Kampa-kampa tena, katiba ya Warioba imekwenda na maji?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,776
102,138
Wakuu Id-Mubarak,

Katika awamu ya nne tulikuwa na mchakato wa kupata katiba mpya. Na katika mchakato wa awali kulikuwa na Tume ya Katiba Mpya, miongoni mwa wajumbe wa Tume-vijogoo walikuwa ni mwenyekiti Jaji Joseph Warioba, Prof.Kabudi Paramagamba, Humphrey Polepole, Prof.Mwesiga Beregu na Dr.Sengondo Mvungi(R.I.P).

Kwa mujibu wa wachambuzi inaaminika kwamba katiba iliyoletwa na Tume ilikuwa katiba iliyojaribu kwa kiasi kikubwa kuchukua mawazo ya Watanzania.Ikaitwa Katiba ya Warioba.Watawala wakaiona ni disaster kwao inaenda kuwazamisha kwa sababu ndani yake kuna uwajibishwaji mkubwa sana wa watawala, mbaya zaidi kulikuwa na hitaji la Tume Huru ya Uhaguzi, na sio Tume ya CCM ''inayotangaza matokeo kama yanavyotumwa-in Lubuva's Voice''
Hakika CCM ni noma, kwenye uchaguzi mkuu 2015, baadhi ya wajumbe wakanaswa, Mwenyekiti Jaji Warioba na H.Polepole, hadharani wakawasaliti waliokuwa nyuma.

Warioba akasikika akisema walikwamisha katiba ya Warioba wamehamia CHADEMA. Polepole akapewa ukuu wa Wilaya huku interior,Katika teuzi za juzi kati mwanae Kippi Warioba akapewa tena, ikaonekana huyu Polepole ni mtu adimu sana aje town-akapewa tena.

Jana kabla jua halijazama, KAMPA-KAMPA TENA kwa wajumbe wa iliyokuwa tume ya katiba mpya ikaendelea. Mwanasheria Prof.Kabudi akapewa uenyekiti TIB.Mwanasheria na investment?Nadhani ni kwa kuwa tu Jaji Warioba amechachoka na umri umekwea, la sivyo naye angepewa!Inachotaka kusema ni kwamba, huu uteuzi mfululizo wa walikuwa wajumbe wa tume sio kunyamazisha makelele ya Katiba ya Warioba? Katiba ya Warioba itaendelea kuwepo na kupiganiwa?au imekwenda na maji
 
Aisee Pesa nyoko, Yan Polepole wa leo, huwez amin kama ndo yule wa Jana
Lakin wakuu mmefamnya utafiti mkaona kiwa kabadili msimamo wake kihusu katiba,? Au mnahisi atabadili msimamo baada ya kupewa cheo? Nadhan tuubiri kwnza atolee ufafanuzi kuhusu msimamo wake kuhusu katiba baada ya kupewa madaraka ndio tuanze kumuhukumu.
 
Wewe na tume yako shauri yako. Sisi ni mbele kwa mbele tu. Hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke. Wenye ngebe tayari kwa pocket. Mvungi RIP nani tena? Nikumbushe nani tena tumemsahau? Yupo kweli?
 
Hili suala la katiba mpya linatakiwa lirudi meza mapema tena ikibidi katika bunge linalokuja mwezi November.
Biashara ya kujadili mambo muhimu ya kikatiba ipewe kipao mbele mapema iwezekanavyo kabla ya 2020.
Alafu sasa tutambue jeuri ya CCM.
 
Nakubaliana na wewe. Nilitarajia mpambanaji kuingia pale tutaona changes. Nikaanza kuangalia. Siku mbali tu nikarudi kwa meku wangu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom