Kamishna Mkuu TRA Dr. Edwin P. Mhede, awanasa Wachina waliotaka kumpa rushwa ya dola 5,000/=. Wahukumiwa kulipa Tsh. Milioni 1 kila mmoja

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,174
4,062
Jana mida ya saa sita mchana ofisini kwa Kamishna mkuu wa TRA alipokea taarifa kutoka kwa watumishi mwenzake sio wa mamlaka ila mtumishi wa umma akimueleza kwamba kuna wateja walitaka kumuona, wana maswala yao ya kikodi wakidai kwamba wamewakadiria kodi kubwa kuliko wanavyopaswa kulipa kwa hiyo wakaomba kupata kikao na Kamishna mkuu ili waweze kueleza hiyo changamoto yao.

Kwa kuwa majadiliano na walipa kodi ni moja ya majukumu yake ya kikazi hivyo alitoa ruhusa kuonana nao, na hakuwepo ofisini mpaka majira ya saa kumi hivyo aliporudi aliwaita hao wageni na walipoingia walitoa karataasi ambazo zilionesha zinahitaji ufafanuzi wa Kamishna mkuu.

Kamishna anadai kuwa alishaweka sera ya kutokufanya kazi peke yake lazima awe na wasaidizi wake, hivyo wakati wageni hao wakiendelea kutoa maelezo wakatoa kibunda cha fedha za kimarekani, na Kamishna hakujua ni kiasi gani na "hapo kwa kweli ilinitoa kwenye reli nikaona hiki ni kitu ambacho sio cha kawaida" akawauliza kwa nini mnafanya hivyo wakadai tunakupa tu kama zawadi.

Akamwambia msaidizi wake ahesabu hizo fedha na zikawa ni dola 5000 akazikataa na hatua alizochukua ni kuwaambia waandike maelezo nao wakaandika kuwa walitaka kumpa fedha Kamishna mkuu akazikataa mbele ya shahidi ambaye ni msaidizi wake.

Kamishna mkuu akaamua kuwachunguza ili ajue ni kina nani akakuta hao ni wamiliki wa kampuni inayoitwa Rong Lan International Industry and Trade Company Limited ambayo ipo Mafinga Mkoani Iringa na kwenye taarifa za TRA zilionesha walikuwa wamekaguliwa muda mfupi na kukutwa na hatia ya kukwepa kodi kiasi cha shilingi Billion moja point 735 na nyaraka anazo kamishna mkuu wa TRA. Pia muda wa kulipa au kukomboa kodi ulikuwa umeisha tangu 21/02/2020 na Kamishna alikuwa kashatoa maagizo kwa watu wa sina hiyo kuwa ni lazima wakomboe kodi.

Pia Kamisha mkuu wa TRA ametoa taarifa kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa na mamlaka husika ambayo ni TAKUKURU.

Pia Kamishna amemaliza kwa kutoa Rai kwa watu wote kuto diliki kutoa rushwa kwani wao hawashawishiki bali wapo kusimamia sheria na hawataingia kwenye urafi wa fedha haramu.

UPDATE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan Intl Industry and Trade Co. Ltd, Zheng Rongman (50) na mkewe Ou Ya (47) kulipa faini ya Tsh. Milioni 1 kila mmoja

Pamoja na hukumu hiyo iliyotolewa leo na Hakimu Mkazi Huruma Shaidi baada ya washtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa la kutoa rushwa, pia Mahakama imetaifisha Tsh. Milioni 11.5 zao

 
Kamishna mkuu wa TRA Dr Nhene amekataa hongo ya dola za Marekani 5000 kutoka kwa raia wawili wa China ambao ni mtu na mkewe.

Wachina hao ni wawekezaji wa Kinyanambo, Mafinga mkoani Iringa.

Kamishna mkuu amesema wachina hao wanadaiwa kodi ya zaidi ya sh bilioni 1 na walijaribu kumuhonga ili awasaidie kulipunguza.

Wachina hao wamefikishwa mahakama ya kisutu na wamekiri kutenda kosa hilo.

Source ITV habari!
 
Nyendo, So what! Ma ccm shida Sana! Sasa dola 5000,Si pesa ya mboga tu, haifiki hata millioni 15Tsh,
Mlituibia billioni 400! Za escrow, melemeta, Richmond, sasa mnataka tuwaone watakatifu kwa kukataa millioni 11.!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mijitu inatafuta sifa kiboya sana, yaani kaishu kama hako ndio anaandikia bango kabisa ili jiwe aione na kuwapandisha cheo, mbona anapewa rushwa za milioni 500 na hakatai? ingekuwa ni rushwa ya milion 300 angekataa na kuitangaza? Tuache unafiki.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom