Elections 2010 Kampeni: Nyumba kwa Nyumba

Jafar

JF-Expert Member
Nov 3, 2006
1,136
52
Jana nilibahatika kukutana na kiongozi mmoja wa CCM wa eneo la Ilala National Housing /Msimbazi, nikawa namcharura kuhusu mikutano yao ya kubeba watu na mabasi zaidi ya 17 kuwapeleka kusikiliza kampeni za JK kama walivyofanya pale Mbagala Zakhem siku mgonjwa JK alipohutubia. Akanijibu mbona hata wapinzani wanafanya mbinu hiyo, any way sikubisha sana kwa sababu nilikuwa sina data hizo. Katika maongezi yetu mafupi pia nilimlaumu kuwavalisha boda-boda fulana za CCM halafu kuwalipa kwa kuwajazia vimafuta kidogo.

Jambo ambalo hasa lilinishangaza na hasa ndio sababu ya kuandika ujumbe huu, huyu mheshimiwa wa CCM alinionesha karatasi (ratiba ndefu) iliyochapishwa ya majina ya kaya alizonazo katika eneo lote la Ilala mchikichini mpaka kule buguruni yenye ratiba ya siri ya kuwapitia hawa watu Nyumba kwa Nyumba kufanya kampeni, ratiba ilionesha muda wa kuanzia saa moja usiku na wakati mwingine anasema wakiona kuwa huo muda kuna watu wengi ambao wanaweza kuwaona wanafanya saa saba au nane za usiku. Nilitamani nimuibie hiyo ripoti lakini naye akawa mjanja akaniambia angalia tu jinsi tunavyojidhatiti kuumaliza upinzani.

Sikujua kama CCM ina aina hii ya kampeni, swali: Je ratiba hii tume wanayo?
 
Kwani CCM na Hiyo TUME kuna tofauti gani?!. CCM ndo Tume, Tume ndo CCM. Fungua machooo:glasses-nerdy:
 
Kwani CCM na Hiyo TUME kuna tofauti gani?!. CCM ndo Tume, Tume ndo CCM. Fungua machooo:glasses-nerdy:

Ilala kumejaa mashombe-shombe na mashombeshombe wote ni CCM.

Tatizo ni hao wenzangu na mimi wenye ngozi nyeusi kama yangu na kipato cha ku-unga-unga na wao wamekuwa na akili za hovyo kama mashombeshombe.
 
Nadhani wakija kwangu watakimbia wenyewe.Maana hata mabosi wamekataa mdahalo.Yaani wakija tu ujue wanataka kukikana cha chao.Kimefanya madudu mengi na hakisafisjiki.
 
Ilala kumejaa mashombe-shombe na mashombeshombe wote ni CCM.

Tatizo ni hao wenzangu na mimi wenye ngozi nyeusi kama yangu na kipato cha ku-unga-unga na wao wamekuwa na akili za hovyo kama mashombeshombe.

Hapa ndiyo umafia wa sisiemu huanzia, wataangalia kaya zenye upinzani watawafuata kwa pesa au vitisho na ikiwezekana watavinunua au kunyang'anya vitambulisho vya kura na kuwarudishia mara baada ya uchaguzi!
Tunahitaji kuwaumbua hao wazee wa sisiemu, Jeuri ya ni pesa na vitisho kwa watu wasiyo jua haki zao. Mtu mmoja mwenye kujua mambo kama sisi tunatosha kulinda mitaa yete na hivi vizee. ikibidi tuwashawishi wale hizo pesa na kura hamna. Pia njia nzuri ni kuwapiga zengwe maana wale wazee hula zaidi ya 90% ya pesa za sisiemu na kuwapa walalahoi hivyo vijicenti. Tuwambie wawadai dau kubwa kama hawatakataa na mchezo kuishia hapo hapo!
 
Back
Top Bottom