Kampeni chafu Arumeru: Chadema Yalalamika, CCM yakanusha kuhusika....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni chafu Arumeru: Chadema Yalalamika, CCM yakanusha kuhusika.......

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by bibikuku, Mar 17, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimenyofoa kipande cha habari iliyopo kwenye gazeti la leo Jumamosi la Mwananchi ili mjionee malalamiko ya Chadema kuhusu kampeni chafu na majibu ya CCM kuhusu malalamiko hayo..................................

  Kampeni chafu zatawala Arumeru
  Mwananchi Machi 17, 2012

  Malalamiko Chadema
  Meneja Mwenza wa Kampeni za Chadema katika uchaguzi huo, Vicent Nyerere akituhumu CCM kwamba kimesambaza waraka mitaani unaowakashifu viongozi wao wakuu.

  Waraka huo ambao gazeti hili limeuona una kichwa cha habari: “Chadema na Masela,” kikiwataja viongozi kadhaa wa chama hicho hasa wabunge wasiooa au kuolewa kwamba wanamuiga Katibu Mkuu wa wao, Dk Willibrod Slaa ambaye wanadai kwamba aliasi kazi ya ukasisi hivyo kufukuzwa.

  Kadhalika, waraka huo unamuonya mgombea wa chama hicho, Joshua Nassari kuachana na Chadema kwa maelezo kwamba atachafua sifa ya familia yake ambayo baba yake ni mchungaji.

  Waraka huo ambao mwishoni umeandikwa “…..itaendelea wiki ijayo,” unakihusisha Chadema na ukabila na kwamba ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) ya kabila la Wachagga ambalo limekuwa likipokea misaada kutoka kwa wafadhili wa nje.

  Hata hivyo, Nyerere alisema Chadema kimeupuuza waraka huo kwani maneno yake yanawiana na kauli alizoziita chafu ambazo alidai kwamba zimekuwa zikitolewa na viongozi wa CCM kwenye kampeni.

  “Huu ni ujinga na wala hauwezi kuwasaidia kushinda kwani hakuna jipya ni yaleyale kila siku, waache wapoteze muda sisi tunapigana kutwaa jimbo na hilo tuna uhakika nalo,” alisema Nyerere.

  Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa Chadema, John Mrema alisema kumekuwapo kwa makundi ya watu ambayo yamekuwa yakiegesha magari karibu na viwanja ambako Chadema kinafanyia mikutano ya kampeni kuwazuia watu wasihudhurie.

  “Katika maeneo mengine tumekuta taarifa kwamba mabalozi wa nyumba kumi wanazunguka kuwashawishi watu wasifike kwenye mikutano yetu kwa kuwatisha kwamba kutakuwa na vurugu, hizi ni siasa chafu ambazo hatuwezi kukubaliana nazo,” alisema Mrema.

  Malalamiko CCM
  Meneja wa Kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa chama chake hakina muda wa kuwachafua Chadema na kwamba hizo ni dalili za kutapatapa baada ya wapinzani wao hao, kubaini kwamba watashindwa kwenye uchaguzi huo.

  Badala yake Nchemba alisema Chadema ndiyo wamekuwa wakiendesha siasa chafu kwa kuwatuma vijana wao kufanya fujo kwenye mikutano ya CCM na kutoa tahadhari kwamba watawashughulikia hata bila kuwafikisha polisi.

  “Hili nalisema hata kwa wanachama wa CCM kama wapo wanaofanya vitendo hivi; siyo lazima uende kwenye mkutano wa kampeni, kama hutaki au mambo wanayozungumza yanakukera, basi lala nyumbani usiende na siyo kwenda kuvuruga mikutano yao,” alisema Nchemba na kuongeza:

  “CCM ni chama kikubwa, mikutano yetu ina watu wengi kwa mfano, pale Mbuguni tulikuwa na watu zaidi ya 5,000 sasa wewe mtu mmoja, wawili au watatu mkija kufanya fujo halafu ule umati ukawageukia mtaweza kupona kweli? Sasa Chadema wawaambie vijana wao waache la sivyo tutawashughulikia.”

  Kuhusu CCM kwamba kinapanga njama za kuwazuia watu wasihudhurie mikutano ya Chadema Nchemba alisema: “Hawa wenzetu wanatafuta huruma kwa wananchi, sisi CCM tuwazuie watu gani kwa sababu hawana watu, tumemwona mgombea wao akikosa watu sehemu nyingi tu, kwa hiyo wasitafute visingizio.”

  Wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM Jumatatu wiki hii, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Ngaresero, Usa River, Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama pia alidai kwamba kulikuwa na njama za kukichafua chama chake kwa kuwavisha sare za chama hicho baadhi ya watu ambao wangetumika kufanya fujo.

  Hata hivyo, Chadema kupitia viongozi wake wamekanusha kuwatuma vijana wao kwenye mikutano ya CCM na badala yake kudai kwamba chama hicho tawala kimekuwa kikipingwa na wananchi kutokana na lugha chafu za wapiga kampeni wake.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni vigumu sana kuitenganisha CCM na SIASA ZA MAJI MACHAFU YA CHOONI. Dawa pekee ni kufanya general UPROOT FROM THE GRASSROOT UP TO THE TOP. Tushikamane ktk kumng'oa nduli huyu.
   
 3. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  ningeshangaa sanaaaaaa kama kampeni zingeisha bila magamba kuja na kituko. igunga walisema eti chadema wameleta alshabaab, wakambadilisha yule DC mkristu aliyevaa kilemba eti kabuliwa hijabu, aisee kweli ccm magamba magumu
   
 4. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  siasa uchwara za maji taka kwenye kampeni ni dalili za kuanza kushindwa kabla ya matokeo
   
Loading...