Kamishina wa Ardhi Rukwa, Mkuu wa Idara ya Ardhi Sumbawanga na Fagio Auctioner wananyanyasa wananchi Rukwa juu ya Kodi ya Ardhi

Mungu Tusamehe Afrika

Senior Member
Jan 18, 2022
139
203
Kichwa cha habari chahusika.

Kumekuwa na unyanyasaji na uvunjifu wa sheria ubaofantwa na Kamishina wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Rukwa,Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Sumbawanga na dalali kutoka mbeya anayeitwa Fagio Auctioneer.

Kiuhalisia dalali huyu ametafutwa na huyo Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Sumbawanga kwa jina Kabaghe ambaye analipwa 10% na Fagio Auctioneer kwa pamoja na Kamishina huyo wa ardhi.

Fagio Auctioneer kulingana na marekebisho ya sheria na. 5/2021 kifungu cha 49 kifungu kidogo cha 48A haruhusiwi kufanya kazi ya udalali wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Sunbawanga kwani hajateuliwa na Msajili wa Mabaraza ya Ardhi -Tanzania kuwa Dalali au Msambaza Nyaraka za Baraza za Ardhi na Nyumba-Sumbawanga aliyeteuliwa kufanya kazi hizo yupo ila Kamishina Msaidizi wa Ardhi -Sumbawanga na huyo Mkuu wa Idara ya Ardhi Manisipaa ya Sumbawanga hawataki kumtumia kwa vile aligoma kuwapatia 10% na alikataa kuwatoza wananchi gharama za kuwasambazia wito wa Baraza la Ardhi na Nyumba bure kwa sheria hailekezi hivyo.

Wanachokifanya na kukitaka ni kuwashitaki wananchi wanaodaiwa kodi kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba Sumbawanga kisha kuwatumia vibarua kusambaza Hati za Wito kwa wanachi kwa kuwalipa pesa kidogo ya kutwa wakati wao siyo wasambaza nyaraka wa Baraza la Ardhi na Nyumba Sumbawanga na hawarejeshi kwa kiapo hati hizo kwa kiapo na baadae wananchi wanaoitika Barazani hutozwa asilimia 10% kama gharama za dalali ambazo huingia mifukoni mwao na tena wao kujilipa posho ya uendeshaji wa zoezi hilo kutoka ofisini.

Kabla hata shauri kusikilizawa barazani Fagio Auctioneer hupewa kazi hiyo ya kuwadai wananchi kodi husika pasipokuwa na sifa wala kufuata taratibu ambapo hukamata nyumba hizo na kuanza kuziuza kinyemela kitu ambacho baadae kitaiingiza serikali na wananchi kwenye mgogoro na hasara kwa tamaa zao.

Ofisi ya Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa imekuwa ikilalamikiwa sana juu ya dhiruma na ubadhirifu hasa kwa kutengeneza migogoro ili kkujipatia fedha za rushwa chini ya kamishina huyo na Afisa Ardhi huyo Kabaghe ikiwemo kutoa hati mara mbilimbili na kudhurumu maeneo ya wananchi.

Haiingii akilini Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa Sumbawanga kwanini anakumbatiwa na ofisi ya Kamishina msaidizi wa ardhi mkoa wa Rukwa na kukalia vyeo ofisi mbili wakati watu wengine wapo huo ni urasimu.

Tunaomba mkuu wa mkoa,msajili wa mbaraza ya ardhi na waziri wa ardhi muingilie kati hawa watu wanatubyanyasa na pia kujilipa pesa za serikali kinyume na utaratibu kwa maslahi yao pasipo kufuata sheria kanuni na taratibu.

