Kampeini za Kikwete Kuhakikisha watoto wa Watanzania hawapati Elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeini za Kikwete Kuhakikisha watoto wa Watanzania hawapati Elimu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kichuguu, Oct 27, 2010.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkutano wa JK wafunga shule tano
  Tuesday, 26 October 2010 21:08
  Kizitto Noya, Mwanza  SHULE nne za msingi na sekondari zilizo kwenye Kata ya Nkome wilayani Geita, jana ziliahirisha masomo ili wanafunzi wahudhurie mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete Shule hizo za sekondari za Kabwela na Nyamboge na shule za msingi za Ihumilo na Mwaloni zenye zaidi ya wanafunzi 5000 kwa pamoja zilisitisha masomo na wanafunzi kufurika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ihumilo ambako mkutano huo ulifanyika.

  Habari zilizopatikana uwanjani humo zimeeleza kuwa shule hizo zilisitisha masomo ama kwa wanafunzi kutaka kuhudhuria mkutano huo au walimu kuwalazimisha wafike kumwona mgombea huyo wa CCM.
  Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwenye Shule ya Sekondari ya Nkome, Michael Faustine alisema kuwa jana walisoma kipindi kimoja tu cha kwanza na baadaye walimu waliwataka warudi nyumbani kubadili nguo na kwenda kwenye mkutano huo.
  "Sisi tulisoma kidogo; tulifika na kusoma kipindi cha kwanza na baadaye walimu walitutawanya na kututaka kurudi kwenye mkutano huo," alisema.
  Bertha Mabingo, mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ihumilo alisema waliambiwa tangu Oktoba 18 mwaka huu kuwa jana kusingekuwa na masomo na badala yake wafike kusikiliza mkutano wa Kikwete.
  "Sisi tulijua mapema kwamba leo (jana) hatutasoma. Walimu walituambia tangu Oktoba 18 kwamba tufike kumwona na kumsikiliza Kikwete," alisema mwanafunzi huyo.
  Mwanafunzi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Happiness Yohana alisema ujio wa Kikwete ni faraja kwao kwa kuwa wanaamini angezungumzia mambo yanayohusu sekta ya elimu.
  "Sisi tuna matatizo mengi. Vitabu hatuna; walimu wachache; hatuna vyoo na mambo mengine mengi yanayofanana na hayo. Ningefurahi kama rais atazungumzia matatizo hayo," alisema
  Akizungumza kwenye mkutano huo uliojaa wanawake na watoto, Kikwete alisema amekuja kuomba kura ili aendelee kuwa rais, akamilishe mambo mbalimbali aliyokwishayaanza.
  "Nakuja kuomba mtuchague tena kwa sababu tatu; Kwanza tumeongoza vizuri nchi hii na kwa amani na utulivu. Ingawa nchi bado maskini, lakini ni wazi kwamba kuna mengi CCM imefanya,"
  "Ninaposema tuchagueni ninamaana mimi niwe rais, ninaposema tuchagueni naamaanisha Donald Max kuwa mbunge weu na ninaposema tuchagueni naamanisha madiwani wa CCM."
  Katika mkutano huo Kikwete alieleza mambo kadhaa anayotarajia kuyasimamia katika kipindi cha uongozi wake ujao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa gati ya Nkome, umeme katika vijiji vyote vinavyoelekea kwenye kata hiyo iliyo kwenye tarafa ya Buganda na ujenzi wa lami katika eneo hilo.
  "Tukimaliza uchaguzi tunaanza kushughulikia suala la kugawanya mipaka. Kata hii ina watu 51,000, idadi ambayo ni nusu ya idadi ya watu kwenye wilaya na zaidi ya mara mbili ya tarafa," alisema Kikwete.
  "Niliahadi lami tumeweza, tutashindwaje kujenga gati," alihoji. "Mambo haya yanawezekana kwa serikali ya CCM."


  Angalia picha hii hapa chini: wengi ni watoto wa shule (zaidi ya 5000!) . Yaani Kikwete hawezi kuona umuhimu wa watoto kuendelea na masomo yao badala yake anawkatisha kwa starehe zake za utamu wa kurudi Ikulu?. Watu wa aina hii ndio hawaoni ubaya kwa kuwap[oteza watoto wa shule kwa faida zao binafsi ikiwa ni pamoja na kuwkatisha shule.

  Samahani sikuweza kupunguza ukubwa wa picha hiyo mara moja, nitafanya hivyo baadaye nikipata kanafasi.

  [​IMG]


  IMG_0890.JPG
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du, hawa jamaa kweli ni desperate!
   
 3. czar

  czar JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo ndo JK bwana mtu wa watu si ndo walivyosema, na bado, sasa utakuta wazazi wanaona sawa tu watoto wao kwenda kwenye kampeni. Hivi ina maana hao walimu walilipwa siku hiyo japo hawakufundisha sio? ufisadi ufisadi mtupu.
   
 4. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,806
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  It's plain hokum. If you can't convince 'em, confuse 'em. It's an old political trick. But this time it won't work.
  Harry S. Truman
   
Loading...