Kambi ya Upinzani yatilia shaka Uteuzi wa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kambi ya Upinzani yatilia shaka Uteuzi wa JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by papag, Jul 14, 2012.

 1. papag

  papag JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 688
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  [TABLE]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]Amtuhumu kuteua ma-DC kwa fadhila

  na Salehe Mohamed, Dodoma
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]KAMBI ya upinzani bungeni imeeleza kutilia shaka uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete kwa nafasi mbalimbali zikiwemo za ukuu wa wilaya, ikidai kuwa wateule wengine ni kama wamelipwa fadhila za kisiasa.

  Akisoma maoni ya kambi hiyo kwa Wizara ya Katiba na Sheria, mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alisema uteuzi huo umekuwa ukichangia kudidimia kwa ufanisi wa kazi kwenye maeneo mbalimbali.

  Aliongeza kuwa wakuu wa mikoa na wilaya ni makada wa CCM na wanatekeleza majukumu yao kwa kulinda maslahi ya chama hicho tawala wakati Tanzania inafuata mfumo wa vyama vingi.

  Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Rais Kikwete alitumia mamlaka yake chini ya ibara ya 2(2) ya Katiba kugawa mikoa mipya ambayo wakuu wake ni makada wa CCM.

  "Wakuu wa wilaya wamekuwa ni wajumbe wa vikao vyote vikuu vya CCM katika ngazi ya Wilaya, Katiba ya CCM Toleo la 1982, Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya (ibara ya 42(3); ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya (ibara ya 44(3); na ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya (ibara ya 46(3)," alisema.

  Lissu alisema kuna ushahidi wa kutosha kwamba kugawa mikoa na wilaya ni namna tu ya kupata fursa ya kuwapatia makada wa CCM ambao kwa sababu mbalimbali wamekosa nyadhifa na marupurupu serikalini kwa kuwateua kuwa wakuu wa mikoa na wa wilaya.

  "Uteuzi wa wakuu wapya wa mikoa na wilaya uliofanywa katika siku za karibuni na Rais Kikwete, kati ya wateuele wake wakuu wa mikoa wapya, wawili ni wabunge wa Viti Maalum katika Bunge hili hili, kati ya wakuu wapya wa wilaya, watano ni wabunge wa Viti Maalum katika Bunge hili hili; 15 ni waliowahi kuwa wabunge au wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki na 22 waligombea ubunge lakini wakashindwa kwenye hatua za kura za maoni za ndani CCM au kwenye Uchaguzi Mkuu," alisema.

  Lissu aliongeza kuwa kuna utata mkubwa wa kikatiba kuhusiana na baadhi ya wateuliwa wa ukuu wa mikoa na wilaya ambapo orodha ya wakuu hao inaonyesha kuwapo kwa wanajeshi nane, ambao kati yao watatu wanatajwa kuwa maafisa wastaafu na waliobaki hawatajwi kama wastaafu na hiyo inaelekea bado wako katika utumishi wa jeshi.

  Aliongeza kuwa uteuzi wa baadhi ya wakuu wapya wa wilaya unaashiria kukithiri kwa rushwa na ufisadi na kukosekana kwa maadili kwa mamlaka ya uteuzi ambapo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Wilson Elisha Nkhambaku, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, aliteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea wake wa ubunge katika Jimbo la Singida Magharibi.

  Alisema mgombea huyo alirubuniwa na CCM na kuamua kujiengua CHADEMA muda mfupi baada ya kampeni za uchaguzi kuanza rasmi na alionekana katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa CCM katika Jimbo la Kibaha Vijijini na sasa kateuliwa kuwa mkuu wa wilaya.

  "Kifungu cha 48 cha Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 ya Sheria za Tanzania kinaruhusu mgombea ubunge yeyote aliyeteuliwa na Msimamizi wa Uchaguzi kujitoa katika kugombea uchaguzi husika.

  Hata hivyo, Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 91B cha Sheria hiyo kinatamka wazi kwamba ni kosa la jinai ya rushwa ya uchaguzi kumrubuni au kumshawishi mgombea kujitoa kugombea kwa malipo, au ahadi ya malipo. Kwa mujibu wa kifungu hicho, adhabu ya kosa hilo ni kifungo kisichozidi miaka mitano jela," alisema.

  Aliongeza kuwa kifungu cha 21(1)(b) cha Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010 kinakataza mtu yeyote, moja kwa moja au kwa namna nyingine yoyote, yeye mwenyewe, wakala wake au kupitia chama chake cha siasa, kwa niaba yake kutoa au kusaidia kutoa au kumpatia wadhifa au sehemu ya ajira mpiga kura au mtu mwingine yeyote kwa nia ya kumshawishi mpiga kura huyo kuacha kupiga kura au kumrubuni kutenda kitendo hicho.

  Lissu alisema kwa mujibu wa kifungu cha 94 cha Sheria ya Uchaguzi, makosa haya mawili ya jinai yana adhabu ya faini isiyopungua sh laki tano au kifungo cha kati ya mwaka mmoja hadi mitatu jela au vyote viwili kwa pamoja.

  Lissu alisema uteuzi wa Nkhambaku kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu ni ushahidi wa wazi wa rushwa ya uchaguzi na ni wazi kiongozi huyo alirubuniwa au kushawishiwa kujitoa kugombea ubunge kwa niaba ya CHADEMA.

  Alikwenda mbali zaidi akisema kuwa kambi yao imeshangazwa na kusikitishwa sana na uteuzi wa Kifu Gulamhussein Kifu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.

  Lissu alibainisha kuwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, Kifu alichaguliwa kuwa mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR-Mageuzi lakini matokeo ya uchaguzi wake yalipingwa katika Mahakama Kuu na Juni 18, 2002, Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika Shauri la Rufaa Na. 2 la 2002 katika Manju Salum Msambya dhidi ya Mwanasheria Mkuu na Kifu Gulamhussein Kifu, ilifuta matokeo ya uchaguzi.

  Alisema kuwa Kifu alienguliwa kwa sababu Mahakama ya Rufani ilithibitisha kwamba mtu huyo alifanya kampeni kwa misingi ya ukabila.

  Lissu alinukuu kauli hizo za ukabila zilizomtia hatiani kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi huo Kifu alisema: "... Waha wenzangu tuelewe kwamba mwaka huu ni mwaka wetu kujikomboa. Tumetawaliwa na kabila la Wabembe kwa muda mrefu. Kabila la Wabembe tunajua ni watu wa Kongo siyo wa Tanzania.

  Ni ajabu Waha tulio wengi katika jimbo hili tuendelee kutawaliwa na kabila chache. Muha popote alipo ahakikishe anipigie mimi Muha mwenzie. Angalieni wanakuja watu huku. Yuko mtu aliyepandikizwa na Msambya. Huyu mtu anakuja na Kabourou.... Kabourou na Msambya wote ni damu ya Kongo, wote ni Wanyakumawe," alisema Lissu.

  Katika mkutano mwingine wa kampeni, Mahakama ya Rufani ilithibitisha kwamba Kifu alitamka maneno yafuatayo: "Tumetawaliwa na wageni kwa muda mrefu ... umefika wakati wa kujikomboa kutoka kwa wageni kutoka Kongo.... Ni wakati mzuri kunichagua mimi kama Muha, Muha mwenzenu ... kwa kuwa sisi ndio tulio wengi katika jimbo hili,"

  Lissu alihoji kuwa mtu huyo aliyepatikana na hatia ya kufanya siasa za kibaguzi za aina hii ameteuliwaje kuwa mkuu wa wilaya.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 2. Asa'rile

  Asa'rile JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  “Tumetawaliwa na wageni kwa muda mrefu ... umefika wakati wa kujikomboa kutoka kwa wageni kutoka Kongo.... Ni wakati mzuri kunichagua mimi kama Muha, Muha mwenzenu ... kwa kuwa sisi ndio tulio wengi katika jimbo hili,”
  Code:
  
  
  ..Ah!.. PRESIDENT LISSU 2015!!
   
 3. T

  Tyegelo Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, kikwete ana mamlaka kikatiba kuteua wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya atakavyo, na inategemewa kuteua watu anaowafahamu.

  Lakini hivi kweli Kikwete amekosa watu anaowafahamu na wenye uwezo zaidi ya hawa ambao ni wabunge tayari, au wana kitu gani cha pekee ambacho wengine hawana?

  Kwa nini awateue watu ambao wananuka mnuko wa kuhongwa?

  Inatia aibu! Kuwahonga wabunge uDC na uRC ni kulidhoofisha bunge. Tukatae.
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kweli Tundu Lissu ameishiwa basi atuambie na kina Zitto kabwe kabila gani.

