Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa | Page 13 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mshimba, Jul 29, 2015.

 1. M

  Mshimba Member

  #1
  Jul 29, 2015
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5


  [​IMG]
  Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM

  Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.

  Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.

  Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..

  Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.

  Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."

  Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..

  Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika.

  Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.

  Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea huyo.

  Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.

  Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..

  Updates;

  CHanzo: CID wa Kongwa.
   

  Attached Files:

  • mb.jpg
   mb.jpg
   File size:
   38 KB
   Views:
   7,296
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. coxson

  coxson JF-Expert Member

  #241
  Nov 16, 2015
  Joined: Apr 10, 2015
  Messages: 2,327
  Likes Received: 1,340
  Trophy Points: 280
  Halafu huyu jamaa hafai kabisa,alilewa unaibu na kutoa watu ovyo nje,mkataeniiiiiii
   
 3. Chachu Ombara

  Chachu Ombara JF-Expert Member

  #242
  Nov 17, 2015
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 4,341
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Wabunge nna kazi maana mtakula bakora mpaka mkome
   
 4. KikulachoChako

  KikulachoChako JF-Expert Member

  #243
  Nov 17, 2015
  Joined: Jul 21, 2013
  Messages: 12,880
  Likes Received: 8,408
  Trophy Points: 280
  Leo amteuliwa na chama kugombea uspika wa BUNGE......ONLY IN TANZANIA....
   
 5. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #244
  Nov 17, 2015
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 5,437
  Likes Received: 2,106
  Trophy Points: 280
  It is very true
  Baada ya huyo jamaa kuukwaa Uspika tutarajie kuwa anaweza hata kuwacharaza bakola wabunge wa upinzani pale atakapoona kuwa hawamtii.
  Hivi ina maana wabunge wa CCM wameamua kumpitisha Ndugai kwa qualification yake kubwa ya kucharaza watu bakora?!
  Hakika natabiri kuwa bunge hili litakuwa na vioja na vurumai kuliko mabunge yote yaliyowahi kuwepo hapa nchini.
   
 6. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #245
  Nov 17, 2015
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 5,437
  Likes Received: 2,106
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hayo mambo yanaweza kutokea Tanzania pekee, kwa mbunge ambaye alithibitika bila shaka yoyote kuwa alimcharaza mgombea mwenzie kwenye kura za maoni za CCM hadi kusababisha huyo jamaa kuzirai na kulazwa hospitalini, lakini leo wabunge wenzie wa CCM ndiyo wanamuona ndiye anapaswa kushika wadhifa huo nyeti kabisa katika nchi.
  Hakika kutokana na mtindo huu wa CCM wa uendeshaji wa nchi hii, ni dhahiri lengo lao ni Bunge hili la 11 litawaliwe na fujo ambazo wao kama kawaida yao watawatupia lawama wabunge wa upinzani kuwa ndiyo wanaosababisha vurumai hizo.
  Hauwezi katika Taifa lolote ukadumisha amani kama watawala wa nchi hiyo husika inachofanya ni kuminya haki za raia wake na kuliona kundi dogo la watawala kama UNTOUCHABLES ambalo liko above law ambalo hakuna mkono wowote wa sheria unaoweza kuwagusa!
   
 7. Majighu2015

  Majighu2015 JF-Expert Member

  #246
  Jan 11, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 2,302
  Likes Received: 2,416
  Trophy Points: 280
  Kwa nini Ndugai hawakumfunga? CCM wanafiki sana
   
 8. g

  gpastory JF-Expert Member

  #247
  Jan 11, 2017
  Joined: Nov 11, 2016
  Messages: 213
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Wapuuzi tu hao cjui na nani wao hapo juuu
   
Loading...