Naam hiki ni kipindi mujarabu sana.
Kampeni zinaendelea kwa kasi kote Bara na Zanzibar.
Leo Tunamwita Dkt. Mwinyi ama timu yake aje hapa ama waje uwanjani.
Tunahitaji tujibiwe baadhi ya masuali yetu muhimu kuhusu Mwelekeo wa sera za CCM na msimamo wa Dkt Mwinyi.
Dkt Kule Zanzibar unaitwa uwajibu haya maswali na nadhani yatakuongezea murua wako na kutathminiwa ili upate kuungwa mkono.
MASWALI
1. Wazanzibari wengi wanataka kujua msimamo wako juu ya Muungano wa serikali tatu au Mkataba ili Zanzibar ipate hadhi, uwezo na nguvu za kujiletea Maendeleo yake baada ya miaka zaidi ya 50 ya Muungano wa serikali mbili bila mafanikio yaliyokusudiwa. Nini msimamo wako kuhusu hili? .
2. Umezungumzia sera ya Uchumi ya Blue na kuahidi Wazanzibari kunufaika na Mafuta. Kwanza Rasilimali za Mafuta na Bahari Kuu ni mali ya Muungano hili unalijuwa. Wazanzibari wanahitaji kuyamiliki mafuta yao na Bahari yao jee uko tayari kuhakikisha Zanzibar inamiliki rasilimali ya Mafuta na bahari kwa kuondoa sheria zinazotoa umiliki kwa Jamuhuri ya Muungano badala ya Zanzibar kama nchi?
3. Tunajuwa kwa sasa CCM na chama chako kinatambua uwepo wa serikali mbili kuelekea moja. Jee utakuwa tayari kusikiliza maoni ya wazanzibari wengi kuhusu Muungano wautakao au utasimamia msimamo wa CCM ?
4. Katiba ya Zanzibar inatambua Zanzibar kama nchi yenye mipaka yake ile iliyokuwepo kabla ya Mapinduzi na inatambuwa muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa pamoja Rais wa Zanzibar kuwa na uwezo wa kuigawa Mipaka ya Mikoa na Wilaya. Unawahakikishia vipi Wazanzibari juu ya uwepo wa Zanzibar yao bila kugawanywa au kuwa nchi moja wakati CCM inatambuwa Serikali mbili kuelekea moja?
5. Huoni kampeni zako zina lengo la kuwahadaa wazanzibari wakati unajuwa fika aina ya Muungano uliopo hautoi fursa za Zanzibar kufunguka kiuchumi kutokana na kubanwa na ilani , katiba ya CCM na Sheria kadhaa za JMT? Uko tayari kupingana na CCM kwa maslahi ya Zanzibar?
6. Unawahikishia vipi Wazanzibari kuhusu Ubaguzi wa kiitikadi na ubaguzi wa ajira kwenye Serikali wakati unajuwa tatizo ni uhafidhina wa CCM. Uko tayari kupambana na wahafidhina kuhakikisha unaleta usawa Zanzibar?
MWISHO KWA LEO.
Tunaomba uje hapa uwanjani useme kinaga ubaga Wazanzibari wakusikie.
Kishada.