Goodguy

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
237
500
Habari za wakati huu wakuu.

Naomba kuzungumza nanyi mnaojiita wanaharakati pamoja na wafuasi wenu.

Hiki kinachoondelea huko mitandaoni sio tamko rasmi la Chama kuwa sasa wameamua kufanya vile, ila ukimya wa viongozi juu ya hili jambo unanambia kuwa chama kimebariki.

Mi naomba mnifafanulie kidogo kwanini mnafanya hivi kwa uyu kijana mtafutaji kama ninyi mlivyo watafutaji ila mlijioficha kwenye pazia la siasa.

Hivi ni kweli Diamond ndo kikwazo cha nyinyi kufikia malengo mliojiwekea kama chama?

Hivi nikweli Diamond ndo chanzo cha ninyi kuanguka katika chaguzi zilizopita?

Hivi ni kweli Diamond ndo anawakwamisha kufanya siasa zenu na wananchi wakazipokea?

Lakini pia kama sijakosea wasanii wengi tu walifanya biashara ya kuuza burudani kwenye kampeni, kwanini Ninyi mmemuona Diamond tu?

Tafadhali naomba mje mtoe ufafanuzi ni kiasi gani huyu Kijana muuza burudani ya muziki anawakwamisha katika siasa zenu.

Bila kusahau ni ninyi mnatuambia uongozi uliokwepo ulikuwa uongozi wa upendeleo na visasi, ulipendelea kichama kidini na hata kikabila, sasa hiki mnachokifanya ninyi kinautofauti gani na hayo mliyotuaminisha yalikuwa yakitendeka.
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,421
2,000
Itakuwa funzo kwa Diamond.. kutokusimama na oppressors. Angalia walichofanya wasanii wa Nigeria dhidi ya serikali yao halafu alichokuwa anafanya Diamond.

Anastahili kuendelea kusagiwa kunguni.. Itakuwa ni funzo la yeye kutokudharau wananchi anatakiwa ajue msanii ni kioo cha jamii
 

Goodguy

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
237
500
Mwendazake ndio kwisha

Hayupo tena

kwisha kwisha kwisha

Mkuu hayupo huyo, Acha uhuru wa watu, Tusipangiane cha kufanya

Aliwazoesha vibaya Mwendazake

Hayupo huyo, Amka amka Amka

Amka amaka hayupo
Kila mtu anao uhuru mkuu ila si vibaya kuhoji, maana wapinzani wametulea katika mazingira ya kuhoji ndo mana namimi nimehoji.

Ni vyema sasa Nikapata majibu
 

Madumbikaya

JF-Expert Member
Jun 6, 2018
243
1,000
Kila mtu anao uhuru mkuu ila si vibaya kuhoji, maana wapinzani wametulea katika mazingira ya kuhoji ndo mana namimi nimehoji.

Ni vyema sasa Nikapata majibu
Wakati watu wanawasema akina Karume na Nyerere ulishawahi ona Makongoro anamtetea Baba yake

legacy haitetewi inajitetea

Nyerere anasemwa sana lakini hotuba zake na kazi zake zianajitetea zenyewe

Hatufanyi kazi ya kuhesabu viwanda vya nyerere na Madaraja

Hao wanavuna chuki waliyoipanda
 

Goodguy

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
237
500
Itakuwa funzo kwa Diamond.. kutokusimama na oppressors. Angalia walichofanya wasanii wa Nigeria dhidi ya serikali yao halafu alichokuwa anafanya Diamond.

Anastahili kuendelea kusagiwa kunguni.. Itakuwa ni funzo la yeye kutokudharau wananchi anatakiwa ajue msanii ni kioo cha

Okay, kwa mantiki iyo wananchi wote Tz ni chadema na diamond kawazarau?

Naona umezunguka zunguka tu, kapitie vizuri ujibu nilichokiuliza. Diamond amemkwamisha nani na kwanamna ipi?
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
13,938
2,000
WASANII (WANA SANAA)
...CCM Chama imara, kimeleta ukombozi Afrika, kinahimiza maendeleo kwa Watanzania.

WASHOBOKAJI SASA...!!
CCM baba lao, Wapinzani piga risasi, chinja, mashoga hao.
Wataweza kweli aah wapii, kushindana nasi aah wapi. Tuna Polisi tuna jeshi wamekwishaa!
 

malang0

JF-Expert Member
Apr 7, 2021
414
500
Acha ugoro umeona tamko la chama wapi dhidi ya huyo nyegezi, tamko la chama anatoa M wenyekiti au Katibu Mkuu zaidi yachapo yanakuwa mawazo binafsi ya watu, na ndiyo demokrasia hiyo, usihusishe mawazo binafsi na chama wewe mtetezi wa
 

Goodguy

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
237
500
Acha ugoro umeona tamko la chama wapi dhidi ya huyo nyegezi, tamko la chama anatoa M wenyekiti au Katibu Mkuu zaidi yachapo yanakuwa mawazo binafsi ya watu, na ndiyo demokrasia hiyo, usihusishe mawazo binafsi na chama wewe mtetezi wa
Vuta pumzi kidogo uondoe mihemko kisha kasome tena unipe majibu ndugu
 

Goodguy

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
237
500
WASANII (WANA SANAA)
...CCM Chama imara, kimeleta ukombozi Afrika, kinahimiza maendeleo kwa Watanzania.

WASHOBOKAJI SASA...!!
CCM baba lao, Wapinzani piga risasi, chinja, mashoga hao.
Wataweza kweli aah wapii, kushindana nasi aah wapi. Tuna Polisi tuna jeshi wamekwishaa!
Kasome tena unisaidie majibu mkuu, Diamond anawakwamisha wapi katika siasa zenu?
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,548
2,000
Too late man, that's a wake up call, mitandao siku hizi ina nguvu zaidi ya polisi na Ndugai, liwe funzo kwa Diamond mwenyewe na wasanii wenzake kina Harmonize, Kiba na wengine, ole wao tena washiriki kampeni za CCM, mbaya zaidi alijitutumua twitter hajawahi kushindwa vita ndio akajiharibia kabisa.
 

mgaka12

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
560
1,000
Hamas na Hezbollah zilianza hv hv kujifanya ni watetezi wa watu then wakaanza kutumia nguvu kusambaza ideology yao kwa nguvu na kulazimisha kila mtu kuamini na kufata itikadi yao na leo vimekuwa vyama vya kigaidi ndo naona uelekeo wa chama fulani hapa Tanzania wanapita njia zile zile za Hamas na Hezbollah kutoka kwenye vyama vya kisiasa mpk kuwa vyama vya harakati mwisho kuwa vyama vya kigaidi .
 

Goodguy

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
237
500
Hamas na Hezbollah zilianza hv hv kujifanya ni watetezi wa watu then wakaanza kutumia nguvu kusambaza ideology yao kwa nguvu leo vimekuwa vyama vya kigaidi ndo naona uelekeo wa chama fulani hapa Tanzania wanapita njia zile zile za Hamas na Hezbollah kutoka kwenye vyama vya kisiasa mpk kuwa vyama vya harakati mwishi vyama vya kigaidi .

Hawa watu wanatuchanganya mkuu, Wako bungeni miaka kibao leo wanataka mapishi yaliyowashinda wao wakati wako jikoni wamtwishe Diamond.

Yani Diamond leo ndo kawa sababu ya chama fulani kutofanikiwa katika mambo fulani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom