Natamani kupiga kura ingekua lazima. Usipo chagua mgombea A au B au C unatumbukiza kura katika sanduku la 'Hakuna nnaemchagua'
Natamani utambulisho wa mpigaji kura ungekuwa kwa nchi/mkoa/wilaya/tarafa/kata/kijiji/mtaa au kitongoji/ubalozi/kaya.
Natamani kabla ya kupiga kura kuwe na siku za wananchi kuchunguza kama raia wote husika wamo katika orodha na kwamba wanajulikana.
Natamani kuwe na uhakiki nani hakupiga kura na kushulikiwa kisheria baada ya uchaguzi.
Natamani Rais aliyekuwa madarakani anapo gombea asiwe na hicho cheo. Awe na hadhi sawa na wagombea wengine.
Natamani matokeo ya uchaguzi yaweze kuhakikiwa na wawakilishi wa wagombea kwa uangalizi wa .....Tume kuwa mshuhudiaji tu.
Natamani matokeo ya kura za urais yaweze kupimwa uhalali kwa mkata rufaa.
Natamani kipindi cha kampeni viongozi wachaguliwa wasi ruhusiwe kutumia majukwaa ya kampeni kufanya kazi yoyote ya kiserikali.
Mkikataa mawazo hayo. Natamani tuwe tunapiga kura za mlolongo. Mnapiga mstari kwa mgombea mnae mpenda na kupata matokeo hapo hapo.
Mnaweza boresha, lakini sina imani na mfumo wa sasa wa uchaguzi.
Hapo sija andika tusi hata moja!