Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Stor inaanzia miaka zaid ya 20 iliyopita ambapo wawili hawa wote wakiwa watumishi katika shirika moja, walikuwa katika mahusiano yaliyofikia stage ya uchumba na kutambulishana nyumbani. Kwa sababu ambazo wanajua wao, mwanaume aliamua kuvunja mahusiano, hali inayosemekana ilimuumiza sana msichana. Miaka imeenda mwanaume kaja kuoa mwingine na mwanamke hakuolewa japo mungu kamjaalia watoto kadhaa. Hapa miaka ya karibuni, yule mwanamke akiwa tayari ni mama wa makamo, kabahatika kuteuliwa kuwa 'boss' katika shirika lile, na mojawapo ya wafanyakazi wake akawamo yule baba.
Kwa bahati mbaya (au pengine kwa mtego), yule baba alikuja kumess up katika kazi, na ikawa inabidi huruma ya 'boss' ndio inayobeba mustakabali wa ajira yake (miaka michache kabla ya kustaafu)...
'Boss' akaamua nae atumie rungu lake, kumuonyesha jamaa kuwa umeingia kwenye anga zangu na akamtamkia kabisa kuwa kwa jinsi ulivyoniumiza wakati umeniacha miaka ile ya 80, lazima nikufanyizie..
..."ama andika barua ya kustaafu kwa hiari, au naukusanya na kuuambatanisha ushahidi huu, nikufukuze kazi"... hayo ndiyo yalikuwa maamuzi ya 'boss' huyu ambaye angeweza kumuonya au kumuambia aandike tu barua ya kuomba msamaha na kuahidi kutorudia tena. Mzee wa watu hakuwa na namna, baada ya kumpigia boss magoti kuomba msamaha ikashindikana, ikabidi aandike barua ya kustaafu kwa hiari kabla ya umri muafaka. mzee wa watu hakuwa amejiandaa kwa kadhia kama hiyo, na kwa namna ya kusikitisha maisha yake yaliharibika ghafla, lakini Mungu sio Athumani, thanks kufunguliwa kwa UDOM ambako alikuja kupata ajira kama ile alokuwa anafanya awali?
Sijui kama ni kawaida kwa maumivu ya mapenzi kuwa makali kiasi hicho cha kuja kulipiza kisasi miaka zaidi ya ishirini baadae...