  Maana Tanzania huko mipakani kote watu wamechanganyika. Kusini tunaungana na wa Mozambique,Zambia, Malawi, Kaskazini wa Kenya , waganda, Kaskazini magharibi kuna Rwanda, Burundi kote huko watu wale wale.

  Kweli Tundu Lissu amefilisika.
   
 5. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Kweli dhaifu saaaana jambazi k,kwa mfumo huo we going in an open grave,shame on them bravo TL
   
 6. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wanataka vyeo...tu!! Hawana dila ya kuongoza..
   
 7. i

  iseesa JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanza tuambie wewe ni kabla gani ndipo tuanze kuchangia mjadala huu.
   
 8. d

  dguyana JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ZIka baba zika CCM.
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mimi sijinasibu kwa kabila langu, najifahamu kama mtanzania.

  wewe ndio utuambie
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Wewe kweli haujasoma... KIFU ni CCM ndio waliomuita MBAGUZi alikuwa NCCR; CCM wakaenda Mahakamani wakamtoa

  Ubunge, sasa wamesahau hayo sasa wanampa Ukuu wa WILAYA
   
 11. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Anachosema Lisu ni kwamba Mtu aliyetiwa hatiani kwa kueneza ukabila na mahakama kuu kwa kauli alizonukuu anateuliwa na Raisi kuwa mkuu wa wilaya. Huu ni udhaifu mkubwa wa mamlaka ya uteuzi.
   
 12. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ni hatari kubwa kuchangia kichwa kichwa kwa kumtukana Lissu bila kuisoma Hotuba yake vizuri.Si kila mada ni lazima mtu achangie maana vinginevyo utachangia mada kwa kujivua nguo kwa kila neno unaloleta hapa.
  Lissu aliwasilisha Hotuba iliyojaa utafiti wa kutosha na hapo alikuwa ananukuu maneno yaliyomtia KIFU hatiani.
  Wazungu walikuwa na makabila na kwa sasa yamekufa kifo cha asili ukabakia utaifa ambao kwa miaka kama 50 hadi 100 ijayo yaweza kuwa utaifa umemezwa na EUROPA.Kuulizana makabila pia ni utani au upotofu wa hatari
   
 13. M

  Mkojo Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe ndiyo maana JKilaza alisema bora Dr. Slaa awe rais kuliko Lissu kuingia mjengoni?? ha ha ha!Hii imekaa njema sana. aaaaaah! kibelaaaaa!!
   
 14. M

  Mkojo Member

  #14
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ukisoma unaelewa au unalewa??? huu ni upofu wa kujitakia huu! yani hata kama hujui kusoma kweli picha pia huielewi??
   
 15. Ndekirhepva

  Ndekirhepva JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  JK mwenyewe sio M Tizedi kwahiiyo hii hainipi shida sana kuelewa kwanini anawapa watu madaraka bila kufuata misingi na kanuni za maadili ya viongozi wa umma,..
  ifike mda sasa tuachwe kutawaliwa na wageni wa komoro, sasa nasisi tujitawale wenyewe kwani hawa jamaa hawana uchungu na nchi yetu, wao wanachuma tu na mwisho wa siku watarejea kwao...

  Jamani haya sio maneno yangu, nimenukuu waraka mmoja uliwahi kuwepo hapa jukwaani kuhusu uraiya wa mzee wa kaya
   
 16. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  maundumula,maundumula kwa nini unajidharaulisha namna hii,au ni kwa vile huna pa kwenda weekend hii unaona ujibu tu bila kusoma/
   
 17. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Jembe Lisu tunakukubali sana kwa hoja nzito dhidi ya dhaifu za magwanda!sijui kama watazijibu hoja hizo nzito na zilizopembuliwa kiyakinifu!!kweli Lisu nio jembe!wajibu basi tusikie sababu gani wanafanya hivyo?wabunge na ukuu wilaya,walioshindwa mahakamani wanapewa ukuu wilaya wakati rufani zao ziko wazi za ukabila!
   
 18. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi nashauri kama wakiingia bungeni wateule wa rais kanuni zibadilishwe wawe upande wa serikali ili wajibu hoja na si kuihoji serikali wakati ambapo na wao ni sehemu ya uozo wanaouhoji.
   
 19. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Mkuu pole sana kufanya kazi ya kumuelewesha mtu asiyetaka kuelewa
   
 20. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Hivi mkuu umesoma ukaelewa au baada ya kusoma ulilewa, hebu rudia halafu uje na constructive idea
   
Loading...