Kamishna wa kazi na Wizara ya uwekezaji mnafukuza wawekezaji

Nenda marekani ndo utajua, sio original, hapa, vitumwe na chuo vikiwa sealed....
Marekani ni nchi iliyoendelea kiviwanda na kiuwekezaji ndio maana hata visa ya Marekani kupata shida wanaringa pesa wanazo tena dola ambazo sisi tunahangaika kuitafutia pale ndio kwao wanazo tele.Huwezi iga Marekani Marekani akija Tanzania visa anapatia airport wewe mwenzangu na Mimi visa ya kwenda Marekani utahenya hadi ukome.Marekani wanahitaji wawekezaji bila kujali Wamesoma au la ila kiwango kinaanzia dola laki tano kwenda juu.Kama unazo kanunue municipal bonds za Marekani ukishanunua omba permanent resident permit ya kuishi Marekani kama mwekezaji wa hizo municipal bonds ulizonunua unapewa na permanent residence permit bila longo longo yoyote
 
Ikiwa kila siku tunaona kilio Bungeni na TIC wakililia mazingira ya uwekezaji kuwa rahisi na kupunguza ukiritimba, bado tunaona kuna Wizara zinajitunguia miongozo inayo kinzana na Sheria iliyopitishwa na Bunge na kusababishia Ugumu kwa wawekezaji kupata vibali vya kazi au vya makazi.

Jana nimeona tangazo la Kamishina wa kazi kwamba kwa mwekezaji anayetaka kibali cha kazi ni lazima kusubmit Vyeti halisi na sio nakala. Binafsi kama mdau katika sekta ya uwekezaji Nchini naona tunajipiga risasi miguuni na kuleta mazingira magumu bila sababu, nasema hivi kwa sababu zifuatazo
i) Sheria ya vibali vya kazi imetamka mahitaji ya mwekezaji anapoomba kibali cha kazi, sheria inasema certified copies ( nakala ya vyeti husika) sasa leo tunaona Kamishna anajitungia miongozo yake kwa kusema lazima kuwe na Vyeti Original

2) Sheria ya Uhamiaji na ya Vibali vya Kazi zinatamka wazi kwamba lazima maombi ya vibali yafanyike mwekezaji au mwajiriwa akiwa nje ya nchi, sasa unajiuliza nini maana ya kuwa na online system kama bado utamtaka mtu asafiri mfano toka Marekani kuleta vyeti halisi Dodoma ? ama nani ambaye yupo razi kutuma vyeti vyake nchini wakati hana uhakika wa kupata hicho kibali??

3) Unakuta mtu ana mtaji wa dola million 1 anataka kuwekeza nchini anaomba kibali cha kazi Class A, bado mnamuomba vyeti vya shule, nani kawaambia wawekezaji wote wameenda shule, mbona wafanyakazi tumekariri sana jamaniii.

OMBI LA HARAKA

Waziri wa uwekezaji naomba tumia mamlaka yako kufuta huu mwongozo mpya mnazidi kufukuza wawekezaji na kusababisha mazingira kuwa magumu ya kuwekeza nchini.

Woga wa nini? Kwani mna vyeti FEKI? Mbona Leseni na passport mnatembea nazo ORIGINAL....
 
Sasa mwekezaji katoka USA unataka akupe original academic certificate kwamba unataka kumdahili au?

Huko aliposoma wewe huna mawasiliano yao utahakiki vipi hivyo vyeti vyake? Au ndio kupoteza muda?

Mtu anataka kujenga kiwanda wewe unataka cheti chake cha form 4
Hii nji bwana
 
Ikiwa kila siku tunaona kilio Bungeni na TIC wakililia mazingira ya uwekezaji kuwa rahisi na kupunguza ukiritimba, bado tunaona kuna Wizara zinajitunguia miongozo inayo kinzana na Sheria iliyopitishwa na Bunge na kusababishia Ugumu kwa wawekezaji kupata vibali vya kazi au vya makazi.

Jana nimeona tangazo la Kamishina wa kazi kwamba kwa mwekezaji anayetaka kibali cha kazi ni lazima kusubmit Vyeti halisi na sio nakala. Binafsi kama mdau katika sekta ya uwekezaji Nchini naona tunajipiga risasi miguuni na kuleta mazingira magumu bila sababu, nasema hivi kwa sababu zifuatazo
i) Sheria ya vibali vya kazi imetamka mahitaji ya mwekezaji anapoomba kibali cha kazi, sheria inasema certified copies ( nakala ya vyeti husika) sasa leo tunaona Kamishna anajitungia miongozo yake kwa kusema lazima kuwe na Vyeti Original

2) Sheria ya Uhamiaji na ya Vibali vya Kazi zinatamka wazi kwamba lazima maombi ya vibali yafanyike mwekezaji au mwajiriwa akiwa nje ya nchi, sasa unajiuliza nini maana ya kuwa na online system kama bado utamtaka mtu asafiri mfano toka Marekani kuleta vyeti halisi Dodoma ? ama nani ambaye yupo razi kutuma vyeti vyake nchini wakati hana uhakika wa kupata hicho kibali??

3) Unakuta mtu ana mtaji wa dola million 1 anataka kuwekeza nchini anaomba kibali cha kazi Class A, bado mnamuomba vyeti vya shule, nani kawaambia wawekezaji wote wameenda shule, mbona wafanyakazi tumekariri sana jamaniii.

OMBI LA HARAKA

Waziri wa uwekezaji naomba tumia mamlaka yako kufuta huu mwongozo mpya mnazidi kufukuza wawekezaji na kusababisha mazingira kuwa magumu ya kuwekeza nchini.
Mkuu umeongea ukweli MTUPU ukiritimba umezidi sana watu wamejitungia miongozo yao kinyume na sheria husika.... mfano mdogo tu kuna watu niliwadirect kwa ajili ya uwekezaji....wakakwama kupata vibali vya kazi...kisa hawana vyeti original...pili walikuwa wakitumia kampuni ya uwakili kwa ajili ya ufatiliaji...cha kushangaza hawataki hawataki mawakili wafatilia hizo mambo.....ajabu sana...
 
Back
Top Bottom