Kampeni Marekani: Palin ageuzwa **** na akina ze-komedi wa Canada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni Marekani: Palin ageuzwa **** na akina ze-komedi wa Canada

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, Nov 2, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,103
  Likes Received: 5,563
  Trophy Points: 280
  TORONTO, Canada

  KATIKA vituko vya mwisho mwisho kwenye kampeni za urais nchini Marekani, mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti kwa tiketi ya Republican, Sarah Palin Jumamosi alijikuta akipokea simu kutoka kwa mchekeshaji maarufu wa Canada aliyejifanya kuwa ni Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.


  Palin alijikuta akieleza hisia zake katika mazungumzo hayo ya simu yaliyodumu kwa dakika sita na kuweka bayana kuwa siku moja ataweza kuwa rais mzuri.


  "Labda katika miaka nane ijayo," alisema Palin huku akicheka huku akieleza ni kwa kiasi gani anamfurahia Sarkozy na mkewe, Carla Bruni ambaye ni mwanamitindo.


  "Kwa kweli tunakuheshimu mimi na (mgombea urais, John) McCain. Na ninakushukuru kwa hatua yako ya kutumia muda wako kuzungumza nami," Palin alimweleza rais huyo feki wa Ufaransa.


  Mgombea huyo wa nafasi ya makamu wa rais kupitia chama cha Republican alizungumza na rais huyo 'feki' wa Ufaransa juu ya mambo kadhaa, ikiwemo kuwinda pamoja na Makamu wa Rais Dick Cheney, na mke wa Sarkozy, katika mazungumzo hayo ya simu ambayo yalirekodiwa na ambayo yatarushwa hewani na stesheni moja ya redio ya mjini Quebec.


  Msemaji wa kambi ya kampeni ya Palin, Tracey Schmitt alithibitisha kuwa mgombea huyo alipokea simu hiyo.


  "Gavana Palin kidogo alishangazwa kujiona kuwa ameshafikia hadhi ya marais wa nchi, akiwemo Rais Sarkozy na watu wengine maarufu, kutokana na kuwindwa na watu hao wa mzaha. C'est la vie (maisha ndivyo yalivyo)," alisema.


  Simu hiyo ilipigwa na wachekeshaji maarufu wa jijini Montreal, Marc-Antoine Audette na Sebastien Trudel. Wachekeshaji hao ambao wanajiita Masked Avengers, wanajulikana kwa usumbufu wao hasa wa kupiga simu za mzaha kwa marais na watu wengine maarufu.


  Audette, aliyeigiza kama Rais Sarkozy, alizungumza kwa lufudhi ya Kifaransa na wakati fulani alitumbukiza maneno yaliyoonyesha kuwa mazungumzo hayo ni mzaha. Lakini Palin alionekana kutogundua.


  Alimwambia Palin kuwa mmoja wa marafiki zake wa zamani anawinda na kwamba pia ni mpenzi wa gavana huyo wa Alaska ambaye ana umri wa miaka 44.


  "Mimi hupenda kuua hao wanyama. Mmm, mmm, kuondoa maisha, ni kitu cha kufurahisha," alisema rais huyo feki wa Ufaransa.


  Alishauri waende kuwinda pamoja kwa helikopta, kitu ambacho alisema hajawahi kukifanya.


  "Ndio, nafikiri tunaweza kufurahia sana tukiwa pamoja wakati tukifanya mambo," alijibu Palin. "Tunaweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja."


  Mchekeshaji huyo alisema kwa mzaha kuwa hawatakiwi kwenda na Cheney kuwinda, akikumbushia tukio la mwaka 2006 ambalo makamu huyo wa rais alimpiga risasi na kumjeruhi rafiki yake wakati wa kuwinda.


  "Nitapigwa risasi," alijibu Palin.


  Akikebehi maneno ya Palin yaliyorushwa sana kwenye televisheni kuwa mgombea huyo wa nafasi ya makamu wa rais anajua sana siasa za nje kwa sababu "unaweza kuiona Russia kutoka hapa Alaska," mpigaji simu huyo alimwambia Palin akisema: "Unajua tuna mambo mengi tunayoshabihiana pia, kwa sababu... kutoka hapa nyumbani kwangu, naweza kuiona Ubelgiji."


  Msanii huyo wa Canada pia alisema kuwa mke wa rais Sarkozy, Carla Bruni ni mtu anayempenda sana Palin na amepanga kumuimbia wimbo maalum wenye jina alilolitafisri kwa kiingereza kuwa ni “Lipstic On a Pig”, lakini bado Palin hakutambua mzaha huo.


  “Tulikuwa tukitaka kujua uwezo wake... ni kwa kiasi gani anajua masuala ya mahusiano ya kimataifa. Kama ulivyosikia mwenyewe, hapa hakuna kitu,” alieleza mchekeshaji huyo Audette, alipozunguma na kituo cha televisheni cha Skynews.


  Kambi ya kampeni ya Palin ilitoa taarifa ya kulaumu kitendo hicho na kusema kuwa gavana huyo alilazimika kupokea simu hiyo na kufany
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,203
  Trophy Points: 280
  Kwa vile lengo la Tanzania, Africa ya Mashariki na Bara zima la Afrika tuko nyuma ya Obama, jinsi Palin anavyochemsha ni kuvuja kwa pakacha kwa kambi ya Obama.
   
Loading...