Elections 2010 Kambi ya Upinzani Bungeni- 2010-2015

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
789
Wachambuzi wa Siasa:

Naomba msaada, nimetafuta kanuni za bunge toleo la mwisho nadhani ni la 2009 bila mafaniko, kuangalia kama CHADEMA inauwezo ya kuunda serikali kivuli yenyewe bila kuihusisha CUF? Yaani waunde kambi ya Upinzani bungeni kwa kuhusisha TLP, UMD tu?

Naomba mtuhabarishe wenye sheria na kanunu za Bunge... nakumbuka ili uweze kuunda hiyo kitu lazima uwe na robo ya Wabunge wote kama si-kosei...

Natanguliza shukrani.
 
Ili uwe na kambi ya upinzani bungeni ni lazima uwe na wabunge kutoka pande zote 2 za muungano yani tanganyika na zanzibar kwa hiyo cuf wanao uwezo wa kuunda kambi ya upinzani peke yao lkn chadema hawawezi mpaka waungane na cuf. Nionavyo mimi kuungana ni njia nzuri lkn unafiki na kutokuaminiana ndio tatizo letu.
 
kwanza hinategemea idadi ya wabunge,asilimia zaidi ya moja chama kilizopata.KWA MJIBU WA BBC mahojina na Mr Zitto Kabwe alisema kutokana na idadi ya kula alizopa Mweshimiwa Dr slaa wanategemea kuunda kambi ya upinzani na kupata viti maalumu sipungufu ya 30.
 
Ili uwe na kambi ya upinzani bungeni ni lazima uwe na wabunge kutoka pande zote 2 za muungano yani tanganyika na zanzibar kwa hiyo cuf wanao uwezo wa kuunda kambi ya upinzani peke yao lkn chadema hawawezi mpaka waungane na cuf. Nionavyo mimi kuungana ni njia nzuri lkn unafiki na kutokuaminiana ndio tatizo letu.
Hakuna kanuni ya aina hiyo labda ni kanuni ya bunge la Rwanda huwezi kulazimisha watu wa sehemu fulani wakuchague hiyo si demokrasia hata CCM haina hata karani wa bunge Pemba. Kinachotakiwa ni idadi ya asilimia 12 ya idadi ya wabunge PERIOD.
 
Nakuunga mkono. Katika Bunge lililopita CUF haikuwa na Mbunge hata moja kutoka Bara, lakini waliweza kuunda kambi ya upinzani -- lakini waliwashirikisha Chadema na UDP.
 
Wachambuzi wa Siasa:

Naomba msaada, nimetafuta kanuni za bunge toleo la mwisho nadhani ni la 2009 bila mafaniko, kuangalia kama CHADEMA inauwezo ya kuunda serikali kivuli yenyewe bila kuihusisha CUF? Yaani waunde kambi ya Upinzani bungeni kwa kuhusisha TLP, UMD tu?

Naomba mtuhabarishe wenye sheria na kanunu za Bunge... nakumbuka ili uweze kuunda hiyo kitu lazima uwe na robo ya Wabunge wote kama si-kosei...

Natanguliza shukrani.

Kasheshe nafikiri unachotaka kuhubiri na kuendeleza zile tofauti ambazo zapaswa kupigwa vita...!!!
Unachotaka kuendeleza ni Upinzani ndani ya Upinzani...!!! Nimeona post nyingi za wanachadema wakisema tuunde "Serikali kivuli bila ushirikiano na CUF"...kwali nyinyi mnataka kuja kujenga nchi?...What will happen ikiwa CUF wakitengeneza Serikali kivuli mkaachwa Chadema Nje?.....!!! Endeleza siasa zako za Kimajimbo !!!
 
waunde tu hiyo serikali yao kivuli ya chadema. lakini kiukweli chadema bado ni chama cha jamii fulani ya watanzania na bado sehemu zingine si zanzibar tu hata hapa bara hakikubaliki na ushahidi ni uchaguzi wa mwaka huu (the same tu CUF)
Njia pekee ya kuendeleza upinzani ni ushiriano na vyama vingine. beleive me.
Nakumbuka 2005 CUF walijifanya kuunda serikali peke yako (kwani walikuwa na wabunge zaidi ya 30 kama katiba inavyosema) Mzee cheyo akasema hii haiingii akilini hiki kichama (cha CUF) cha kikanda kuunda serikali kivuli peke yake. kwa maeneo mengine ya watanzania hakifahamiki na wala hakijui matatizo ya huko.
 
Ushirikiano na vyama makini vyenye lengo mahsusi la kuing'oa CCM madarakani unakubalika. Lakini ushirikiano na vyama vinavyoganga njaa na ambavyo havina mpango wowote wa kuiondoa CCM ni unafiki na usaliti kwa watanzania.

Asialani siishauri CHADEMA waungane na chama chochote cha upinzani kabla ya kuset MOU ya kuiondoa CCM.
 
Kuunda kambi ya upinzani na vyama vingine vya upinzani mi naona ni vyema ila Chadema lazima iweke prinspos na kukubaliana na ivyo vyama itakavyoshirikiana navyo waziheshimu izo prinspo lasivyo itakuwa mvurugano,nadhani mnakumbuka ishu ya Cheyo kambi inakubaliana kupinga budget ye anaenda kinyume wa2 kama hawa hawafai nadhani hata Mrema atakuwa sampuli hii.
 
Back
Top Bottom