Kampeni Ushetu; Baadhi ya nukuu za Katibu wa NEC itikadi na uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,893
940
NUKUU: BAADHI YA NUKUU ZA KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM SHAKA HAMDU SHAKA-KAMPENI USHETU.

"Wananchi ninazo taarifa juu ya vitendo viovu vya kupambikiziwa kesi za kukamatwa na bangi vijana na wanawake vinavyofanywa na baadhi ya askari wetu wasio waaminifu wanaotaka kulitoa doa jeshi letu la Polisi, hili halikubaliki"

"CCM haitakubali kuona wananchi kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu wakiishi kama vile wao ni wakimbizi katika nchi yao. TFS acheni uonevu na unyanyasaji wa wananchi wanaopakana na misitu hususani hapa Jimbo la Ushetu"

"Kibaya zaidi wanapowafikisha watuhumiwa polisi, hawawapeleki hata mahakamani wanatoza faini hazina stakabadhi, niwakikishie wananchi Serikali CCM inayongozwa na Rais Samia haitavumilia jambo hili tunasimama upande wenu, kuweni na amani endeleni kutiii sheria bila shurti".

"Chama Cha Mapinduzi tutazungumza na IGP leo hii jicho lake liangalie wilaya ya Kahama haiwezekani wananchi wako kwenye nchi huru leo hii wakafanywa wanaishi kama wakimbizi kwa vitu vya kusingiziana na kubambikiziana kesi kubwa na zito"

"Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu wakala wa misitu (TFS) kupiga wananchi hadi kuwavunja miguu na kisingizo cha kuwakamata na mkaa ama kuwabambikia kesi zizizo msingi. Iwe mwanzo na mwisho, serikali ya Mama Samia imejipambane tusimamie sheria bila mateso".

"Chama Cha Mapinduzi kitamuelekeza Waziri wa Utalii juu ya kadhia hii wakishawamaliza vijana wote kuwavunja miguu,nguvu kazi ya Taifa itatoka wapi?Nyakati zote Rais Samia amekuwa akisimama na wananchi hatuwezi kufumbia macho uchonganishi huu kwa kisingizio eti kuvunja sheria"

"Jumamosi tarehe 9 Oktoba, 2021 ili akashirikiane na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wanaushetu mchaguenu Emmanuel Cherehani anatosha na amekidhi vigezo na viwango vya kuwa mbunge wenu".

kjTT3AUv_400x400.jpg
 
Zina msaada katika kutupunguzia madhila ya tozo na gharama za ongezeko la kimywa kimya ya gharama za bundle za data.Hata tushawishike kutumia bundle za maumivu kufuatia nukuu hizo?
 
NUKUU: BAADHI YA NUKUU ZA KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM SHAKA HAMDU SHAKA-KAMPENI USHETU.

"Wananchi ninazo taarifa juu ya vitendo viovu vya kupambikiziwa kesi za kukamatwa na bangi vijana na wanawake vinavyofanywa na baadhi ya askari wetu wasio waaminifu wanaotaka kulitoa doa jeshi letu la Polisi, hili halikubaliki"

"CCM haitakubali kuona wananchi kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu wakiishi kama vile wao ni wakimbizi katika nchi yao. TFS acheni uonevu na unyanyasaji wa wananchi wanaopakana na misitu hususani hapa Jimbo la Ushetu"

"Kibaya zaidi wanapowafikisha watuhumiwa polisi, hawawapeleki hata mahakamani wanatoza faini hazina stakabadhi, niwakikishie wananchi Serikali CCM inayongozwa na Rais Samia haitavumilia jambo hili tunasimama upande wenu, kuweni na amani endeleni kutiii sheria bila shurti".

"Chama Cha Mapinduzi tutazungumza na IGP leo hii jicho lake liangalie wilaya ya Kahama haiwezekani wananchi wako kwenye nchi huru leo hii wakafanywa wanaishi kama wakimbizi kwa vitu vya kusingiziana na kubambikiziana kesi kubwa na zito"

"Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu wakala wa misitu (TFS) kupiga wananchi hadi kuwavunja miguu na kisingizo cha kuwakamata na mkaa ama kuwabambikia kesi zizizo msingi. Iwe mwanzo na mwisho, serikali ya Mama Samia imejipambane tusimamie sheria bila mateso".

"Chama Cha Mapinduzi kitamuelekeza Waziri wa Utalii juu ya kadhia hii wakishawamaliza vijana wote kuwavunja miguu,nguvu kazi ya Taifa itatoka wapi?Nyakati zote Rais Samia amekuwa akisimama na wananchi hatuwezi kufumbia macho uchonganishi huu kwa kisingizio eti kuvunja sheria"

"Jumamosi tarehe 9 Oktoba, 2021 ili akashirikiane na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wanaushetu mchaguenu Emmanuel Cherehani anatosha na amekidhi vigezo na viwango vya kuwa mbunge wenu".
View attachment 1968241View attachment 1968242
IMG_20211008_171157_118.jpg
 
Hiki cheo kapewa mtu dhaifu Sana na hajulikani hata akisema hakuna anayesikiliza Labda wewe uliyeanzisha Uzi.
Enzi za akina Nape na hata Polepole watu walikuwa wanawafuatilia wanachoongea.
 
60yrs ya kututawala sio kutuongoza na ahadi after ahadi!utekelezaji upo wapi?pls njoo kwetu huku Lingusenguse ushangae kuwa maisha yamesimama!
 
Miaka yote hio ilkuwa ikiongozwa na chama gani!?,leo shaka anataka awafumbe macho wasukuma,ili kesho wakachague tena uonevu?!
 
Mbona uchaguzi umepoa Sana?

Hauna ushindani yaani.

Enzi zile CCM yote ingehamia jimboni!
 
Back
Top Bottom