KAMBI rasmi ya Upinzani Bungeni imemtaka Spika wa Bunge Job Ndugai kutengua uamuzi wake wa kusitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma akiwa ameambatana na wabunge wa upinzani, Msemaji wa kambi hiyo, John Mnyika amesema kama Spika hatatengua uamuzi wake watatumia kila njia za kibunge ikiwemo Mbunge kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika.
“Kamati ya bunge ya uongozi haijawahi kukaa kikao chochote cha kusitisha kufanya kazi na CAG, huu uamuzi ni uamuzi binafsi wa spika ambao kambi hatuungi mkono na hatukubaliani nao,”amesema.
Ametoa wito kwa Spika kujitokeza kwa umma kueleza kuwa ni kikao gani alikaa na akina nani kufanya huo uamuzi huo.
“Uamuzi huo umeenda sambamba na kusambaratisha kamati za bunge za Hesabu za serikali(PAC) na Hesabu za serikali za mitaa(LAAC), Kamati za bunge hizo zimesitishwa kufanya kazi zake kuanzia 14-25 januari,mwaka huu na kwa mujibu wa ratiba ya bunge kamati zinamaliza kazi zake tarehe 25,”amesema.
Mnyika amesema Spika amesitisha kamati kufanya kazi zao za kikatiba kwa mujibu wa ratiba.
“Tunapinga hatua hii na tunapinga huu uamuzi, tunataka Spika abadilishe mara moja huu uamuzi na kamati zikutane na kufanya kazi ya kikatiba,”alisema.
Ameongeza “Spika anasema kwasababu CAG ameitwa tarehe 21 januari kwenye kamati kwa madai kuna mgogoro kati ya Bunge na CAG wakati hakuna kamati ya bunge iliyotangaza Bunge lina mgogoro na CAG na kauli hiyo ni binafsi si kauli ya bunge wala taasisi ya bunge,”
Chanzo: IPP