Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Baraka Andrew "Baraka Da Prince" amenaswa akimtomasa staa mwenzake, Estalina Sanga "Linah" kwa kumshika sehemu zake nyeti walipokuwa nyuma ya jukwaa(back stage) walipokuwa wakisubiri muda wao wa kutumbuiza ufike.
Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita katika Ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na shoo ya kuadhimisha miaka kumi ya staa wa Muziki wa Dansi, Christian Bella.
Baraka alionekana akiwa ameingiza mkono kwenye kifua cha Linah huku mrembo huyo akionekana kumpa ushirikiano.
"Mh! Huu ni udhalilishaji, hata kama wameamua kuwa na uhusiano, kwa nini haya mambo wasifanyie chumbani? Baraka anamdhalilisha tu Linah. Naye sijui kwa nini anakubali kuingizwa mkono vile," alisikika mmoja mwa watu waliokuwa karibu.
Linah alipoulizwa na baadhi ya watu waliotaka kujua kulikoni kutomaswa nyuma ya jukwaa alidai haoni tatizo kwani atakuwa amerejea kwenye himaya yake ya zamani.
"Naona ni bora kumrudia wa zamani ambaye nimemzoea," alijibu Linah na kuomba aachwe.
Kwa upande wake Baraka ambaye inafahamika ni mpenzi halali wa mtoto mzuri Naj, hakutaka kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kuishia kucheka tu.
Linah na Baraka waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kila mmoja kuchukua hamsini zake hadi waliponaswa wikiendi iliyopita ufukweni hapo.