Kamera za Kamanda Kova

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Kamera kuwekea gesti: Kova ajiwa juu...!

2008-06-30 16:20:23
Na Waandishi Wetu, Jijini

Wazo la Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, la kutaka hoteli na nyumba zote za kulala wageni almaarufu kama gesti zifungiwe kamera maalum za usalama limepokelewa tofauti na baadhi ya wadau ambao wengine wameliunga mkono huku baadhi wakimjia juu Kamanda huyo na kumtaka aache suala hilo.

Wakizungumza la Alasiri kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, baadhi ya wadau hao wamedai kuwa wazo la Kamanda Kova, likitekelezwa linaweza kuleta madhara makubwa, hasa kwa wale wanaofanya baishara ya gesti mitaani na pia wateja wao, wakiwemo madada wanaojiuza almaarufu kama machangudoa au \'ma-cd\' na vibosile wanaowachukua kila kukicha.

``Nimestushwa sana na pendekezo hilo la Kamanda Kova... ingawa moyo wake ni safi na dhamira yake ina lengo zuri la kutuhakikishia usalama, kamwe siungani naye kwa sababu likitekelezwa, sisi wenye gesti tutapata hasara kubwa,`` akasema mmiliki mmoja wa gesti maarufu iliyopo katika eneo la Sinza.

Akifafanua zaidi, mmiliki huyo akasema:``Baadhi ya wateja wetu wanafahamika kuwa si wageni kweli bali ni watu wenye wake zao.

Tena wengine wana heshima kubwa katika jamii.

Kwa sababu hiyo, hawatakuwa tayari kunaswa na hizo kamera, matokeo yake siye tutakufa njaa kwa kupoteza wateja wa namna hii ambao kwakweli ndio wengi zaidi kwenye majumba yetu haya ya wageni. Na Serikali pia itapoteza mapato yatokanayo na kodi tunazolipa,`` akasema mmiliki huyo.

Mfanyabiashara mwingine akasema wazo la Kova likitekelezwa, mbali na kutishia biashara yao kwa kukosa wateja na pengine watu waliowaajiri kupoteza kazi, pia itawagharimu pesa nyingi katika kuzifunga.

``Hizi kamera si rahisi... zinahitaji pesa nyingi ambazo kwa sisi wenye gesti za uswahilini zinaweza kutushinda. Ni bora tuendelee na mbinu hii ya kushirikiana na polisi kwa kuwapa taarifa za wateja wetu wanaoshukiwa kwa uhalifu badala ya ya kufunga kamera,`` akasema mmiliki mwingine wa gesti moja iliyopo katika eneo la Tandika Jijini.

Aidha, madada poa wanaoishi kwa kutegemea biashara chafu ya kujiuza miili yao almaarufu kama ma-cd, nao wamemuwakia Kamanda Kova na kumtaka asi1tekeleze wazo lake hilo kwa kile wanachodai kuwa linaweza kuwakimbiza mjini kwa njaa.

``Nikwambieni ndugu zangu... sisi wateja wetu wengi ni waume za watu na wengine ni wafanyabiashara maarufu. Pia wapo vigogo wenye heshima zao katika jamii. Haya mambo ya kufunga kamera gesti yatawakimbiza kwa sababu hawapendi kujulikana. Na sisi hatuna maeneo mengine ya kumalizana nao zaidi mahotelini na kwenye magesti. Aache (Kova), asije akatuua kwa njaa,`` akasema dada mmoja aliyejitambulisha kama Anti R, mkazi wa Manzese Uwanja wa Fisi.

Cd mwingine wa maeneo ya Kinondoni Jijini akamtaka Kova na Jeshi lake la Polisi washupalie majambazi kwa staili nyingine na si hiyo ya kufunga kamera kwenye gesti.

``Atuache kama tulivyo... hayo makamera yatatuharibia mambo yetu. Yeye ashirikiane vizuri na sisi ili tumpe data kwa sababu hata majambazi pia ni wateja wetu wazuri,`` akasema.

Aidha, baadhi ya vibosile wamedaiwa kutofurahia wazo hilo la Kova, kutokana na hofu yao ya kuumbuka pindi kamera zikifungwa katika gesti zote Jijini.

Hata hivyo, wakazi wengine waliozungumza na Alasiri wameunga mkono wazo la Kamanda Kova na kusema kuwa pindi kamera hizo zikifungwa, matukio ya uhalifu yanaweza kupungua kwa kiasi kikubwa Jijini.

``Sura zao zitaweza kufahamika na hili linamaanisha kuwa wahusika wataweza kudakwa kirahisi,`` amesema Mzee Shomvi, mkazi wa maeneo ya Ilala.

Kamanda Kova amekaririwa wakati akiwaambia wamiliki wa gesti na hoteli akisema kuwa njia mojawapo inayoweza kuwadhibiti majambazi na wahalifu wengine ni kufunga kamera kwenye nyumba za kulala wageni (gesti) na kwenye hoteli zote Jijini, kwani uzoefu unaonyesha kuwa wengi hukodi vyumba na kujificha kwenye majengo hayo kabla ya kufanya uhalifu.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Kamanda Kova amesema yeye alitoa ushauri tu kwa wenye nyumba hizo kwa ajili ya usalama wao na wala sio amri.

``Huo mimi nimetoa ushauri tu kwa wenye nyumba za kulala wageni kwa ajili ya usalama wao na raia wengine,`` akasema Kamanda Kova.

Aidha amesema kuwa amependekeza kamera hizo zifungwe sehemu za mapokezi tu na wala sio vyumbani, au sehemu nyingine ambako zinaweza kuingilia uhuru wa mtu.

``Kamera hizo hazifungwi chumbani, mimi nimependekeza zifungwe kwenye maeneo ya mapokezi ili kupata picha za watu wanaoingia na kutoka kwa ajili ya usalama wao tu,`` akasisitiza Kamanda Kova.

Aidha Kamanda Kova amesema tayari ameshafanya utafiti Jijini Dar es Salaam na kubaini kuwa zipo kamera nzuri na zenye bei poa zinazoweza kutumika sehemu hizo.

SOURCE: Alasiri
 
Ni wazo zuri litapunguza kasi ya maambukizi ya ukimwi, ujambazi,mmomonyoko wa maadili,pamoja na wimbi la biashara ya uchangudoa nadhani ni suala muafaka kama kuna anayepinga huyo atakuwa aitakii mema jamii ya watanzania.
 
...
``Nimestushwa sana na pendekezo hilo la Kamanda Kova... ingawa moyo wake ni safi na dhamira yake ina lengo zuri la kutuhakikishia usalama, kamwe siungani naye kwa sababu likitekelezwa, sisi wenye gesti tutapata hasara kubwa,`` akasema mmiliki mmoja wa gesti maarufu iliyopo katika eneo la Sinza.

Akifafanua zaidi, mmiliki huyo akasema:``Baadhi ya wateja wetu wanafahamika kuwa si wageni kweli bali ni watu wenye wake zao.

Tena wengine wana heshima kubwa katika jamii.

Kwa sababu hiyo, hawatakuwa tayari kunaswa na hizo kamera, matokeo yake siye tutakufa njaa kwa kupoteza wateja wa namna hii ambao kwakweli ndio wengi zaidi kwenye majumba yetu haya ya wageni. Na Serikali pia itapoteza mapato yatokanayo na kodi tunazolipa,`` akasema mmiliki huyo.

Mfanyabiashara mwingine akasema wazo la Kova likitekelezwa, mbali na kutishia biashara yao kwa kukosa wateja na pengine watu waliowaajiri kupoteza kazi, pia itawagharimu pesa nyingi katika kuzifunga.

``Hizi kamera si rahisi... zinahitaji pesa nyingi ambazo kwa sisi wenye gesti za uswahilini zinaweza kutushinda. Ni bora tuendelee na mbinu hii ya kushirikiana na polisi kwa kuwapa taarifa za wateja wetu wanaoshukiwa kwa uhalifu badala ya ya kufunga kamera,`` akasema mmiliki mwingine wa gesti moja iliyopo katika eneo la Tandika Jijini.

Aidha, madada poa wanaoishi kwa kutegemea biashara chafu ya kujiuza miili yao almaarufu kama ma-cd, nao wamemuwakia Kamanda Kova na kumtaka asi1tekeleze wazo lake hilo kwa kile wanachodai kuwa linaweza kuwakimbiza mjini kwa njaa.

``Nikwambieni ndugu zangu... sisi wateja wetu wengi ni waume za watu na wengine ni wafanyabiashara maarufu. Pia wapo vigogo wenye heshima zao katika jamii. Haya mambo ya kufunga kamera gesti yatawakimbiza kwa sababu hawapendi kujulikana. Na sisi hatuna maeneo mengine ya kumalizana nao zaidi mahotelini na kwenye magesti. Aache (Kova), asije akatuua kwa njaa,`` akasema dada mmoja aliyejitambulisha kama Anti R, mkazi wa Manzese Uwanja wa Fisi.

Cd mwingine wa maeneo ya Kinondoni Jijini akamtaka Kova na Jeshi lake la Polisi washupalie majambazi kwa staili nyingine na si hiyo ya kufunga kamera kwenye gesti.

``Atuache kama tulivyo... hayo makamera yatatuharibia mambo yetu. Yeye ashirikiane vizuri na sisi ili tumpe data kwa sababu hata majambazi pia ni wateja wetu wazuri,`` akasema.

Aidha, baadhi ya vibosile wamedaiwa kutofurahia wazo hilo la Kova, kutokana na hofu yao ya kuumbuka pindi kamera zikifungwa katika gesti zote Jijini.

...kwa hali hii tatizo ni kubwa kuliko linavyofikirika!

Tanzania bila UKIMWI na ujambazi, HAIWEZEKANI!
 
aanzie huko huko kwenye magesti, aendelee kwenye kona zenye ujambazi na pia vituo vya polisi.
Kwamba polisi imeoza, ni vizuri wajisafishe lakini wasiache kufanya kazi nyingine wakati wanajisafisha.
Tuko nyuma yako kamanda,
wazo zuri, sasa ni utekelezaji tu.
isije ikawa tena siasa
 
Kamera kuwekea gesti: Kova ajiwa juu...!

2008-06-30 16:20:23
Na Waandishi Wetu, Jijini

Aidha, madada poa wanaoishi kwa kutegemea biashara chafu ya kujiuza miili yao almaarufu kama ma-cd, nao wamemuwakia Kamanda Kova na kumtaka asi1tekeleze wazo lake hilo kwa kile wanachodai kuwa linaweza kuwakimbiza mjini kwa njaa.

``Nikwambieni ndugu zangu... sisi wateja wetu wengi ni waume za watu na wengine ni wafanyabiashara maarufu. Pia wapo vigogo wenye heshima zao katika jamii. Haya mambo ya kufunga kamera gesti yatawakimbiza kwa sababu hawapendi kujulikana. Na sisi hatuna maeneo mengine ya kumalizana nao zaidi mahotelini na kwenye magesti. Aache (Kova), asije akatuua kwa njaa,`` akasema dada mmoja aliyejitambulisha kama Anti R, mkazi wa Manzese Uwanja wa Fisi.

Cd mwingine wa maeneo ya Kinondoni Jijini akamtaka Kova na Jeshi lake la Polisi washupalie majambazi kwa staili nyingine na si hiyo ya kufunga kamera kwenye gesti.

``Atuache kama tulivyo... hayo makamera yatatuharibia mambo yetu. Yeye ashirikiane vizuri na sisi ili tumpe data kwa sababu hata majambazi pia ni wateja wetu wazuri,`` akasema.

...kwa hali hii tatizo ni kubwa kuliko linavyofikirika!

Tanzania bila UKIMWI na ujambazi, HAIWEZEKANI!

Nimecheka niliposoma comment yako; ukweli mtupu!

.
 
Hili Wazi Ni Safi N Litekelezwe Mapema, Kama Kuna Wanaofikiri Maisha Bila Guest Hayawezeni Wafikirie Namna Nyingine, Tatizo Langu Ni Kova Ninayemfahamu Kwa Muda Mrefu, Ni Mwerevu Kujijenga Kwenye Vyombo Vya Habari Lakini Ni Mlegevu Kwenye Utendaji. Tuliokuwa Mbeya Kwenye Kipindi Chake Tulishafikiri Kuwa Mbeya Imemshinda, Kumbe Igp Wake Alikuwa Anfikiri Tofauti
 
au alielewa sana somo la polisi shirikishi katika ile semina elekezi?
manake kuna mambo yao haya ya polisi jamii sijui nini
hata mimi nilimuona huko mbeya kama mtendaji anayeangalia kama ishu yake imejulikana ndio anapata nguvu zaidi.
Ila nasikia kipindi yuko mbeya uchunaji wangozi ulipotea, ila ulianda wizi wa maalbino,
 
aanzie huko huko kwenye magesti, aendelee kwenye kona zenye ujambazi na pia vituo vya polisi.
Kwamba polisi imeoza, ni vizuri wajisafishe lakini wasiache kufanya kazi nyingine wakati wanajisafisha.
Tuko nyuma yako kamanda,
wazo zuri, sasa ni utekelezaji tu.
isije ikawa tena siasa
Kama kawaida ya viongozi wetu,ni wazo lisilofanyiwa utafiti.Hatuna sababu ya kupongeza.
 
Kamanda Kova vita juu ya wapiga debe isukwe haraka iwezekanavyo. hawa watu wanavuna wasipopanda. Mtu katoka nyumbani najua naenda wapi wao wanapiga kelele na kulazimisha kulipwa, na wengine wanapora wasafiri. WASHUGHULIKIE WATAFUTE KAZI INAYOWAFAA HAWANA TOFAUTI NA MA CD
 
...kwa hali hii tatizo ni kubwa kuliko linavyofikirika!

Tanzania bila UKIMWI na ujambazi, HAIWEZEKANI!

Kuna jambo la kujifunza hapa zaidi ya ujambazi! majibu wa wawakilishi mbalimbali wa jamii ya watumiaji na wanufaikaji wa huduma ya guest house yanatisha. Hoja hii imeibua one of the cross cutting issues!

Nashauri wizara ya afya, tacaids, ofisi ya waziri mkuu majanga kufanya research zaidi juu ya hoja hii ya Kova, kwa mantiki ya kupunguza mbolea ya ukimwi na mmomonyoko wa maadili ktk jamii. Ni chungu tamu lakini ni muhimu, guest no choice kama tukitaka kuwa serious na ukimwi.

hivi kimaadili hao waume za watu ambao wanazitumia sana guest hizo unadhani what is going on behind their families? Lots of excuses! Lots of dont care or just ignoring their own realities!

Ukimwi, ujambazi, maadili bora kuyarejesha au kuyaweka sawa kwa Tanzania ya leo lazima uwe kama kichaa na dikteta kama Mugabe!

Sio kila kitu watu wote watakubali, hasa kama litakuja kwa mlengo wa uzinifu! Naamini tukilipigia kura hili, majority watasema ndio, weka kamera!
 
Mimi naona anatuzuga tu, mtakumbuka hata Makamba alipoteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa Dar es Salaam alianza na machangudoa, kisha wapiga debe nk halafu Mzee Kandoro naye akaanza na wamachinga, machangu na wapiga debe. Mzee Tibaigana alikuwa ni Mzee wa Level Seat akagomewa sasa tunaye Kova nMzee wa Ubunifu. Lakini nauliza "Mbona mashairi na beti nyingi ngoma yenyewe haipigwi tukaona inavyochezwa????
 
Ataanza gesti halafu atasema kwenye mashule na majumbani halafu atafika mpaka vyumbani, kuwa monitor mababa mabazazi wanaowabeza na kubaka wake zao.

Hivi tunajua hata gharama zinazohusika na CCTV na effectiveness yake? Wrong priorities, wrong approach, wrong PR, wrong ethics, pure Orwellian totalitarianism.
 
kwanza niulize nilisikia dar wanaweka kamera mitaani hasa katikati ya jiji,je hizo kamera zilishafunwa au ni maneno tu.
 
Hapa sioni tatizo kabisa for security reasons. Camera zinaweza wekwa lounge, front and back kwenye hoteli. Sababu ni kuwa hata kama wizi unaweza tokea kwenye kaunta basi wataonekana walioko pale, parking lot zitaonyesha wanaoingia na kutoka na kurahisisha upelelezi. Kuweka vyumbani au kwenye hallways inaingilia privacy za watu hapo!
 
SHUGHULIKIA MAFISADI KWANZA, na polisi waache kushirikiana na majambazi wizi utaisha nakila tukio la ujambazui likitokea polisi wafenye kweli, mabadiliki utayaona na suala la kufunga kamera amablo ni wazo zuri litaisha hivyo wenye gesti na hotel hawataingia gharama kubwa ya kufunga CCTV
 
Hapa sioni tatizo kabisa for security reasons. Camera zinaweza wekwa lounge, front and back kwenye hoteli. Sababu ni kuwa hata kama wizi unaweza tokea kwenye kaunta basi wataonekana walioko pale, parking lot zitaonyesha wanaoingia na kutoka na kurahisisha upelelezi. Kuweka vyumbani au kwenye hallways inaingilia privacy za watu hapo!

Mkuu,

Upo right kabisa na huu ndio utaratibu katika nchi zilizoendelea.

Ila inaendelea zaidi kwa kuhakikisha wanaoingia mahali hapo wanatoa taarifa zao zote kuhusu wapi wanaishi na namba zao za simu na za magari yao.

Mtu unakwenda kustarehe bana, kwanini uwe na wasiwasi?
 
Back
Top Bottom