Kampeni dhidi ya Mkapa asishinde Tuzo ya uongozi bora

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
56
Haya Jamani,

Zimebakia siku chache kabla ya Mshindi wa tuzo ya uongozi bora Afrika atangazwe. Mshindi huyo si tu atapata ujiko wa kuitwa kiongozi bora Afrika, ila pia atashinda tuzo ya mabilioni ya shilingi.

Kati ya majina ya maraisi wastaafu 11 wa Afrika ambao wametajwa kushiriki, Rais wetu mstaafu Benjamin W Mkapa ni miongoni mwao na kwa wale mnaofahamu siasa za dunia, Mkapa pia ana nafasi ya kushinda.

Zitto alianzisha thread hapa zamani kidogo kuuliza maoni yetu kuhusu Mkapa kushinda hiyo tuzo. Juzi Bubu aliweka story ya BBC iliyoelezea kwa kiasi kuhusu hiyo tuzo. Inaonekana hii ni big deal (au hata kama sio big deal, mimi naiona hivyo).

Mimi nakampeni dhidi ya Mkapa ili ashindwe. Najua maneno yangu hayatasaidia ila yatasikika hapa na kwa waandaji nitakaowatumia email kuhusu hili. Mkapa ameonyesha kiburi cha hali ya juu sana.

piece ya habari hii kama ilivyo kwenye bbc...

As former African leaders wait to see who has won the Mo Ibrahim prize for good governance, BBC world affairs correspondent Mark Doyle finds Mozambique ex-President Joaquim Chissano's shock and amusement at the value of the prize endearing.
"It's worth how much? Five MILLION dollars?"

.....

The winner of the Mo Ibrahim prize for African governance is to be announced on 22 October at a ceremony in London hosted by former UN Secretary General Kofi Annan.

Sudanese businessman Mo Ibrahim is sponsoring the prize

....

The idea is to encourage democracy, transparency and decency.

All 11 former presidents who left office in Africa in 2004, 2005 or 2006 are automatically eligible for consideration.

A spokesman for Mo Ibrahim said the "long list" of candidates (i.e. the list of eligibles who have not been selected in any way by the judges) was, in no particular order:


Mathieu Kerekou (Benin)
Azali Assoumani (Comoros)
Domitien Ndayizeye (Burundi)
Henrique Rosa (Guinea Bissau)
Maaouya Ould Sid'Ahmed Taya (Mauritania)
Joaquim Chissano (Mozambique)
Sam Nujoma (Namibia)
Benjamin Mkapa (Tanzania)
Abass Bonfoh (Togo)
Gnassingbe Eyadema (Togo)
Bakili Muluzi (Malawi)
France-Albert Rene (Seychelles)
Abdiqassim Salad Hassan (Somalia)

.....

Source bbc....

Ninajua kuna mengi mazuri Mkapa ameifanyia Tanzania ila vitendo vyake na tabia zake za kipindi cha pili cha utawala wake vinatia aibu. Haya majibu yake ya dharau yanasononesha mioyo.

Mkapa, haufai kupewa tuzo ya uongozi bora Afrika. Umeitia aibu nchi yako na umemsaliti Nyerere aliyekuweka madarakani.
 
Hawezi kupata hata bila ya kampeni. Huyo Mo sio mjinga na anafahamu uchafu wa rais wetu Mkapa. Chisano atachukua mark my word.
 
waliotayarisha hiyo tuzo natarajia sio wazembe kiasi cha kumchagua bwana benjamini.

ila kama kuna uwezo wa sisi watanzania kumpigia kampeni ya kuhakikisha hafikiriwi hata kwenye tatu bora, na iletwe, najua waunga mkono watakuwa wengi.

kama kuna mtu anaweza kuirusha kwenye vyombo vya habari vya nje kuwa watanzania hawataki (maoni ya kutokutaka yakishakutolewa) benjamini apate, natarajia itasaidia japo kidogo
 
lakini mkumbuke kuwa wao watakuwa wanaangalia mabo gani muhimu kiongozi huyo aliyeifanyia nchi yake..hasa ki uchumi na ukumbuke bwan Mk.alishusha na ku control inflation na kuinua uchumi wetu kwa kiasi chake kulinganisha na alivyo ikuta..so wanaweza mpa..kama ufisadi na mambo ya rushwa hakuna kiongozi ambaye duniani akishakuwa raisi utegemee akae madarakani awe clean labda mnipe mfano wa huyo kiongozi..hata Mfalme Daudi mwenyewe enzi hizo he was mtu wa Mungu lakiniii......

pia nikiangalia jopo la ma judge wenyewe tuu napata hofu kuwa chinga wetu anaweza shinda!!!lets wait n see tym will tell
 
Wala hamtafanikiwa maana dua zenu ni za kuku haliwezi kumpata kunguru!

BWM amefanya mengi sana hapa bongo, amerekebisha uchumi, ameacha ma fedha kibao hazina sijui mnataka nini hasa!
 
Kutokana na tamaa yake aliyo onyesha akiwa Ikulu haswa katika muhula wa pili, na dharau kwa vyombo vya habari na umma kwa ujumla kuhusiana na kujibu tuhuma hizo hizo anayoonyesha, nami si 'msupport' apate hiyo tuzo.

Hakika katika moyo wangu ningependa sana Mh. Mkapa apokee hiyo tuzo. Pia ni kiongozi ambaye nilimwamini kweli kweli alipoingia madarakani... lakini leo hii ana aibisha kwa kweli. Sifa zote ambazo angeweza kupokea kama kiongozi mmojawapo bora Afrika na duniani kote kazitelekeza kutokana na tamaa, na haswa kama habari nyingi zinavyosema, tamaa ya Mama Mkapa. Ni aibu kuona the fruits of his early hard labour that would have been beneficial to Tanzania and Iconic to the whole society are 'trodden and let to rot' by influences of one in his family! Shame shame shame.

SteveD.
 
Naunga mkono Mkapa asipewe hiyo tuzo,kaua demokrasia Tanzania,katuingiza mkenge,hafai,hafai,jamani itakua aibu akipata hiyo tuzo.Mwafrika wa kike tunaomba ufikishe huo ujumbe ili wamuengue mapema asifike hata 5 bora.
 
nothing will influence yeye kupewa ama kutopewa zawadi yake, pengine hadi sasa hivi mwenyewe keshajua atapata hiyo zawazi bado kuaacept tu ! keep haiting !
 
Tunaomba ukiwaandikia hiyo mail,taja madudu yake yote,mfano ununuzi wa ndege,radar,mauaji ya pemba,wizi na kashfa nzito katika uongozi wake.
 
..mimi nadhani kampeni ya namna hiyo haitakuwa kwa maslahi yetu Watanzania.

..nafikiri hizo pesa,ikiwa atapewa, zina masharti kwamba zitatumika ktk projects ndani ya Tanzania.

SteveD said:
Sifa zote ambazo angeweza kupokea kama kiongozi mmojawapo bora Afrika na duniani kote kazitelekeza kutokana na tamaa, na haswa kama habari nyingi zinavyosema, tamaa ya Mama Mkapa.

Mkapa kwa KIBURI na KUJIAMINI kwake si mtu wa kuburuzwa kufanya jambo asilokubaliana nalo. Kwa msingi huo haiyumkiniki kwamba Mama Mkapa ndiye aliyemlazimisha Mkapa kukiuka maadili ya kazi yake.

Kama mnataka kumshtaki Mama Mkapa instead of Mzee Mkapa basi endeleeni...
 
..mimi nadhani kampeni ya namna hiyo haitakuwa kwa maslahi yetu Watanzania.

..nafikiri hizo pesa,ikiwa atapewa, zina masharti kwamba zitatumika ktk projects ndani ya Tanzania.



Mkapa kwa KIBURI na KUJIAMINI kwake si mtu wa kuburuzwa kufanya jambo asilokubaliana nalo. Kwa msingi huo haiyumkiniki kwamba Mama Mkapa ndiye aliyemlazimisha Mkapa kukiuka maadili ya kazi yake.

Kama mnataka kumshtaki Mama Mkapa instead of Mzee Mkapa basi endeleeni...
JokaKuu, kwa hiyo unakubaliana kuwa kuna 'jambo la tamaa' ambalo linamhusu yeye au member wa familia yake lililofanya kashfa zinazotajwa zimlenge yeye?!

SteveD.
 
Utamaduni wa vigogo kulindana ndio umeifikisha nchi mahali ilipo. I was expecting wale woote waliokataa tuhuma za ufisadi + Mzee Mkapa kuwa wameshafungua mashtaka. Badala yake they are going cold. People...we need to put pressure on them. I tell you, makelele yetu yakizidi they will come out one at a time. Lets keep this fire going kwa sababu I am sick of these BUSTARDS. Wanatoa ahadi nzuri wanapopita kuomba kura 'kula' and then wanageuka wanakuwa na JEURI na CHOYO na UBINAFSI. Hawatufai hawa. CCM and its leaders gotta go..and that day is coming soon
 
Ebu tuangalie vigezo vya ushindi (according to Thisday)

THE Mo Ibrahim Foundation will next week award over $5m (approx. 6.5bn/-) to one former African head of state adjudged to have demonstrated exemplary leadership. And Tanzania’s immediate former president Benjamin Mkapa is in the running for what organisers of the award call ’the world’s biggest prize’ said:
Tuanze na kigezo cha kwanza -Democracy. Tujiulize kwanza what is democracy.... According to http://dictionary.reference.com/ democracy is
1. government by the people; a form of government in which the supreme power is vested in the people and exercised directly by them or by their elected agents under a free electoral system.
2. a state having such a form of government
3. a state of society characterized by formal equality of rights and privileges.
4. political or social equality; democratic spirit.
5. the common people of a community as distinguished from any privileged class; the common people with respect to their political power.

Wana JF tunampa maksi ngapi?

Tukija kwenye kigezo cha pili - transparency.
Transparency is The full, accurate, and timely disclosure of information.... (Reference dictionary.reference.com)
Je, kwa habari zinazoendelea sasa hivi nchini kwetu, sisi wana JF tunampa maksi ngapi?

Tukija kwenye kigezo cha mwisho cha tatu - good governance.
Kwa kutumia reference ya wikipedia http://en.wikipedia.org/wiki/Good_governance

Good governance can be understood as a set of 8 major characteristics:

-participation,
-rule of law,
-transparency,
-responsiveness,
-consensus orientation,
-equity and inclusiveness,
-effectiveness and efficiency
-accountability.

These characteristics assure that
-corruption is minimized,
-the views of minorities are taken into account and
-that the voices of the most vulnerable in society are heard in decision-making

Je wana JF mnampa maksi ngapi?

Ukiniuliza mimi nitampa ngapi, I guess you know my answer already...
 
Utamaduni wa vigogo kulindana ndio umeifikisha nchi mahali ilipo. I was expecting wale woote waliokataa tuhuma za ufisadi + Mzee Mkapa kuwa wameshafungua mashtaka. Badala yake they are going cold. People...we need to put pressure on them. I tell you, makelele yetu yakizidi they will come out one at a time. Lets keep this fire going kwa sababu I am sick of these BUSTARDS. Wanatoa ahadi nzuri wanapopita kuomba kura 'kula' and then wanageuka wanakuwa na JEURI na CHOYO na UBINAFSI. Hawatufai hawa. CCM and its leaders gotta go..and that day is coming soon

Capitol Hill, karibu jamvini, Style uliyoingia nayo ni 'kumkoma nyani giledi' natumaini utaidumisha!

SteveD.
 
SteveD,
unapojaribu kumlenga Mama Mkapa kwamba ndiye aliyemlazimisha Mzee Mkapa kukiuka maadili basi lazima uangalie kwamba ana leverage kiasi gani ktk maamuzi ya mumewe.

Tony Blair alishindwa kumburuza Mkapa hata kwa kumtishia kumkatia misaada, ije kuwa Mama Anna? Mbona tumekuwa wepesi namna hii kusahau misimamo ya Mzee Mkapa?

kwa uelewa wangu mdogo tu wa jinsi Mkapa anavyo-operate ninaamini kila jambo lilifanyika with his KNOWLEDGE and BLESSINGS.
 
SteveD,
unapojaribu kumlenga Mama Mkapa kwamba ndiye aliyemlazimisha Mzee Mkapa kukiuka maadili basi lazima uangalie kwamba ana leverage kiasi gani ktk maamuzi ya mumewe.

Tony Blair alishindwa kumburuza Mkapa hata kwa kumtishia kumkatia misaada, ije kuwa Mama Anna? Mbona tumekuwa wepesi namna hii kusahau misimamo ya Mzee Mkapa?

kwa uelewa wangu mdogo tu wa jinsi Mkapa anavyo-operate ninaamini kila jambo lilifanyika with his KNOWLEDGE and BLESSINGS.

JokaKuu, nimekuelewa mkuu, ila sikusema kumlazimisha, nilisema kum-influence.

Lakini naomba pia usi 'undermine' influence ya wanawake haswa katika 'ndoa', kuna viongozi wengi wa kiume wameangushwa au kuteleleka katika maswala fulani kutokana na influence zilizo za tamaa za wake zao. Mama Blair mwenyewe umeshasikia jinsi alivyokuwa analopoka saa nyingine hivyo kumweka mumewe katika utata kwenye maswala mawili matatu hivi.

SteveD.
 
Sitashangaa sana kama Mkapa ndiyo atanyakua tuzo hiyo, wakiangalia makaratasi Tanzania ilifanya vizuri chini ya uongozi wake, na zaidi ya yote kati ya wote waliomo kwenye hiyo orodha ni yeye peke yake amejijenga katika majukwaa ya kimataifa. So, ingawa sipendi apewe tuzo hiyo kwa sababu amewadharau watu waliompa nafasi hiyo kuangaza na ametumia madaraka yake vibaya.. ukweli ni kuwa atashinda tuzo hiyo na kutunyanyulia kidole cha kati!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom