Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inafanya nini wananchi wanapouawa mikononi mwa Polisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inafanya nini wananchi wanapouawa mikononi mwa Polisi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 24, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp]Siku ya tatu sasa tangu mauaji ya raia kutokea mjini Songea na hadi hivi sasa tayari tumesikia kauli toka Polisi Mkoa wa Ruvuma na uongozi wa kisiasa wa mkoa huo ambao umesema utaunda tume kuchunguza mauaji hayo. Wakati huo huo tumesikia Jeshi la Polisi Makao Makuu limemtuma Kamanda anayesimamia mafunzo Bw. Paul Chagonja kwenda kuchunguza kuhusika kwa jeshi hilo katika mauaji hayo. Hadi hivi sasa chombo pekee kilichopewa wajibu wa kikatiba wa kusimamia haki za binadamu nchini yaani Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iko kimya ikiachilia wahusika na watuhumiwa kuhusika na mauajia kuchungazana wenyewe.

  [/FONT]
  [FONT=&amp]Inashangaza kuwa hadi hivi sasa Kamisheni hii iko kimya wala kuonesha uharaka wa kuingilia kati sakata ili ili ukweli nao usiwe mhanga wa kwanza wa tukio hili. Tunafahamu hadi hivi sasa siyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma wala Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wana uwezo na uhuru wa kutosha kusimamia uchunguzi wowote na hatua za kuwakamata polisi wane kuwahoji ni kuchezea akili za Watanzania kwani viongozi hao tayari wameshahalalisha mauaji hayo na lolote litakalotokea yumkini itakuwa ni kuwabebesha lawama askari hao huku wakuu waliotoa baraka silaha za moto kutumika wakiachwa bila kuguswa. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kamisheni hii imewekwa Kikatiba kuwa ni kimbilio kwa Watanzania na mlinzi wa haki za Watanzania. Ukiondoa mahakama chombo hiki kimeundwa kikiwa na wajibu wa pekee wakusimamia vyombo vingine vyote linapokuja suala la haki za binadamu. Na kati ya haki hizo za binadamu hakuna haki ya msingi zaidi kama haki ya kuishi – kwani haki nyingine zote zinadhania uwepo wa haki hii. Haki ya kuishi haiwezi na haipaswi kuvunjwa kiholela na bila kujali matokeo (with impunity). Jeshi la Polisi nchini – chini ya Said Mwema na Mkuu huyu huyu wa Operesheni Bw. Paul Chagonja limekuwa ni tishio la haki hii ya msingi. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kamisheni hii haiitaji mtu aje kuitaarifu kuwa kuna uvunjivu wa haki za binadamu. Ibara ya 15:1a imeipa kamisheni hii madaraka ya kuanzisha uchunguzi wake yenyewe bila kuombwa au kupigiwa kelele na mtu mwingine. Ni kutokana na hili wananchi wengi hata hawajui uwepo wa kamisheni hii au uwezo wake. Ni nani anajua kuwa kamisheni hii ina madaraka ya kuleta mashtaka kwenye mahakama yoyote baada ya kukusanya ushahidi wake? Lakini hadi leo hii nani amewahi kusikia kamisheni hii imeleta mashtaka yoyote baada ya matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu? [/FONT]


  [FONT=&amp]Tunafahamu kuwa Kamisheni hii ina uwezo wa kumuita na kumhoji mtu yeyote na binafsi ningependa kusikia Kamisheni hii inawaita kina Kagonja ambaye bila kuangalia ushahidi amesimama hadharani na kuyahukumu maandamano ya wananchi wa Songea kuwa ni ya "kihuni". Ningependa kusikia Mkuu wa Polisi wa Ruvuma ambaye alisimama na kujaribu kuhalalisha mauaji hayo anaitwa na kweli kabisa hao askari wanne wanaoshikiliwa na Polisi waitwe nao kutoa maelezo yao walipewa amri na nani. [/FONT]

  [FONT=&amp]Ni matumaini yangu – na bila ya shaka – matumaini ya wapenda haki wote kuona kuwa Kamisheni hii inafanya kazi yake kwa haraka, uwazi na kwa uthubutu bila woga wala upendeleo wowote. Vinginevyo, maisha ya Watanzania yataendelea kuwa katika rehani ya polisi na polisi wataendelea kuyapopoa maisha hayo wakijua kuwa wanakingiwa kifua na wakuu wao na kwamba uongozi wa kisiasa hauna uthubutu wa kuingilia kati.[/FONT]

  [FONT=&amp] Hili ni kweli siyo katika suala hili tu la juzi la Songea bali pia hata katika lile sakata la madaktari ambapo uongozi wa kisiasa ulionekana kushindwa kujua umuhimu wa nini cha kufanya na kuhatarisha maisha ya wananchi. Tulitarajia wengine kamisheni ya haki za binadamu ingeangalia jambo lile kwa kutumia mwanga wa haki za binadamu na kuingilia kati ili kutetea maisha ya Watanzania ambao walijikuta kwenye njia panda ya wale wenye nguvu. Lakini Kamisheni hii haikutoa kauli yoyote wala kuonekana inatekeleza wajibu wake na hili ni aibu hasa kamisheni inayoongozwa na mmojawapo ya majaji wetu maarufu na waliobobea Bw. Amir Manento. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kama kamisheni hii haitoweza kusimamia na kupigania haki za wananchi na kuwa ya kwanza kupaza sauti yake unapotokea uvunjaji wa haki za binadamu Watanzania watumainie nini au nani? Kama hawa waliokula kiapo cha kufanya kazi zao kwa uadilifu bila upendeleo hawawezi kukemea jeshi la polisi kama walivyolaani mauaji ya wale 17 kule Mara nani mwingine ataweza kufanya hivyo? Kama kamisheni hii inashindwa kumkemea Bw. Paul Kagonja ambaye ni kamanda wa Mafunzo na Operesheni ambaye ni wazi mafunzo anayowapa polisi wetu ni mabovu na hatari kwa raia nani atamkemea? Ni mara ngapi sasa tumeona polisi waliopewa mafunzo chini ya Chagonja wakiuawa wananchi bila kujali (with impunity) halafu ni huyo huyo Kagonja anatumwa kwenda kuchunguza?

  [/FONT]
  [FONT=&amp]Hivi nani anamchunguza Kagonja wakati Kagonja anawachunguza wenzake? Nani anamuuliza aina ya mafunzo ambayo polisi wetu wamepewa chini ya Kagonja? Nani anaweza kumuuliza Mwema kuhusu suala la haki za raia na binadamu katika jeshi la Polisi? Kama siyo Kamisheni hii nani basi? Au tusubiri viongozi vijana – kama kweli wapo – wahoji juu ya hili? Au tusubiri wapinzani kwa sababu ndio wana uchungu zaidi na maisha ya Watanzania? [/FONT]

  Na wananchi wasipoiuliza kamisheni hii wakati haki zao zinavunjwa na utu wao kudharauliwa nani aiulize?

  Ukitaka kujua zaidi juu ya Kamisheni hii BONYEZA HAPA
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,298
  Likes Received: 22,082
  Trophy Points: 280
  Kamisheni ya hAki za binadamu nA utawala bora inanuka rushwa na ni mali ya CCM.
  Rushwa inapumbaza taifa letu
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mpaka uwasikie wewe ndio ujuwe kuwa wanafanya kazi? Unashindwa kufahamu kuwa hata huu uchunguzi uliotangazwa ni kazi ya Kamisheni?
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Uliwahonga nini?
   
 5. k

  king kong Senior Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cadres in public offices is ridiculous.
  Wanateuliwa wanalinda kazi zao on the expens of citizens lives
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani wao sio citizens? Hebu wacheni porojo zenu za kujaza chuki kila siku. Kuweni kidogo na fikra poeitive. Nyie kila kitu negative tu. basi hata huo upinzani ndio unakuwa hivyo? upinzani ni majukumu tena ni makubwa sana kuliko Serikali ilikyoko madarakani.

  Mnaweza mkaunda nyinyi tume yenu ya Haki za binaadam ya upinzani, mkafanya uchunguzi mkaelezea ukweli, sio mnakaa majungu tu saa zote. Nyie vipi? mna asili ya uchawi?
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hawa wanaingia mitaani wanazingira Ikulu na Ofisi za mkuu wa Mkoa bila taarifa wala ruksa ya kufanya maandamano, halafu waachiwe wanatazamwa macho? Tandika tu. Hawakuamua maandamano ya amani hawa, huo ni ugaidi, kuvamia ofisi ya Rais na Mkuu wa mkoa.

  Zile ofisi zinalindwa na askari wenye silaha, unafikiri zile silaha huwa za show tu. Unaambiwa usisogee huku, wewe unakuja tu, unaambiwa tawanyika wewe unaleta ubishi. Tandika tu. Wale askari wako kazini pale na wamepewa majukumu ya kulinda zile ofisi. Mimi hata nyumbani kwako nikija namna hiyo utantandika na silaha yoyote uliokuwa nayo, hata meno utntafuna kama hauna silaha nyingine. Au utangoja ushahidi?
   
 8. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo wanatumia watuhumiwa kuchunguza na wewe unaona sawa tu?
   
 9. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  haya yote ni matokeo ya kuunda taasisi zenye muelekeo wa kisiasa. Hii tume inaelekea inafanya kazi kwa maelekezo toka juu, ndio maana tumekuwa tukilalamikia sana madaraka makubwa ya rais, maana kama rais ndio anateua tume hii wajumbe wanawajibika kwake, ila kama tume ingekuwa inateuliwa na bunge ingewajibika kwa moja kwa moja kwa wananchi tume sio yetu ndio maana haitetei haki za raia wanaouwawa kama kuku,polisi wamegeuka mahakama katili sana ambayo inatoa hukumu ya kifo bila kesi au kumsikiliza mtuhumiwa,halafu Mwema aliyewahi kuwa interpol nae ametumbukia kwenye siasa, Kagonja alishahalalisha mauaji kwa kuita maandamano ya kihuni., na kuwa polisi wana akili wasingeweza kupiga risasi bure! sasa huko songea wanatumwa wakafanye nini tena wakati wameshatoa majibu??inaqshangaza pale polisi wanapojichuguza wenyewe haki itapatikana je?? Tume ya haki za binadamu ilitakiwa izibe hili gap lakini nayo ni kama inaunga mkono mauaji haya kwa kukaa kimya.Watanzania tujinasue hapa tulipo kwanza kwa kupata katiba safi pili mfumo wote uliopo sasa uwe wa jeshi la polisi, uwe wa serikali na taasisi zake ufumuliwe na kusukwa upya na hii itawezekana endapo tuweka serikali mpya chama kipya madarakani 2015! lazima mamlaka tuliopokwa na watawala hawa katili tuyahifadhi, wametukandamiza kwa wizi, ufisadi, huduma mbovu za afya elimu, miundo mbinu n.k hiyo haitoshi sasa wanatumiminia risasi, sasa tume NOOOO ITS ENOUGH
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sikiliza wewe, kila jeshi wana haki na moja ya kazi zao kuchunguza matokeo yanayowahusu hususan kukiwa kuna vifo. Hakuna askari anaeuwa bila kufanywa uchunguzi. Usiwe punguani.

  Ni polisi ya nchi ipi duniani ambayo haifanyi uchunguzi askari wake akiua au akiuliwa? ni lazima wajiridhishe kama aliuwa kwa haki au aliuwa bila haki. Na wamesha sema kama ikibainika kuwa hawajatenda haki watachukuliwa hatua za kisheria. Cha ajabu ni nini hapo?
   
 11. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Ndugu unashabikia kwa kuwa hajakupata wewe, huwezi amini kuna mtu amepigwa risasi simply alikuwa anataoka hospitali anapita tu wala hajui kuna maandamano ghafla kakutana na risasi!! ingekuwa wewe je ungejisikiaje?? pia hata kama wananchi walienda huko kote walibeba silaha?? walipewa fursa za kutoa dukuduku lao!! kwa mfano polisi wangewatuliza raia bila silaha au mabomu na kuwaahidi mkuu wa mkoa anatoka na kuongea nao vurugu zingetokea wapi??Usishangilie kifo au kuunga mkono mauaji na jinai polisi wamefundishwa njia mbalimbali za kuzuia ghasia bila kuua,
   
 12. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  ukiangalia picha za tukio la songea utaona raia walikua mikono mitupu,ina maana polisi hawana mbinu nyingine zaidi ya mtutu?kuna mama amepigwa risasi wakati akitokea hospitali sasa na huyu naye alikuwa anavamia ikulu?
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe ulitaka wachukuwe maelekezo kutoka chini? halafu matokeo jana, leo unataka tume ikupe ripoti? hivi huwa mnafikiri kabla ya kuandika?
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Soma kwa makini, wawe mikono mitupu au wawe wamebeba silaha, hawana haki ya kwenda kuivamia Ikulu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Kuna Askari wanalinda pale, ambao hawajui mnakuja kundi zima kuvamia kwanini. Wanakulamba risasi halafu maelezo baadae, hiyo ndio kazi yao, kulinda zile ofisi. Hawako pale kuchekelea wahalifu.
   
 15. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  kumbe kamisheni ya haki za binadamu na utawala bora ni kitengo cha polisi!!!
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe unavamiwa na kundi la watu, utaanza kuwaambia haya mnaotoka hospitali kaeni pembeni?

  Mnaambiwa tawanyika! kama hamjatawanyika mnalambwa risasi. Huwezi kuvamia Ofisi ya Rais na ya Mkuu wa Mkoa uwachiwe, nani wewe?
   
 17. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  nani kasema wale ni wahalifu?kwa hiyo polisi wamekuwa mahakama?
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kamisheni ni kitu kingine na Polisi kitu kingine. Hivi wewe unaufahamu haswa? hujui kuwa jeshi la polisi lazima lichunguze kila kifo kilichsababishwa na askari wake? na hiyo haihusiani kabisa na kamisheni.

  Kamisheni unayoongelea, vitokee vifo jana, leo wawe wameshakupa ripoti, wameshachunguza, wameshafika Songea? hivi umesha amka au bado umelala?

  Usichanganye na uchunguzi wao wa ndani polisi na uchunguzi wa kamisheni ya haki, au tume nyingine yoyote itakayoundwa, hiyo uliyoisikia ni tume ya polisi ya ndani. Hebu funguka kidogo.
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Yeyote anaevamia Ikulu au Ofisi za Mkuu wa Mkoa bila taarifa na kuizingira ni mhalifu, tena ni gaidi. Sheria za Ugaidi si Mkapa alizipitisha mbiombio bungeni, au huzijui?
   
 20. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  soma post #3 uliyoiweka saa 07:14 halafu ujipange!
   
Loading...