Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,191
- 4,104
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)imesema katika kipindi cha Ugonjwa wa Covid-19 baadhi ya Watanzania walitumia mwanya huo kujifanya Wagonjwa na kwenda kutibiwa nchini India ilhali wakiwa wamebeba dawa za kulevya. Hata hivyo licha ya kutumia mbinu ya kupata vibali vya kutibiwa nje ya nchi walikamatwa kutokana na intelejensia ya Wakaguzi kutoka Nchi mbalimbali zinazodhibiti dawa hizo.
Akizungumza Jijini Arusha wakati wa utoaji mafunzo kwa Watumishi wa Idara mbalimbali za Serikali ikiwemo uhamasishani wa mradi wa upunguzaji madhara kwa Watumiaji wa Dawa za Kulevya Mkoani Arusha, Kamishna Jenerali, Gerald Kusaya amesema Wasafirishaji wana mbinu mbalimbali za kusafirisha dawa hizo lakini Mamlaka hiyo imedhibiti
Kusaya ameomba Watumishi wa Afya kuwa makini wanapotoa vibali vya Wagonjwa kusafiri "Haiwezekani Mtu anaomba kibali kwenda kutibiwa nje ya Nchi anapewa halafu katika ugonjwa wa covid-19 anaenda kutibiwa ukimwangalia huyo mgonjwa mwenyewe unajiuliza sana Watu wa afya mtusaidie katika hili maana Watumiaji wa dawa za kulevya au Wasafirishaji wana mbinu nyingi na ukiondoka hata Tanzania salama utakamatwa nje ya Nchi na dawa zako na kifungo ni maisha au miaka 20 na 30 jela"