Kamharibia mwenzake maisha, kwa kisa kuwa aliwaahi kumkataa miaka ya nyuma...

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
7,288
Stor inaanzia miaka zaid ya 20 iliyopita ambapo wawili hawa wote wakiwa watumishi katika shirika moja, walikuwa katika mahusiano yaliyofikia stage ya uchumba na kutambulishana nyumbani. Kwa sababu ambazo wanajua wao, mwanaume aliamua kuvunja mahusiano, hali inayosemekana ilimuumiza sana msichana. Miaka imeenda mwanaume kaja kuoa mwingine na mwanamke hakuolewa japo mungu kamjaalia watoto kadhaa. Hapa miaka ya karibuni, yule mwanamke akiwa tayari ni mama wa makamo, kabahatika kuteuliwa kuwa 'boss' katika shirika lile, na mojawapo ya wafanyakazi wake akawamo yule baba.
Kwa bahati mbaya (au pengine kwa mtego), yule baba alikuja kumess up katika kazi, na ikawa inabidi huruma ya 'boss' ndio inayobeba mustakabali wa ajira yake (miaka michache kabla ya kustaafu)...

'Boss' akaamua nae atumie rungu lake, kumuonyesha jamaa kuwa umeingia kwenye anga zangu na akamtamkia kabisa kuwa kwa jinsi ulivyoniumiza wakati umeniacha miaka ile ya 80, lazima nikufanyizie..
..."ama andika barua ya kustaafu kwa hiari, au naukusanya na kuuambatanisha ushahidi huu, nikufukuze kazi"... hayo ndiyo yalikuwa maamuzi ya 'boss' huyu ambaye angeweza kumuonya au kumuambia aandike tu barua ya kuomba msamaha na kuahidi kutorudia tena. Mzee wa watu hakuwa na namna, baada ya kumpigia boss magoti kuomba msamaha ikashindikana, ikabidi aandike barua ya kustaafu kwa hiari kabla ya umri muafaka. mzee wa watu hakuwa amejiandaa kwa kadhia kama hiyo, na kwa namna ya kusikitisha maisha yake yaliharibika ghafla, lakini Mungu sio Athumani, thanks kufunguliwa kwa UDOM ambako alikuja kupata ajira kama ile alokuwa anafanya awali?

Sijui kama ni kawaida kwa maumivu ya mapenzi kuwa makali kiasi hicho cha kuja kulipiza kisasi miaka zaidi ya ishirini baadae...
 
Ave Ave Maria

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,735
5,613
Binadamu tunatofautiana kuna wengine the way alivyokupenda sana ndivyo atakavyokuchukia, sasa hawa hata kulipa kisasi ni kitu cha kawaida! Yaani kwa maumivu uliyomsababishia, kila akikumbuka anakuona we kama mnyama na haustahili kupewa yaliyo mema!!
 
Nailyne

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
350
111
acha kabisa na suala la maumivu ya mapenzi kuna watu hawasamehi kabisa akitendwa, anajiapiza akapata chance lazima alipize.., binadamu tumeumbwa tofauti na uwezo wetu wa kupokea na kukubali vile watu wengine wanatufanyia inategemea mtu na mtu embu fikiria huyo mama analo hilo donge kwa zaid ya miaka 20!!
 
Vin Diesel

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
9,095
6,321
Hapa najiuliza huyo mama aliwezaje kupata nafasi kama hiyo wakati ana maamuzi kama haya...
Au ndio mambo ya tukiwezeshwa,tunaweza?
 
newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,377
538
bado alimfanyia utu,angeweza kumfukuza bila kumpa nafasi ya kuandika barua ya kustaafu,na ingekuwa ngumu kwake kuajiriwa tena ktk tasisi kama udom.
2-ili amsamehe ingebidi bosi apindishe maamuzi kwa upendeleo,lakini ilishadhiirika kuwa jamaa si muaminifu,aliona haina sababu kurisk her neck kwa ajili ya mtu ambaye alishampa boot wakati wa ujana
 
Kyalow

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,415
2,322
msamahaa ni muhimu sana vitabu vya mungu vinasema...ingawa wanadamu wana msemo wao usimuinglie adui wako anapofanya makosa
 
fabinyo

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,828
1,658
sishangai,maumivu hayo atakuwa nayo ukizingatia hajawahi kuolewa tena!na hao watoto itakuwa ni matokeo ya kumwacha kiama,maskini akawa anajitupia kwa kila mwanaume tu...
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,332
Stor inaanzia miaka zaid ya 20 iliyopita ambapo wawili hawa wote wakiwa watumishi katika shirika moja, walikuwa katika mahusiano yaliyofikia stage ya uchumba na kutambulishana nyumbani. Kwa sababu ambazo wanajua wao, mwanaume aliamua kuvunja mahusiano, hali inayosemekana ilimuumiza sana msichana. Miaka imeenda mwanaume kaja kuoa mwingine na mwanamke hakuolewa japo mungu kamjaalia watoto kadhaa. Hapa miaka ya karibuni, yule mwanamke akiwa tayari ni mama wa makamo, kabahatika kuteuliwa kuwa 'boss' katika shirika lile, na mojawapo ya wafanyakazi wake akawamo yule baba.
Kwa bahati mbaya (au pengine kwa mtego), yule baba alikuja kumess up katika kazi, na ikawa inabidi huruma ya 'boss' ndio inayobeba mustakabali wa ajira yake (miaka michache kabla ya kustaafu)...

'Boss' akaamua nae atumie rungu lake, kumuonyesha jamaa kuwa umeingia kwenye anga zangu na akamtamkia kabisa kuwa kwa jinsi ulivyoniumiza wakati umeniacha miaka ile ya 80, lazima nikufanyizie..
..."ama andika barua ya kustaafu kwa hiari, au naukusanya na kuuambatanisha ushahidi huu, nikufukuze kazi"... hayo ndiyo yalikuwa maamuzi ya 'boss' huyu ambaye angeweza kumuonya au kumuambia aandike tu barua ya kuomba msamaha na kuahidi kutorudia tena. Mzee wa watu hakuwa na namna, baada ya kumpigia boss magoti kuomba msamaha ikashindikana, ikabidi aandike barua ya kustaafu kwa hiari kabla ya umri muafaka. mzee wa watu hakuwa amejiandaa kwa kadhia kama hiyo, na kwa namna ya kusikitisha maisha yake yaliharibika ghafla, lakini Mungu sio Athumani, thanks kufunguliwa kwa UDOM ambako alikuja kupata ajira kama ile alokuwa anafanya awali?

Sijui kama ni kawaida kwa maumivu ya mapenzi kuwa makali kiasi hicho cha kuja kulipiza kisasi miaka zaidi ya ishirini baadae...

Mimi sioni kama hicho ni kulipa kisasi, labda kama sijaelewa, mama katimiza majukumu yake kama Boss, kumbguka kwamba mama huyu alifika hapo na kuwa Boss na alimkuta huyo mzee, kama angkuwa anataka kulipa kisasi asingengoja mpaka mzee huyo afanye kosa angemtafutia visa vidogo vidogo hadi mzee aache kazi mwenyewe. lakini labda niseme tu kuwa sisi tumefundishwa kuangalia upande mbaya wa kila jambo, hilo ni kosa kubwa. kama watu tukijifunza kuangalia kila tukio linalotutokea kwa jicho la tatu, hakika kusingekuwa na tukio baya maishani.
Si mmeona hata huyo mzee amapata kazi U DOM na huenda huko ana raha kuzidi pale alipokuwepo awali.
Na Pengine anamshukuru yule mama yaani Boss aliyemfukuza kazi.
Kumbuka kwamba hata kufukuzwa kazi ni BARAKA!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom