Kamishna wa elimu. kwa walipa kodi awajibike ipasavyo kupanua wigo wa kodi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamishna wa elimu. kwa walipa kodi awajibike ipasavyo kupanua wigo wa kodi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohammed Shossi, May 2, 2012.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kati ya watanzania mil 40 ni Watanzania mil 1.2 tu ndio wana TIN hawa ni wa driving licence, magari, pikipiki na wafanyabiashara na VAT registered ni only 320,000! Kwa takwimu hizo inamaana TRA hawapo serious kwenye kukusanya kodi na hawatekelezi jukumu lao kuu ambalo ni "To raise substancial government revenue" Iffike mahali TRA na Serikali kwa ujumla iangalie vyanzo zingine vya mapato na sio kuongeza kodi kwenye bidhaa hizo hizo.


  Pale TRA kuna Commissioner for Tax Payer Education hawaelimishi watu kuhusu kodi anakula pesa ya umma ya bure tu! Sioni anafanya kazi gani hasa ilihali mtanzania wa kawaida hajui hata anatakiwa kodi gani alipe na kodi asilipe kuna malalamiko ya watu kubambikiwa kodi au kutishwa na maafisa wa kodi wasio waaminifu! Hii inatokana na wananchi kutokuwa na uweledi wa maswala ya kodi ambayo kamisna wa elimu kwa walipa kodi ndio kazi yake hasa na analipwa kwa ajili hiyo!

  Inauma zaidi kuona ni watz wachache sana wanalipa kodi na katika hicho kidogo kinachopatikaka kinaliwa viz kujenga banda la maonyesho ya nane nane kwa gharama ya 600 mil kama alivyosema Waziri wa afya! Hii hali inachangia pia watu kukwepa kodi lakini kama kodi zitatumika ipasavyo yaani kila ukienda sehemu unakutana na kodi yako. Ukienda Dondwe unakuta barabara safi ukienda Mwanuzi unakuta zahanati safi yenye dawa na wafanyakazi. Ukienda matombo unakuta shule safi yenye waalimu wazuri!
   
Loading...