Kamishna Mkuu TRA Dr. Edwin P. Mhede, awanasa Wachina waliotaka kumpa rushwa ya dola 5,000/=. Wahukumiwa kulipa Tsh. Milioni 1 kila mmoja

Bongo movies zenu tumezichoka bana ni uwongo mtupu huu atafuta Sifa kwa boss wake ili aonekane yuko msafi kumbe mpigaji Mkubwa tu hana lolote
 
Hongera sana, sasa mahakama imesukwa upya, mchina kaenda mahakamani jana leo kala faini ya 2m, yeye 1m na mkewe 1m na 11m zimekwenda, arudi iringa akatafute 1.3bn yetu
 
Mtu kaweza kuhonga million kumi na moja anahukumiwa kulipa million 1 tu, angekua mzawa hapo angeambiwa kahujumu uchumi alipe million 100
 
Jana mida ya saa sita mchana ofisini kwa Kamishna mkuu wa TRA alipokea taarifa kutoka kwa watumishi mwenzake sio wa mamlaka ila mtumishi wa umma akimueleza kwamba kuna wateja walitaka kumuona, wana maswala yao ya kikodi wakidai kwamba wamewakadiria kodi kubwa kuliko wanavyopaswa kulipa kwa hiyo wakaomba kupata kikao na Kamishna mkuu ili waweze kueleza hiyo changamoto yao.

Kwa kuwa majadiliano na walipa kodi ni moja ya majukumu yake ya kikazi hivyo alitoa ruhusa kuonana nao, na hakuwepo ofisini mpaka majira ya saa kumi hivyo aliporudi aliwaita hao wageni na walipoingia walitoa karataasi ambazo zilionesha zinahitaji ufafanuzi wa Kamishna mkuu.

Kamishna anadai kuwa alishaweka sera ya kutokufanya kazi peke yake lazima awe na wasaidizi wake, hivyo wakati wageni hao wakiendelea kutoa maelezo wakatoa kibunda cha fedha za kimarekani, na Kamishna hakujua ni kiasi gani na "hapo kwa kweli ilinitoa kwenye reli nikaona hiki ni kitu ambacho sio cha kawaida" akawauliza kwa nini mnafanya hivyo wakadai tunakupa tu kama zawadi.

Akamwambia msaidizi wake ahesabu hizo fedha na zikawa ni dola 5000 akazikataa na hatua alizochukua ni kuwaambia waandike maelezo nao wakaandika kuwa walitaka kumpa fedha Kamishna mkuu akazikataa mbele ya shahidi ambaye ni msaidizi wake.

Kamishna mkuu akaamua kuwachunguza ili ajue ni kina nani akakuta hao ni wamiliki wa kampuni inayoitwa Rong Lan International Industry and Trade Company Limited ambayo ipo Mafinga Mkoani Iringa na kwenye taarifa za TRA zilionesha walikuwa wamekaguliwa muda mfupi na kukutwa na hatia ya kukwepa kodi kiasi cha shilingi Billion moja point 735 na nyaraka anazo kamishna mkuu wa TRA. Pia muda wa kulipa au kukomboa kodi ulikuwa umeisha tangu 21/02/2020 na Kamishna alikuwa kashatoa maagizo kwa watu wa sina hiyo kuwa ni lazima wakomboe kodi.

Pia Kamisha mkuu wa TRA ametoa taarifa kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa na mamlaka husika ambayo ni TAKUKURU.

Pia Kamishna amemaliza kwa kutoa Rai kwa watu wote kuto diliki kutoa rushwa kwani wao hawashawishiki bali wapo kusimamia sheria na hawataingia kwenye urafi wa fedha haramu.

UPDATE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan Intl Industry and Trade Co. Ltd, Zheng Rongman (50) na mkewe Ou Ya (47) kulipa faini ya Tsh. Milioni 1 kila mmoja

Pamoja na hukumu hiyo iliyotolewa leo na Hakimu Mkazi Huruma Shaidi baada ya washtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa la kutoa rushwa, pia Mahakama imetaifisha Tsh. Milioni 11.5 zao

Hii haikuwa kesi ya kuitangaza kama ilivyotangazwa. Yaani yeye angekataa tu na kuwaambia walipe tu hiyo kodi au angeicheki kuona kama kweli wamebambikiwa. Inawezekana kweli wamebambikiwa likodi likubwa kwani hii ndiyo kawaida ya TRA. Sioni mantiki ya kuipublicize kama ilivyofanyika halafu wamelipa faini milioni moja moja tu!!!! What is the big deal hapa!!!!
 
Back
Top Bottom