Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,938
- 3,034
Kamera kuwekea gesti: Kova ajiwa juu...!
2008-06-30 16:20:23
Na Waandishi Wetu, Jijini
Wazo la Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, la kutaka hoteli na nyumba zote za kulala wageni almaarufu kama gesti zifungiwe kamera maalum za usalama limepokelewa tofauti na baadhi ya wadau ambao wengine wameliunga mkono huku baadhi wakimjia juu Kamanda huyo na kumtaka aache suala hilo.
Wakizungumza la Alasiri kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, baadhi ya wadau hao wamedai kuwa wazo la Kamanda Kova, likitekelezwa linaweza kuleta madhara makubwa, hasa kwa wale wanaofanya baishara ya gesti mitaani na pia wateja wao, wakiwemo madada wanaojiuza almaarufu kama machangudoa au \'ma-cd\' na vibosile wanaowachukua kila kukicha.
``Nimestushwa sana na pendekezo hilo la Kamanda Kova... ingawa moyo wake ni safi na dhamira yake ina lengo zuri la kutuhakikishia usalama, kamwe siungani naye kwa sababu likitekelezwa, sisi wenye gesti tutapata hasara kubwa,`` akasema mmiliki mmoja wa gesti maarufu iliyopo katika eneo la Sinza.
Akifafanua zaidi, mmiliki huyo akasema:``Baadhi ya wateja wetu wanafahamika kuwa si wageni kweli bali ni watu wenye wake zao.
Tena wengine wana heshima kubwa katika jamii.
Kwa sababu hiyo, hawatakuwa tayari kunaswa na hizo kamera, matokeo yake siye tutakufa njaa kwa kupoteza wateja wa namna hii ambao kwakweli ndio wengi zaidi kwenye majumba yetu haya ya wageni. Na Serikali pia itapoteza mapato yatokanayo na kodi tunazolipa,`` akasema mmiliki huyo.
Mfanyabiashara mwingine akasema wazo la Kova likitekelezwa, mbali na kutishia biashara yao kwa kukosa wateja na pengine watu waliowaajiri kupoteza kazi, pia itawagharimu pesa nyingi katika kuzifunga.
``Hizi kamera si rahisi... zinahitaji pesa nyingi ambazo kwa sisi wenye gesti za uswahilini zinaweza kutushinda. Ni bora tuendelee na mbinu hii ya kushirikiana na polisi kwa kuwapa taarifa za wateja wetu wanaoshukiwa kwa uhalifu badala ya ya kufunga kamera,`` akasema mmiliki mwingine wa gesti moja iliyopo katika eneo la Tandika Jijini.
Aidha, madada poa wanaoishi kwa kutegemea biashara chafu ya kujiuza miili yao almaarufu kama ma-cd, nao wamemuwakia Kamanda Kova na kumtaka asi1tekeleze wazo lake hilo kwa kile wanachodai kuwa linaweza kuwakimbiza mjini kwa njaa.
``Nikwambieni ndugu zangu... sisi wateja wetu wengi ni waume za watu na wengine ni wafanyabiashara maarufu. Pia wapo vigogo wenye heshima zao katika jamii. Haya mambo ya kufunga kamera gesti yatawakimbiza kwa sababu hawapendi kujulikana. Na sisi hatuna maeneo mengine ya kumalizana nao zaidi mahotelini na kwenye magesti. Aache (Kova), asije akatuua kwa njaa,`` akasema dada mmoja aliyejitambulisha kama Anti R, mkazi wa Manzese Uwanja wa Fisi.
Cd mwingine wa maeneo ya Kinondoni Jijini akamtaka Kova na Jeshi lake la Polisi washupalie majambazi kwa staili nyingine na si hiyo ya kufunga kamera kwenye gesti.
``Atuache kama tulivyo... hayo makamera yatatuharibia mambo yetu. Yeye ashirikiane vizuri na sisi ili tumpe data kwa sababu hata majambazi pia ni wateja wetu wazuri,`` akasema.
Aidha, baadhi ya vibosile wamedaiwa kutofurahia wazo hilo la Kova, kutokana na hofu yao ya kuumbuka pindi kamera zikifungwa katika gesti zote Jijini.
Hata hivyo, wakazi wengine waliozungumza na Alasiri wameunga mkono wazo la Kamanda Kova na kusema kuwa pindi kamera hizo zikifungwa, matukio ya uhalifu yanaweza kupungua kwa kiasi kikubwa Jijini.
``Sura zao zitaweza kufahamika na hili linamaanisha kuwa wahusika wataweza kudakwa kirahisi,`` amesema Mzee Shomvi, mkazi wa maeneo ya Ilala.
Kamanda Kova amekaririwa wakati akiwaambia wamiliki wa gesti na hoteli akisema kuwa njia mojawapo inayoweza kuwadhibiti majambazi na wahalifu wengine ni kufunga kamera kwenye nyumba za kulala wageni (gesti) na kwenye hoteli zote Jijini, kwani uzoefu unaonyesha kuwa wengi hukodi vyumba na kujificha kwenye majengo hayo kabla ya kufanya uhalifu.
Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Kamanda Kova amesema yeye alitoa ushauri tu kwa wenye nyumba hizo kwa ajili ya usalama wao na wala sio amri.
``Huo mimi nimetoa ushauri tu kwa wenye nyumba za kulala wageni kwa ajili ya usalama wao na raia wengine,`` akasema Kamanda Kova.
Aidha amesema kuwa amependekeza kamera hizo zifungwe sehemu za mapokezi tu na wala sio vyumbani, au sehemu nyingine ambako zinaweza kuingilia uhuru wa mtu.
``Kamera hizo hazifungwi chumbani, mimi nimependekeza zifungwe kwenye maeneo ya mapokezi ili kupata picha za watu wanaoingia na kutoka kwa ajili ya usalama wao tu,`` akasisitiza Kamanda Kova.
Aidha Kamanda Kova amesema tayari ameshafanya utafiti Jijini Dar es Salaam na kubaini kuwa zipo kamera nzuri na zenye bei poa zinazoweza kutumika sehemu hizo.
SOURCE: Alasiri