku-criticise of which unakaribishwa kuzitoa.
   
 12. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  I think ur the one who should go there b'se even allen i think he knows the fisadis lakini kaleta thread yake ili watu wachangie may be something new can come out. But others who think they're smart like you wanathani watu wote wanajua kila kitu. Tuko tofauti kama ulijua huwezi kutaja makampuni then hukutakiwa kutaja hata hilo jina. Because ur the one who mentioned mengi.

  Je huko kwa michuzi ndiyo kuna thead inayotaja makampuni ya mengi? Je kama sijui utakuwa umenisaidia vipi? People have different interests labda yako ni mengi na yangu ni RA na wengine. Je nitajua makampuni ya mengi?

  Toa uswahili taja makampuni...
   
 13. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Fafanua unyangumi wa ufisadi wa mengi si kutaja tuu.Ufisadi papa wa Rostam Aziz ni KAGODA,EPA,RICHMOND,TTCL na DOWANS.
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Kama ni ubishi wewe ndio unaouleta sasa. Kwenye post yako unakiri kuwa "kila mtu anazijua biashara za Mengi" sasa kama zinajulikana ya nini tena kuzitaja? huoni ni kujaza bandwith bure. On the same note, nadhani ww ndio unatakiwa ukasome kichwa cha habari cha thread labda kwa kukusaidia kinasema hivi " Kampeni: Wito kususia biashara za mafisadi" ( msisitizo wangu) kwa maneno mengine jukumu la kwanza ni kumjua fisadi (jina) tukishampata ( tushampata ) then kinachofuata ni kususia bidhaa zake ( Kila mtu anazijua )

  Got it?
   
 15. M

  Masatu JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Kindly refer post #14....
   
 16. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ...Alafu tununue bidhaa/huduma za nani aliye 'safi' Tanzania??Watu wenyewe tumeambiwa hawazidi kumi Tanzania,Swala la kujiuliza ni je; wakaamua wao 'kususa',Tuna mbinu mbadala??
   
 17. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Kazi kweli kweli . . . .

  Masatu hakuna mahali ambapo nimeandika "Kila Mtu anazijua biashara za Mengi". Usijekuwa unaquote wengine unasema ni Allien.

  Hata kwa kutumia akili ya kawaida, kama hii ni kampeni ya kitaifa, je kila mtu anajua bidhaa za Mengi ni zipi na makampuni yake ni yapi?

  Angalia moja ya extracts ya post yangu:

  "Nitajuaje Huduma na Bidhaa Zao?
  Kila asomaye hapa na aandike kwa Uhakika Makampuni yote Yanayomilikiwa na Mafisadi kwa Majina na Kutaja wamiliki wake na Ufisadi Uliofanywa"
   
 18. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Wandugu,

  Kama kususia magazeti yote ya New Habari Corp kutasadia kwa namna moja au nyongine mimi naunga mkono...ufisadi ni lazima upigwe vita na kila mtu kulingana na uwezo wake. Mimi uwezo wangu unaishia kwenye kutokununua magazeti yote ya New Habari Corp, wengine wataweza kususia line ya Vodacom n.k kila mmoja kwa nafasi yake; infact I feel good kususia bidhaa za RA..!!

  RA hana biashara nyingine anazozimiliki kwa proxy zinazojulikana...naamini sio Vodacom na NHC peke yake.

  June 1st 2009..susia kununua bidhaa au kutumia huduma yoyote inayotolewa na kampuni zinazomilikiwa na RA "unazozifahamu" kwa kadri utakavoweza.
   
 19. M

  Masatu JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hilo linahitaji thread nyingine ya " Kampeni: Wito wa kununua bidhaa za wafanyabiashara safi" Tunaomba usituharibie thread hapa ni kampeni kwa wafanyabiashara mafisadi
   
 20. M

  Masatu JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Allien, Ngoja nikufahamishe vizuri unajua sisi tuliosomea ualimu tuna namna nyingi za kufikisha ujumbe.

  Ipo hivi wewe mwenyewe kwa kauli yako umekiri hapa kuwa "si kila mtu anajua bidhaa za Mengi" thats goes without saying kuwa kuna portion ya watu wanazijua b idhaa za Mengi na mimi ninawa address hao.

  Upo hapo?
   
Loading...