Kamisheni ya Kikwete Umoja wa Mataifa yamaliza kazi yake nchini Norway.

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
KAMISHENA YA UMOJA WA MATAIFA YA KUGHARAMIA FURSA ZA ELIMU YAKAMILISHA KAZI YAKE, OSLO.

Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kugharamia Fursa za Elimu Duniani iliyo chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mheshimiwa Gordon Brown imekamilisha kazi yake ya kuandaa Taarifa yenye mapendekezo ya kuiwezesha dunia kuhakikisha kila mtoto popote alipo duniani anapata fursa ya elimu ya ubora wa elimu unaolinganaifikapo mwaka 2030.

Kamisheni hiyo ya Elimu iliyoundwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa imefanya kikao chake cha majumuisho tarehe 2 Julai, 2016 jijini Oslo. Kufuatia Kikao hicho cha majumuisho kilichopitia ripoti ya Kamisheni na mapendekezo yake, ripoti ya Kamisheni sasa inatarajiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York tarehe 18 Septemba, 2016.

Akizungumza mara baada ya Kikao cha Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mmoja wa Makamisha wa Kamisheni hiyo ameelezea matumaini yake kuwa mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti iwapo yatatekelezwa yataiwezesha dunia kuhakikisha kuwa hakuna mtoto atakayeachwa nyuma kwa upande wa elimu bora ifikapo mwaka 2030 na kuendelea kama ilivyoazimiwa katika Malengo ya Dunia ya Maendeleo Endelevu (SDG). Ameendelea kueleza kuwa ili kufikia lengo hilo, hapana budi viongozi wa dunia wafanye maamuzi ya kimapinduzi ili kuwezesha kupatikana kwa fedha zitakazowezesha kila mtoto kila mahali alipo duniani apate fursa ya elimu na elimu yenye ubora unaolingana.

Kamisheni hiyo inayoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza
na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Elimu inaundwa na jopo la watu mashuhuri wakiwemo Mawaziri Wakuu Wastaafu, Mawaziri Wastaafu, Wafanyabiashara na Matajiri Wakubwa kutoka Sekta Binafsi na Wanaharakati kutoka Asasi za Kiraia duniani.
Wajumbe wa Kamisheni ya Elimu katika Picha ya Pamoja.jpg
 
Aliyosema Nyerere yametimia! walisoma bure kwa kodi za wakulima! walisogeze Taifa na leo wanaenda K uchangia mambo ya Elimu na wafanya biashara na private sector!! mbona Sh ukrani Kaumbwa+ Milugo na mbeya bila mtaala na syllabus miaka naenda Rudi hadi vilaza unaenda kufanya nn? Angeenda pombeJPM+ NDALI wachaako ukithamini hapo sawa!!!! ningeunga mikono hoja
 
Ulitaka afanyie mkutano huo Gezaulole au? Tusiwe na mawazo ya kuku,toka bandani kwenda kuchakua kutafuta wadudu na kurudi bandani! Tupatie maana halisi ya kuzurura na anachokifanya Kikwete.
Yaani umekaza misuli ili umtetee kikwete kwa tabia yake ya uzururaji bila faida
Unatatizo we sio bure
 
Nchi hii ina ****** wengi sana ukiambiwa huyu anaongoza watu kwa hii comment unaweza jiuliza hao wanaoongozwa akili zao zikoje .


Hongera sana JK tunakumiss .

labda wame-hack jamani. huyo dada ana akili tu!
 
Yaani umekaza misuli ili umtetee kikwete kwa tabia yake ya uzururaji bila faida
Unatatizo we sio bure
Jibu hoja.Watu wengine mmejaaliwa uzushi na ubishi mwingi tukija kwenye hoja yenye mashiko zinachipuka hoja za kitoto kama hii kwamba namtetea Kikwete,Mimi sio wakili wake na after all hakuna kesi dhidi yake katika mahakama yoyote kwamba anahitaji utetezi.Toa hoja ueleweke usipende kufuata mkumbomaneno.
 
Back
Top Bottom