Kambi ya Samuel Sitta na Mwakyembe yapata pigo kubwa!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kambi ya Samuel Sitta na Mwakyembe yapata pigo kubwa!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by samirnasri, Apr 2, 2012.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kambi ya wale wanaojiita wapambanaji dhidi ya ufisadi ndani ya chama tawala cha CCM imepata pigo kubwa kufuatia matokeo ya uchaguzi wa ubunge jimbo la arumeru mashariki na chaguzi za udiwani katika kata 8 tofauti. Kambi hiyo ilitoa wafuasi wake watatu kushiriki katika kampeni za chaguzi hizo mbalimbali. Samuel Sitta ambaye ndio kiongozi wa kambi hiyo alipiga kambi jijini mwanza na kuongoza kampeni katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Kirumba na kushindwa kuwashawishi vilivyo wakazi wa Kirumba ambao walimchagua mgombea wa CHADEMA kuwa diwani wao. Naye Anne Kilango alipiga kambi huko kiwila kuongoza kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Kiwira lakini naye aliangukia pua kwani mwisho wa siku mgombea wa CHADEMA aliibuka mshindi dhidi ya mgombea wa CCM. Kama hiyo haitoshi, Christopher Ole Sendeka alikuwa mmoja wa wana ccm walioshiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki lakini pia ushawishi wake na ule wa makada wengine wa ccm haukutosha kubadili mawazo ya wananchi wa Arumeru ambo bila ajizi wamemchagua Joshua Nassari wa CHADEMA kuwa mbunge wao. Matokeo hayo kwa ujumla ni pigo kubwa kwa kambi ya Samuel Sitta ambayo wakati Fulani ilionekana kuaminiwa na wananchi. Pigo limekuja wakati huu ambapo Samuel Sitta ameshaeleza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sasa wananchi wameonesha kwamba hawana imani hata na wana CCM wanaojipambanua kama wapinga ufisadi. Sasa nani aaminiwe ndani ya ccm!!!!!?????????/
   
 2. T

  THE QUANTS New Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mabadiliko ya kisiasa bado yanaendelea
   
 3. S

  Shembago JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna wakuaminiwa ndani uya CCM
   
 4. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania hawamwamini tena mtu yeyote ndani ya magamba kwani wamekuwa wanafiki wakubwa na kujali maslahi binafsi. M4C.
   
 5. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tuna imani na Ridhiwani Bilionea!!!
   
 6. r

  rwazi JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yule mzee muuaji wa mwalimu na mla panya yupo jamani,mbona kimya
   
 7. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Huko Arumeru alikuwepo Mkapa,Wassira,Lowasa,Nchemba jee hao wote ni kambi ya Sitta?naona una makengeza ya kisiasa weye sio bure
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  big up zittn regardless,mwanza na mbeya alimwaga kombati
   
 9. l

  luckman JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  NAOMBA NIKUNGATE SIKIO KITU KIMOJA BROTHER, USHINDI WA NASARI NI USHINDI WA MZEE 6, Kwa nini, sitta ndiye kiongozi wa kudi lililomkataa Sioi na kutaka uchaguzi urudiwe, wenyewe walimtaka Salakikya kwani alionekana kuwa na ushawishi wa kisiasa, lakini kutokana na pesa ya bwana mamvi alipitishwa tena ikiwa ni harakati za kuongeza ushawishi wake kisiasa on the way to 2015, ikumbukwe sitta na lowassa ni chui na paka, na sioi anamuoa Pamela Lowasa binti yake waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashifa! baada ya hapo ccm ilimeguka na bado kulikuwa na minyukano ya kufungua kampeni kwani mwanzo mkapa aligoma na baadae akakukubali na siamini kwamba ipo siku Mkapa atarudi jukwaani tena kwa yale yote aliyoyakuta! Chiligati, Nape, malecela, sitta, na wenzao walijitenga kabisa na kampeni za sioi, so kushindwa kwake bwana sioi na lowasaa wake ni ushindi wa sitta ni ushindi wa nape, ni ushindi wa chadema na ushindi wa central comittee nzima ya ccm!
   
 10. r

  rimoy Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM haiaminiki tena kwa wananchi, Tusubiri 2015 upinzani uchukue nchi
   
 11. Shukurani

  Shukurani JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unaposhindwa sababu kama hizi huwa hazikosekani. Hapa suala ni moja, kila mtanzania anajua ugumu wa maisha na ahadi hewa za ccm. Dawa hapa ni mabadiliko. Sitta ni mnafiki. Usitegemeee ccm kupata ushindi arusha, mwanza na mbeya. Huko songea wangoni wamekuwa ccm damu miaka nenda rudi lakini sasa mabadiliko yanakuja taratibu na ndiyo maana kuna madiwani wa cdm
   
 12. K

  Kasimpya Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Cha maana ni CCM kuacha kukumbatia mafisadi
   
 13. LUPITUKO

  LUPITUKO JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Kambi ya Sita na wenzake wapi na wapi ktk uchaguzi wa arumeru na udiwani? Mbona walikuwepo mpaka Lowasa huko? Fanyia uchunguzi wa kina kabla ya kuandika thread humu mkuu watu wengi wa humu ni vichwa hatutaki umbea au upendeleo na hatufungamani na chama chochote hapa ni kazi tu, ukifanya vizuri tunasifia ukiharibu tunabonda pia. Very possible hujui kambi ya Sita ni nini kwa sababu kwanza hakuna kambi rasmi ya aina hio kilichopo ni watu waliwagroup hawa wabunge na mawaziri kutokana na hoja zao za kutetea maslahi ya Taifa pengine hata wao kwa wao hawapendani zaidi ya Sita na Mwakyembe. Mbona Magufuli ni mpambanaji wa kusimamia sheria kwani huko c kupinga ufisadi? Ufisadi ni kuvunja sheria pia lakini hatajwi kwenye kundi hilo kbs though yupo against na kila uozo serikalini.
   
 14. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kumbe Lowassa Arusha ni joka la kibisa halipandi mtungi wala halishuki mferejeni!
   
 15. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,071
  Likes Received: 7,282
  Trophy Points: 280
  a.k.a kipipa
   
 16. n

  nketi JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakika mtu hawezi kuwa mpiganaji ndani ya ccm . Akiwa hivto basi
   
 17. a

  arinaswi Senior Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nakubaliana na wewe nketi. ndani ya sisiemu haiwezekani kukawa na mtu 'msafi'. labda magufuli tu. wengine wanajenga kambi but wamo humo humo tu, watoke basi kama kweli wamechoshwa na ufisadi
   
 18. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  details kwa faida ya nani? CCM imefail Arumeru, nukta.
   
 19. M

  Miruko Senior Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna kambi iliyopoteza kama ya Lowassa.

  Mosi, Amemsimamisha mkwewe. Ameshindwa.
  Pili, Amesimama mwenyewe jukwaani kumtetea, ameshindwa.
  Tatu, Amemtumia Sendeka, Nape ili kumpa nguvu, ameshindwa.
  Nne, Ametumia gazeti la rafiki yake Rostam, Rai, kufanya utafiti feki kushawishi wapiga kura, ameshindwa.
  Tano, Ametumia mabilioni, kwenye kura za maoni mara mbili, amenoa.
  Kwa hiyo basi, kama ni kambi kupoteza, kambi zote mbili zimenoa. Wewe hilo hulioni? au mvi za mzee zimekufunika macho?
   
 20. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Kuna kauli aliitoa Mwakyembe siku moja bungeni kuwa kuna watu wameendeleza minong'ono na maneno juu ya tume yao ilipochunguza sakata la Richmond kisha akamalizia kwa kusema kuwa anawaaomba waache maana wakiendelea wao yaani kina mwakyembe watasema na yale waliyokuwa wameyamezea. Hii kitu ilinitoa kwenye mood kabisa na tangu hapo nikagundua kuwa hawa ni ndege wa aina moja tofauti ni rangi tu! They are all contaminated, usiwaamini kabisa hawa ni kama walizidiana tu kwenye madeal maana ukimchunguza kila mmoja nyuma yake anakajiskendal. Ili kuuau mfumo huu inabidi kuwang'oa wooote kabisa na kutupa kuleeeee!
   
Loading...