mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Nafuatilia mwenendo wa bunge la bajeti ya kwanza ya Serikali mpya ya Dr Magufuli, ambaye wapinzani wamempa majina kiasi cha ujazo wa kebehi na wakimwombea ateleze ili wapate pa kupandia kisiasa.
Nasikitika na kushangaa jinsi kambi ya upinzani inavyochangia hii bajeti ya kwanza ya mbaya wao.
Katika kuchangia, Mawazari Vivuli hotuba zao zimesheheni lawama za utendaji wa Serikali kuhusu bajeti iliyopita na masuala mengine. Hilo ni sahihi kabisa.
Au kwa kutokujitambua, au kutokujua nafasi yao kama Wabunge wa JMT, au umbumbu au makusudi, hawarejei nia yao ya upinzani kushika madaraka ya dola.
Je, wangia Ikulu, katika bunge lao la kwanza, agenda yao ingekuwa nini! Kuishambulia Serikali iliyopita kwa utendaji wake au kutetea bajeti yao, wakitumia mifano ya nyuma!
Kambi ya Upinzani Bungeni AMKENI. Mjadili kilicho mbele yenu (bajeti ya Serikali)kama inatekelezeka na ina manufaa kwa taifa letu, badala ya kungangania yaliyopita.
Yaliyopita si ndwele, lakini mwenye hekima, busara na mwelevu hutumia mazuri ya nyuma na kurekebisha mapungufu yake, kusonga mbele. Ndivyo BAJETI ya Serikali mpya imezingatia na kuaandaa hiyo bajeti.