Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,786
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema kuwa watu wote ambao wanaishi mabondeni watoke mara moja kwa sababu kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha na ambaye hatafanya hivyo atakamatwa., hivyo amewaagiza maOCD kuwakamata wote wanaoishi maeneo hatarishi ikiwemo mabondeni, yeye atajua sehemu ya kuwapeleka.
--------
Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam limewataka wananchi wote wanaoishi mabondeni jijini Dar es salaam kuhama mara moja, na kwamba kuanzia sasa jeshi hilo litapita kwenye mabonde yotekuwakamata wote watakaokaidi agizo hilo, kwani kazi ya jeshi hilo ni kulinda usalama wa raia na mali zao.
Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa kanda Maa;um ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro amesema jeshi la polisi haliwezi kuvumilia kuona watu wakipoteza maisha na wengine kuhatarisha usalama wa maisha na mali zao wakati moja ya kazi zake ni kuhakikisha usalama wao na mali zao, hivyo amekwishatoa muongozo kwa wakuu wa jeshi hilo katika wilaya zote za kanda yake.
Kamishna Sirro amesema kufuatia mvua zilizonyesha jana jijini dar es salaam zimesababisha kifo cha mtoto IMELDA NGONYANI mwenye umri wa miaka kumi na mitatu, aliyekutwa na mauti wakati anajaribu kuvuka mto Msimbazi alipokuwa akielekea shuleni kwake Mongo la Ndege ambako alikuwa anasoma darasa la tano ambapo wenzake watano aliofuatana nao walinusurika.
Chanzo: Mitandaoni