Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,864
- 155,820
Ndugu zangu,
Jana niliangalia taarifa ya habari ya usiku kwenye moja ya tv zetu. Ikaja habari kutoka Kampala, kwamba watu wamekamatwa kwa kunyunyuzia dawa za kuhifadhi maiti kwenye nyama na samaki ili zikae muda mrefu.
Wakati ubongo wangu ukitafakari kuwa nikiwa Kampala ni bora kula maharage taarifa ikaendelea kusema kuwa wengine wamekamatwa kwa kutumia panadol kuivisha maharage.
Baada ya habari kuhitimishwa mtangazaji anatamka; " Ni habari ya kusisimua hiyo!"
Mimi nilidhani ni habari ya kushtusha na kuogopesha sana. Je, wewe unasemaje?