Hatukatai kushitakiwa kwa kudaiwa lakini sheria,kanuni na taratibu zifuatwe kamishina ashitaki Barazani, wadaiwa tuletewe hati za wito kupitia msambaza nyaraka wa baraza,tufike barazani, shauri lisikilizwe na baraza pasipokuingiliwa na Kamishina msaidizi wa ardhi na mkuu wa idara ya ardhi manispaa ya sumbawanga, hikumu itolewe, kamishina/mdai akishinda mdaiwa apewe muda wa kutekeleza hukumu ai kukata rufaa na akishindwa ateuliwe dalali wa baraza wa mkoa wa Rukwa atekeleze hukumu siyo aletwe dalali bora dalali, apewe notisi ya siku 14 mshindwa tuzo kulipa deni

Mshindwa tuzo akishindwa kutekeleza hukumu baraza litowe amri ya kuuza nyumba,dalali mteuliwa atanfaze kuuza kwa siku 30 baada ya uthaminishaji, nyumba ikiuzwa dalali apeleke gharama zake baraza lizipie alipwe kwanza yeye na baadae kamishina ndipo alipwe, pesa ikibaki arejeshewe mshindwa tuzo,kinyume na hapo utekelezaji wote utakuwa batili na unaweza kupingwa mahakama za juu na mshindwa tuzo kushinda.

Sasa huyu Afisa Ardhi Kabaghe yeye ni nani au anauwezo gani kuwashinda wenzie aweze kufanya kazi na kutoa maamuzi ofisi zote za ardhi mkoani Rukwa?

Ni wakati sasa atafutiwe sehemu nyingine kwani amekuwa ni tatizo katika ofisi za ardhi hapa Sumbawanga mhasibu yeye,mtunza ofisi yeye,mwanasheria yeye,transport officer yeye,hr yeye,msaidizi wa kamishina yeye,n.k.
 
Apr 8, 2015
26
57
Huko wataalam hawapataki ndo maana afisa ardhi yeye ndo surveyor yeye ndo mipango miji na yeye ndo Mkuu wa idara..ukienda kichwakichwa unaweza kufa huko Sasa Cha kufia nini wakati Engineering survey inalipa hata hapa town kidogo cadastral ndo imeyumba
 

PALANGAVANU

Member
Jan 3, 2011
27
4
Kwa maelezo yako wewe ndie msambaza nyaraka wa mkoa wa Rukwa na inaonekana ulinyimwa kazi ya kusambaza nyaraka hivyo umekuja kulalamika hapa.

Anyway wahusika wataona na kufanyia kazi
 

Mungu Tusamehe Afrika

Senior Member
Jan 18, 2022
139
203
Kwa maelezo yako wewe ndie msambaza nyaraka wa mkoa wa Rukwa na inaonekana ulinyimwa kazi ya kusambaza nyaraka hivyo umekuja kulalamika hapa.

Anyway wahusika wataona na kufanyia kazi
Hayo ni mawazo yako na ujinga wako kwanini nisiwe mwenyenyumba,dalali,ndugu ama raia mwema unakimbilia msamnaza nyaraka?
 

PALANGAVANU

Member
Jan 3, 2011
27
4
mwenyenyumba
Yaani kwa kusoma tu ulichoandika tu naweza predict mwandishi mwananchi asingeandika habari za msambaza nyaraka wala vibarua kwani hazimhusu ujira mdogo kwa vibarua we mwananchi unakuhusu nini na umejuaje kuwa vibarua wanalipwa ujira mdogo uliiona mikataba yao au unavithibitisho gani kwenye hoja yako. Kwa hiyo we mwananchi unaacha kutafuta pesa ulipe kodi ya ardhi unahangaika na ujira wa aliyekuletea bill itakusaidia nn

kama kweli ww ni mwananchi jipange namna ya kuwasilisha hoja zako nenda moja kwa moja kwenye issue yako achana na yale ulosikia na usiyo na uhakika. Kama umeonewa sema umeonewa nn ww binafsi hayo ya watu wengine waachie wahusika watayafikisha.

Lakini pia kwa mwananchi kuna namna ya kufikisha malalamiko kwa wahusika wapo wakuu wa wilaya, mikoa na wizara je huko umefika? Au we umeamua jf iwe njia yako kufikisha ujumbe nayo sawa lakini ni maamuzi yako.

Watu wengi huwa wanakuwa na hoja lakini wanashindwa kusaidiwa kwa kushindwa kupangilia hoja zao wanafikisha hoja kama majungu hivi.
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom