Kamishina Chagonja apatwa na kigugumizi kuhusu bomu lililolipuka Arusha.

Breki sina

Member
Jun 3, 2013
96
31
Akizungumza VoA muda mfupi anadai hajawaagiza chadema kupeleka ushahidi wao kwa Rais bali ni ushauri tu huku akijikanyanga kuwa kabla ya siku moja aliongea na mh Lema na kumwambia kuwa anaushahidi kuwa polisi hawakuhusika anamshangaa tena kubadilisha hiyo kauli yake,huku akidia mh mbowe alimweleza kuwa anafahamu kuwa polisi hawahusiki huyu si mwingine bali ndiyo huyu baada ya kifo cha Mwangosi kule Nyororo alisimama kwenye vyombo vya habari akikanusha kuwa mwandishi marehemu Mwangosi hajauwawa na polisi bali kuna kitu kizito kilitokea upande ule wa pili akimaanisha cdm nani anaweza kumuamini Chagonja kwa sasa,mfano wa pili kuonyesha kuwa Chagonja haaminiki ni kuhusu lile tukio la majeneza mjini Tarime kutelekezwa barabarani huko Nyamongo mie nilikuwepo Chagonja kwa sehemu kubwa alihusika kwenye mpango ule kwa kutorosha majeneza ya marehemu usiku wa manane,na maiti hizo zikatelekezwa njiani ambapo polisi walihusika na mauaji yale ni nani anaweza kumuamini Chagonja na timu huyo iliyoundwa na IGP,kuwa itatenda haki.
 
Hivi Chagonja anajisikiaje anaposimama kwenye public ambayo inafahamu udhaifu wake kuhusiana na kauli zake kuhusu kifo cha Mwangosi pamoja na scandal ya mkewe? Kweli kuna watu hawana aibu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Watu wa namna ya chagonja wamelewa na kuvimbiwa madaraka kichwani ni patupu na ni pilot controlled.

Uchungu wa kuuliwa ndugu jamaa na watoto wao haujawafika, naamini mjinga akierevuka mjanja huwa mashakani

Ni muda tu na siku si nyingi watanzania waliovumilia kwa muda mrefu maumivu watachukuwa hatua na akina chagonja watalia na kusaga meno.
 
Inasikitisha nchi hii vyombo vya dola Na usalama badala ya kulinda usalama wa raia Na Mali zao vimeamua kushiriki kwenye kuhujumu usalama Wa raia Na usalama Wa nchi!
 
Ikumbukwe kwamba kila nafsi itaonja mauti . Hakuna mwenye ujanja mbele ya muumba wakati wake ukifika hata uwe unalindwa na FBI bado mauti hupenya tu. Unaweza ukawadanganya wanadamu lkn mbele ya muumba hatuwezi kuficha kitu sijui siku hiyo ya mwisho itakuaje tu mara wenye haki , waliokatiliwa maisha yao kwa hila jinsi watavyokua wanamweleza Bwana yale waliyotendewa na wanadamu wenzao ee Mungu ama kweli siku hiyo itakuwa kilio na kusaga meno. Walikuwepo watawala wengi wenye nguvu lkn siku zao za kuishi duniani zilipoisha hawakua na jinsi isipokua kutii tu, sasa wamelala na nani anajua kinachowakabili huko. Naamini kilio cha mnyonge kitalipwa na mwenye haki.
 
Chagonja anayeshindwa kumchunguza mkewe anayelala naye kitanda kimoja
kwamba ni Mtusi na ni Tapeli la kutupa ndio ataweza kuchunguza Ugaidi? haya ni masikhara.

Duh! Kweli hapa Intelejensia ImeFail, Hivi huyu mama si ndiye alilamba hela za watu kwa dili la kuwaajiri TiSs na Takukuru ?
 
Kwa ulimwengu wa digital, huwezi ukadanganya kwa mbinu za enzi ya ujima,

Jamaa wamejifunza propaganda kwa enzi za zamani ambapo kufukia ukweli ni kutikisa tu ulimi,
Ushahidi wa Mwangosi kilichowaumbua ni ile video, na hawakuwa na pakutokea,
Hili la Arusha nalo ni hivyo hivyo maana kazi kubwa wanayofanya ni kujua video iko wapi kisha waharibu ushahidi.

