Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa | Page 12 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mshimba, Jul 29, 2015.

 1. M

  Mshimba Member

  #1
  Jul 29, 2015
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5


  [​IMG]
  Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM

  Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.

  Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.

  Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..

  Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.

  Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."

  Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..

  Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika.

  Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.

  Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea huyo.

  Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.

  Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..

  Updates;

  CHanzo: CID wa Kongwa.
   

  Attached Files:

  • mb.jpg
   mb.jpg
   File size:
   38 KB
   Views:
   7,378
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. I

  Ilungu Senior Member

  #221
  Jul 30, 2015
  Joined: Apr 11, 2015
  Messages: 195
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama akipona ndo ajifunze kuwa kumpiga mtu picha bila ridhaa yake ni aina ukorofi na mara nyingi huamsha hasira na ghadhabu.
   
 3. zugimlole

  zugimlole JF-Expert Member

  #222
  Jul 30, 2015
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 1,742
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 280
  Nilidhani ndugai mutu ya busara kumbe wa hovyo
   
 4. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #223
  Jul 30, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,625
  Likes Received: 1,656
  Trophy Points: 280
  atavuna alichopanda.
   
 5. m

  manpierre New Member

  #224
  Jul 30, 2015
  Joined: Mar 15, 2014
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Dah ebana siasa ni Nooomaaa
   
 6. mkalli

  mkalli JF-Expert Member

  #225
  Jul 30, 2015
  Joined: Mar 21, 2014
  Messages: 225
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Una makengeza ??
   
 7. G3T

  G3T JF-Expert Member

  #226
  Jul 30, 2015
  Joined: May 21, 2013
  Messages: 825
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mpaka octoba ifike,mengi tutayaona na kuyasikia.
   
 8. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #227
  Jul 30, 2015
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 962
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Vipi mkuu,umeshakuwa na Imani na UKAWA?
   
 9. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #228
  Jul 30, 2015
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,835
  Likes Received: 2,105
  Trophy Points: 280
  Mkuu bado sina imani na UKAWA lakini nataka mabadiliko
   
 10. s

  sngwangwalu New Member

  #229
  Jul 30, 2015
  Joined: Apr 5, 2014
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Toka smartphone zimeingia...zimekuwa so helpful kufanya watu wawe pia smart na general awareness kuhusu politics. Asante mzungu.
   
 11. Diva Beyonce

  Diva Beyonce JF-Expert Member

  #230
  Jul 30, 2015
  Joined: Mar 6, 2014
  Messages: 12,953
  Likes Received: 6,064
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli siku hizi watu wanapata habari ya mambo yanayoendelea tofauti na zamani kudaganywa kulikua nje nje.
  Chama tawala wajipange sana watu hawadaganyiki wakati uu. Naziheshimu sana smartphone
   
 12. chisagapipi

  chisagapipi JF-Expert Member

  #231
  Jul 30, 2015
  Joined: Jun 27, 2015
  Messages: 467
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Ile fimbo aliyokuwa nayo ndugai inaitwa subwaa kwa lugha ya dodoma.nahis itakuwa mti wa mkole au msechela.huwa ni ngumu saana.ndugayi amechemsha saana.
   
 13. e

  eddy JF-Expert Member

  #232
  Aug 2, 2015
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 10,591
  Likes Received: 4,716
  Trophy Points: 280
  Pole sana Dr.Chilongani, fimbo umepata na ubunge umekosa, lakini usife moyo wewe bado kijana 2020 sio mbali kajipange upya tu kijana.
   
 14. M

  Mshimba Member

  #233
  Aug 4, 2015
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Bado hajakosa mpaka kikao cha NEC kitakapoamua kama mchakato utalikuwa fair ama la!!
   
 15. g

  gilaibomba JF-Expert Member

  #234
  Aug 4, 2015
  Joined: Jun 11, 2015
  Messages: 354
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka kwenye bunge hili la mwisho,akiendesha kikao Mh. Naibu Spika alimkejeli Mb wa CUF kutoka ZNz ambaye aliyeanguka ktk kura za maoni kwa kumuambia awape matokeo ya kura huko angali akijuwa jamaa kapigwa chini.Sasa inakula kwa Ndugai.....chezea Pemba weyeee.
   
 16. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #235
  Aug 16, 2015
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 8,349
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Hilo fimbo kabeba la nini kwenye mkutano?

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. screpa

  screpa JF-Expert Member

  #236
  Nov 14, 2015
  Joined: Sep 10, 2015
  Messages: 6,462
  Likes Received: 8,380
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu alipitapitaje ubunge kwa tukio hili, Na akiwa spika vipi hatakuja Na hilo gongo lake bungeni?
   
 18. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #237
  Nov 14, 2015
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 47,525
  Likes Received: 30,150
  Trophy Points: 280
  Hivi mtu kama huyu bado anataka kugombea uspika ?
   
 19. i

  ibesa mau JF-Expert Member

  #238
  Nov 14, 2015
  Joined: Sep 17, 2015
  Messages: 1,566
  Likes Received: 995
  Trophy Points: 280
  ndo utashangaa anakuwa spika ,. ccm watu wakorofi korofi ndio inawapendaga.
   
 20. M

  Martinez JF-Expert Member

  #239
  Nov 16, 2015
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 520
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Hii ndio ccm, ...chama tawala !!!
   
 21. G

  Gamba la Chuma JF-Expert Member

  #240
  Nov 16, 2015
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,247
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nilidhani kampiga Dr Tulia
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...