Kampeni 2015: Lowasa sawa ila dr. Slaa nitam-miss haswaa,ikibidi aombwe awe kampeni meneja

JERRY

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
630
502
Nakumbuka uchaguzi 2010 jinsi dr.alivyoweza kuwashawishi watu kwa hoja za uhakika huku akilimiliki jukwaa vilivyo na kuwaacha wapinzani wake wakipumulia mashine kwa hoja dhaifu za udini.

Hebu fikiria mfuko wa simenti by then ilikuwa karibu 10,000 na zaidi dr.akaja na mchanganuo wa kiuchumi ni jinsi gani ataweza kushusha bei ya simenti mpaka 5000 na somo likaeleweka wasio elewa ni kwamba walikomaa tu.
Suala la elimu bure ndo alifunika kabisa,kwa hoja nzito ni jinsi gani serikali yake ingegharamia elimu nchini,katiba mpya ndo sisemi kabisa maana alifunika.

Safari hii kwa ukawa bado sijajua vizuri sana strengh za lowasa kwenye kujenga hoja jukwaani na kulimiliki jukwaa, magufuli kwa harakaharaka nikimtathmini anaonekana anaweza kujenga hoja ila sasa itategemea kama hoja zitakuwa za mashiko ingawa siipendelei sana kauli yake ya "sitawaangusha" naona kama imekaa kichama zaidi
 
Dr Slaa hawezi kushiriki kuwa sehemu ya maovu..hawezi kukubali aandikwe upande mchafu wa historia
 
Back
Top Bottom