kampeni chafu dhidi ya Dr Slaa By Mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kampeni chafu dhidi ya Dr Slaa By Mafisadi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by August, Sep 14, 2010.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Awali katika uchunguzi huo wa kina wa waandishi wetu ambao walifanikiwa kumkuta Mahimbo akiwa amejificha juu ya ghorofa, nyumbani kwa kigogo mmoja wa serikali hapa jijini Dar es Salaam, walifanikiwa kumhoji na sehemu ya mahojiano hayo yakianza na mwenyeji wake yalikuwa kama ifuatavyo:

  Mwandishi: Habari gani?
  Ndugu: Nzuri, wewe ni nani na tukusaidie nini?

  Mwandishi: Ni mwandishi wa habari kutoka Gazeti la Uwazi, naomba kumuona Mahimbo
  Ndugu: Nani kakuambia yupo hapa?

  Mwandishi: Kuna rafiki yake wa karibu huyu hapa niliyefuatana naye ndiye aliyeniambia yupo hapa.
  Rafiki: Niko na huyu mwandishi, tunaomba kumuona Mahimbo wala msiwe na wasiwasi, ila naomba nitete kwanza na Mahimbo pembeni.

  Baada ya muda Mahimbo na rafiki yake walimaliza kuteta, mahojiano naye yakaanza.
  Mahimbo: Karibu sana mwandishi
  Mwandishi: Nashukuru! Pole sana kwa misukosuko ya hapa na pale.

  Mahimbo: Ahsante sana.
  Mwandishi: Mbona uko huku wakati ndugu na marafiki zako wanakutafuta na wala hawakupati katika simu zako?

  Mahimbo: Nimekuwa na wasiwasi juu ya maisha yangu kwani nimekuwa nikitumiwa ujumbe na kupigiwa simu za kifo, nikaona hii ni hatari nijihami na siwezi kukaa huko kwangu kwa sasa.
  Mwandishi: Hebu nipe picha halisi kuhusiana na Josephine pia Dk. Slaa.

  Mahimbo: Josephine ni mke wangu wa ndoa kabisa na tuliifunga Septemba 7, 2002 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kijitonyama chini ya mchungaji Lewis Hiza.
  Mwandishi: Sasa imekuwaje kuwa na mgogoro na yupo wapi?

  Mahimbo: Mke wangu ni mfanya biashara na mtumishi wa NGO moja, alikuwa akiniaga kuwa anakwenda mikoani, nikawa namruhusu lakini ilipofika Machi mwaka huu akaniambia ananiachia kibanda changu na anakwenda kwenye nyumba yake, aliondoka na sikujua alipo, na kwa hivi sasa namuona majukwaani akitambulishwa kama mke wa Dk. Slaa.

  Mwandishi: Je, taarifa ya kuwa mkeo yuko na Dk Slaa ulizipata lini?Na kwanini sakata hili liwe la moto kipindi cha kampeni na siyo kipindi cha nyuma?

  Mahimbo: Nilipata tetesi tangu zamani ila nilipata ukweli pale alipotangazwa Jangwani na Dk. Slaa katika ufunguzi wa kampeni za Chadema wala hakuna chama chochote cha siasa kilichonituma kulalamika.

  Mwandishi: Mkeo alikuwa akikuaga au kukutoroka na je ulikuwa ukimchunguza?
  Mahimbo: hapana nilikuwa nafanya uchunguzi wa kina ndipo nichukue hatua.

  [​IMG]
  Wakisherehekea harusi yao ufukweni.
  Mwandishi:Naona sakata hili umeshalifikisha mahakamani kwa kumdai Dk. Slaa shilingi Bilioni moja, kwa nini usimdai mke badala ya fedha? Je, ukishinda kesi utamchukua mkeo ukaishi naye?
  Mahimbo: Suala la kuishi naye itategemeana, ila mambo yote naiachia mahakama na tayari kuna wakili wangu anayesimamia hiyo kesi.

  Mwandishi: Hapa kwa kigogo unatarajia kutoka lini?
  Mahimbo: Huwa kuna muda natoka nikitumia gari lenye vioo vyeusi (Tinted) na kurudi haraka, kutoka kwanza napima hali ya hewa kwanza.

  Mwandishi: Ndugu na marafiki zako wanakuulizia hawajui ulipo na hata wakikupigia simu hawakupati, tuwaambie nini?
  Mahimbo: Waambie mimi ni mzima ila sitaki watu wajue nilipo, na simu nimeamua kuzima kutokana na vitisho juu ya maisha yangu hivyo nimeamua kutokuwa hewani ili nipumzike kidogo.