Sasa ukimpa raisi video ili iweje, inamaana yeye hajui au ni kutafuta tu kujua jamii inajua kiasi gani hicho anachojua.

Kati ya vitu ambavyo huwezi kuviamini hata siku moja ni
1. police
2. ccm
3. wanaohusiana kwa ukaribu na hivi vyombo viwili.
 
Akizungumza VoA muda mfupi anadai hajawaagiza chadema kupeleka ushahidi wao kwa Rais bali ni ushauri tu huku akijikanyanga kuwa kabla ya siku moja aliongea na mh Lema na kumwambia kuwa anaushahidi kuwa polisi hawakuhusika anamshangaa tena kubadilisha hiyo kauli yake,huku akidia mh mbowe alimweleza kuwa anafahamu kuwa polisi hawahusiki huyu si mwingine bali ndiyo huyu baada ya kifo cha Mwangosi kule Nyororo alisimama kwenye vyombo vya habari akikanusha kuwa mwandishi marehemu Mwangosi hajauwawa na polisi bali kuna kitu kizito kilitokea upande ule wa pili akimaanisha cdm nani anaweza kumuamini Chagonja kwa sasa,mfano wa pili kuonyesha kuwa Chagonja haaminiki ni kuhusu lile tukio la majeneza mjini Tarime kutelekezwa barabarani huko Nyamongo mie nilikuwepo Chagonja kwa sehemu kubwa alihusika kwenye mpango ule kwa kutorosha majeneza ya marehemu usiku wa manane,na maiti hizo zikatelekezwa njiani ambapo polisi walihusika na mauaji yale ni nani anaweza kumuamini Chagonja na timu huyo iliyoundwa na IGP,kuwa itatenda haki.

Hata hivyo Serikali imejifunza kuhusiana na hizi timu za uchunguzi. Walimpa kazi mzee wa polanium kuhusu Rich.. na akatenda kweli nusura serikali ing'ooke. Unadhani leo watatuma mtu ambaye yuko serious tena ili watikisike?
 
Chagonja has reclaimed his brain and now he can see that using fear to exploit people is not something valid to this generation which believes that fear is nothing but something made of ignorance of someone's own self.
 
Ikumbukwe kwamba kila nafsi itaonja mauti . Hakuna mwenye ujanja mbele ya muumba wakati wake ukifika hata uwe unalindwa na FBI bado mauti hupenya tu. Unaweza ukawadanganya wanadamu lkn mbele ya muumba hatuwezi kuficha kitu sijui siku hiyo ya mwisho itakuaje tu mara wenye haki , waliokatiliwa maisha yao kwa hila jinsi watavyokua wanamweleza Bwana yale waliyotendewa na wanadamu wenzao ee Mungu ama kweli siku hiyo itakuwa kilio na kusaga meno. Walikuwepo watawala wengi wenye nguvu lkn siku zao za kuishi duniani zilipoisha hawakua na jinsi isipokua kutii tu, sasa wamelala na nani anajua kinachowakabili huko. Naamini kilio cha mnyonge kitalipwa na mwenye haki.

nimeipenda hiyo 'kilio cha mnyonge hulipwa na mwenye haki'
 
Hata hivyo Serikali imejifunza kuhusiana na hizi timu za uchunguzi. Walimpa kazi mzee wa polanium kuhusu Rich.. na akatenda kweli nusura serikali ing'ooke. Unadhani leo watatuma mtu ambaye yuko serious tena ili watikisike?
Hahahahaha umenichekesha sana mkuu kuhusu mzee wa Polanium. Hawatakaa wamteue tena au mzee Sitta.
 
Sasa kama chagonja aliongea na Mh Lema siku moja kabla na Lema akamwambia polisi hawahusiki,leo wanasema Mbowe na Lema wametoroka how?
Kwanini wakati Lema na Mbowe wanaongea nae wasikamatwe hapo?
Nina wasiwasi sana na huyu jamaa!
Watajuta tu walichofanya,watajikanyaga mwisho watatuambia ukweli tu!
Shame on him!!!!!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom