Kampeni chafu mpaka ahera

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Mwanasiasa wetu mmoja alifariki na kabla ya kuhukumiwa ahera malaika wakamshauri achague mwenyewe ikiwa anataka muingia peponi au motoni, lakini wakamsisitiza kuwa uchaguzi wowote atakaofanya ni mara moja tu, hakuna kughairi.

Kwanza walimpeleka motoni kuona mazingira yake. Kule walikuweko marafiki zake wanaponda maraha ya aina zote. Alipopelekwa peponi akakuta raha ndo zile zile lakini hakukuwa na mtu isipkuwa yeye tu. Akabakia pale siku tatu. Malaika waliporejea wakamuliza anataka kubakia wapi akajibu, "bora niende motoni kwani hapa panaboa sana".

Kufika motoni akawakutia marafiki zake wamevaa magwanda, jua kali, wanazoa kinyesi, kazi za sulubu na mijeledi mgongoni. Alishangaa sana. Alipowauliza ilikuwaje hali kubadilika namna ile wakamjibu, "Pale ulipokuja mara mwanzo tulikuwa katika kampeni". Karibu, jisikie nyumbani
 
hii ni hatari ......
kama alikuwa na dini yeyote hapa duniani
asingechagua hilo.....
labda hajui tofauti ya moto na Pepo
 
Dini haina msaada wowote katika maisha yajayo,ina msaada hapa hapa wa kiuchumi,madaraka,ajira etc.Ana dini huyu maana ametokea duniani ila ndio hivyo tena.
 
Back
Top Bottom