Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa | Page 11 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mshimba, Jul 29, 2015.

 1. M

  Mshimba Member

  #1
  Jul 29, 2015
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5


  [​IMG]
  Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM

  Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.

  Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.

  Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..

  Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.

  Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."

  Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..

  Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika.

  Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.

  Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea huyo.

  Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.

  Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..

  Updates;

  CHanzo: CID wa Kongwa.
   

  Attached Files:

  • mb.jpg
   mb.jpg
   File size:
   38 KB
   Views:
   7,378
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. I

  Igangilonga Senior Member

  #201
  Jul 29, 2015
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 121
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuna hadi video clip ya hizo vurugu. Km hujaipata weka namba yako nikutumie
   
 3. Andfaru

  Andfaru JF-Expert Member

  #202
  Jul 29, 2015
  Joined: Nov 9, 2012
  Messages: 210
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  na mimi nasema wapigwe tu maana hakuna namna nyingine sasa
   
 4. p

  p.masters Member

  #203
  Jul 29, 2015
  Joined: Jul 15, 2015
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Police walikua wapi hapo?
   
 5. SIMBA45

  SIMBA45 JF-Expert Member

  #204
  Jul 29, 2015
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siasa syo mabavu,uadui, ama hoja ya nguvu ni swala la nguvu za hoja.. na tabia aina dawa, sasa ccm washazoea kuwa na kiburi na mabavu ya madaraka kuwaonea vyama vya upinzani, tabia hyo imejengeka mpaka ndani ya chama chao wenyewe na kuanza kuwadhuru their opponents.
   
 6. baba angel

  baba angel Member

  #205
  Jul 29, 2015
  Joined: Feb 7, 2015
  Messages: 46
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Watungasheria hao
   
 7. K

  KIBAKA WA MAREKANI New Member

  #206
  Jul 29, 2015
  Joined: Nov 27, 2014
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Duuuh! kwa heri ccm tutakukumbuka daima!
   
 8. t

  tedywite JF-Expert Member

  #207
  Jul 29, 2015
  Joined: Apr 10, 2015
  Messages: 284
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hawa ccm wamejisahau sana.

  Huyu Ndugai hakustahili kuwa naibu spika.
  Shame on him.
   
 9. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #208
  Jul 29, 2015
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,378
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ndugai hasira za nini?
   
 10. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #209
  Jul 29, 2015
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,378
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
 11. tz2015

  tz2015 JF-Expert Member

  #210
  Jul 29, 2015
  Joined: Jun 23, 2014
  Messages: 986
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nahona kosa la mkutano huo hakukuwa na wale polisi wanaovaa suti
  na gloves nyeupe ili mheshimiwa ndungai awaamuru wawatoe nje ya mkutano
  wapinzani wake.Nashauri mkutano ujao wahakikishe hilo linafanyika,ili mheshimiwa
  asitumie nguvu ya ziada.
   
 12. G

  Gandachungu New Member

  #211
  Jul 29, 2015
  Joined: Jun 20, 2015
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahaaaa! Ndo yale ya Mizengopinda ukileta fujo unapigwa tu!
   
 13. s

  sitaki shobo Member

  #212
  Jul 29, 2015
  Joined: Jun 9, 2015
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha uongooo
   
 14. mwachisabwe kibona

  mwachisabwe kibona Senior Member

  #213
  Jul 29, 2015
  Joined: Aug 5, 2014
  Messages: 116
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  DO kweli dalili ya mvua ni mawingu, rip Ccm
   
 15. h

  hamic abdallah Senior Member

  #214
  Jul 29, 2015
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 105
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Saka tonge
   
 16. GREATTHINKERDAIMA

  GREATTHINKERDAIMA JF-Expert Member

  #215
  Jul 29, 2015
  Joined: Feb 26, 2014
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Finito job ndu ga i.
   
 17. Things Fall Apart

  Things Fall Apart Senior Member

  #216
  Jul 29, 2015
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Sasa ni dhahiri bundi katoka UKAWA katua rasmi CCM
   
 18. muuza ubuyu

  muuza ubuyu JF-Expert Member

  #217
  Jul 29, 2015
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 2,713
  Likes Received: 838
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaaa, magamba kazi kweli kweli!
   
 19. t

  tajiri Jose Member

  #218
  Jul 29, 2015
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado yupo hai? Maana kuna za chini chini kama jamaa kafariki
   
 20. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #219
  Jul 30, 2015
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,191
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  Hivi ni kwa nini hadi sasa Ndugai hajakamatwa na kufunguliwa mashtaka!
   
 21. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #220
  Jul 30, 2015
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  waandishi muwe makini jamani, ingawaje Ndugai alichofanya ni kosa kubwa sana, na inatisha naibu spika kufikia hapo lakini kuna tofauti kati ya kumtandika mtu na fimbo na kumpiga na GONGO.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...