  Mwandishi: Pole sana, nashukuru kwa mahojiano, tutaonana tena Inshaalah!
  Mahimbo: Ahsante sana, ila sitaki watu wajue nilipo.

  Mwandishi alipomtafuta Josephine kwa njia ya simu kutaka kujua kama yeye ni mmoja wa watu wanaotoa vitisho kwa Mahimbo, mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
  Mwandishi: Josephine habari gani?
  Josephine: Nzuri, wewe nani?

  Mwandishi: Mimi ni mwandishi wa habari kutoka Gazeti la Uwazi
  Josephine: Unataka nini?
  Mwandishi: Kuna madai kwamba umekuwa ukimtishia Mahimbo kwa ujumbe mfupi pia kwa simu unazompigia mara kwa mara juu ya maisha yake. Je ni Kweli?

  Josephine: Sikiliza, mambo ya ndoa ni yangu binafsi na hayavihusu vyombo vya habari, mimi ni mwanamke niliyefundwa, siwezi kutoa siri zangu za ndoa kama yeye (Mahimbo). Wote tuna wazazi ambao ndiyo pekee wanaoweza kuingilia suala hili na si vyombo vya habari.

  Mwandishi alimtafuta Dk. Slaa kwa simu lakini ilikuwa haipatikani ila mshauri wa Chadema ambaye pia ni wakili wa kujitegemea Mabere Marando alisema kuwa suala la Mahimbo na Josephine lina mkono wa kisiasa na si bure.

  [​IMG]
  Dk Slaa.
  “Nashangaa kumuona Mahimbo akimtafuta mkewe majukwaani na siyo kufuata taratibu za kisheria. Naamini alikuwa akifahamu kila kitu tangu mapema lakini hakuchukua hatua yoyote mpaka pale kampeni zilipoanza. Kwa kuwa ameshalipeleka suala hili mahakamani kudai fidia tutapambana huko huko,” alisema Marando.

  Kwa upande wa Mchungaji Lewis Hiza anayedaiwa kufungisha ndoa kati ya Mahimbo na Josephine mwaka 2002 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kijitonyama, alipoulizwa kama ni kweli alifungisha ndoa hiyo alikiri kufanya hivyo lakini akagoma kuendelea kulizungumzia suala hilo kwa kuwa tayari limeshaandikwa kwenye vyombo vya habari.

  “ Suala hili limeshajadiliwa katika vyombo vya habari, kwa maadili yangu ya kichungaji siwezi kuzungumza chochote, asante na pole,” alisema Mchungaji Lewis Hiza.
  Tags: uwazi11
  Share Twitter Facebook

  Ipo kwenye magazeti ya Shigongo aliyekuwa ana gombea Ubunge Buchosha Sema tu kura hazikutosha.
   
 2. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Hii issue iko mahakamani, tusiizungumzie.
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Inaniuma sana nikifiria huwaga ninalia..huu ni wimbo wa juma nature.
  Kuna wakati huwa nawaza kama watu wanajua kuwa kampeni chafu dhidi ya Slaa wanazifanya wenyewe na si vinginevyo?mnajuaje labda kuliendeleza suala hili kumchafua slaa na wala si kumsaidia? nadhani kama ilivyosemwa awali ni vyema mkaendeleza mjadala juu ya masuala muhimu kwa maendeleo ya taifa ni masuala ya kimbea tu.
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Maihmbo! Mahimbo! Maihmbo! Mbona unatumiwa hivyo!mke mke unatafuta umarufu, nakumkomoa josephine. Check alivyo na busara za ufirst lady kweli kwako aliingia choo yakiume. Humfai kabsaaa ndiyo maana kakukimbia !
   
 5. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Dume la uhakika halimchungulii mkewe..hahah,mahimbo kiazi tu!
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,640
  Likes Received: 21,851
  Trophy Points: 280
  Hili gazeti linastahili kufungiwa na mhariri wake kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuandika maelezo ambayo yanahusiana na kesi iliyoko mahakamani
   
 7. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Kwa hakika huyu jamaa atakuwa amejipunguzia miaka kadhaa ya kuishi kwa stress kama alikuwa kabakiza miaka kumi ya kuishi basi miaka sita yote ameipunguza mwenyewe....
   
Loading...