Kambi ya Lowassa kazini: Askofu Laizer aunga mkono Lema kuondolewa Arusha!

Si vyema kumkebehi askofu kwa kuwa ana miono kutoka mbinguni, heshimuni viongozi wa dini tusije pata matatizo katika taifa letu.

Kwahiyo unataka tumheshimu kwa kuwa yeye ni kiongozi wa dini? Angekuwa anazingatia kazi aliyotumwa na Mungu wala asingekubali kutumika kisiasa. Shame upon him!
 
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati,
Thomas Laizer, ameunga mkono hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ya kumpokonya
ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) na kusema ni haki na ukweli mtupu.

Alisema hayo jana katika Ibada ya Umoja wa Madhehebu ya Kikristo, iliyofanyika kwenye
uwanja wa Shekhe Amri Abeid, huku kauli yake hiyo ikipokewa kwa miguno na minong’ono kutoka kwa waumini.

Akihutubia halaiki hiyo muda mfupi baada ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu, kuonya vyombo vya Dola na Mahakama nchini, kuacha kupoka haki za watu na kunyanyasa wananchi kwa kuwapiga, Laizer alisema anaunga mkono hukumu hiyo.

“Mimi sijawahi kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Lema, lakini niliwahi kusikia kuwa Lema alisema katika mikutano yake, kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi wa Malaigwanani, kama alisema hivyo kweli na anastahili hukumu,” alisema Askofu Laizer.

Kauli hiyo ilionesha kuchukiza waumini waliofurika katika ibada hiyo na kuguna na kutokea minong’ono mingi, kuashiria kutokubaliana naye.

“Hata kama ninayosema hamuyakubali, lakini huo ndio ukweli mtupu na anastahili hukumu, nafahamu wengi hamfurahii uamuzi wa Mahakama, lakini imetoa haki, hakuna kutupa lawama kwa Kikwete (Jakaya) wala Ridhiwani Kikwete,” alisisitiza Askofu Laizer, huku watu wakiguna.

Kauli ya Askofu Laizer ilikuja siku moja baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kumvua ubunge Lema ambaye Mahakama ilimkuta na hatia nane zikiwamo za matusi, kashfa na kejeli katika mikutano ya kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka juzi.

Askofu Lebulu, alisema hata wakati Yesu alipigwa makofi, wakati akisulubiwa na alipouliza sababu za kupigwa kwake, aliendelea kupigwa, hivyo hali hiyo inazidi kukithiri nchini kwa watu kupokwa haki zao za msingi.

“Ngoja ninukuu maneno ya Biblia, kuna sehemu inasema Yesu alipigwa makofi, akauliza sababu za kupigwa kwake, hapa nafananisha na leo watu wanapigwa makofi na mahakama zetu, Serikali na vyama vyao, jambo ambalo linapaswa kukemewa lisiendelee,” alisema.

Alimwomba Mungu kumsaidia ili asiropoke, kwa sababu katika miaka 35 ya utumishi wake, hajawahi kuropoka.

Alipomaliza hotuba hiyo kama Msemaji Mkuu wa Umoja huo, alishangiliwa na watu, huku wakipiga vigelegele na baadhi yao wakirukaruka kuashiria kuunga mkono hotuba yake.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi, alipokaribishwa kusalimia waumini, alisema lazima watu wafike mahali wajue, haki inastahili kutolewa kwa watu kuheshimu haki na kufahamu wajibu wako.

Alisema ni wajibu wa kila mtu kupata haki, ila haki hiyo itapatikana tu kwa mtu kuheshimu wajibu wake serikalini na katika familia, kisha unaweza kudai haki kwa wengine.

My take: Nimeingiwa na Mashaka na Askofu wangu Thomas Laizer, kiasi kwamba naweza kusema amenunuliwa na Lowassa, ukizingatia anatokea Monduli kwa Lowassa.

Batila Burian aliwahi kuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa KKKT Dayosisi hii ya Askofu Lekule Laizer kama sikosei! Maaskofu nao ni binadamu wenye mapungufu kama tulivyo wengi wetu. Ukichukulia mfumo wa Kanisa letu la Lutherani wa namna maaskofu wanavyopatikana usishangae na wao wanavyotumika.
Ila kama anataka kuendelea kuongoza kanisa lenye umoja inafaa aige mfano wa mwenzie wa RC aliyesema hapendi kuropoka
 
Achana naye huyo askofu kwani yeye ni mungu asubiri atachomwa moto na mungu siku ikifika

Kuna kitu nimeng'amua kutoka kwa huyu askofu wangu. Mi nadhani ni Kada wa CCM ndiyo maana amejibu kwa kujiamini.
Anasema hakuwahi kuhudhuria kampeni za Lema, ila alikuwa akisikia kuwa kamadhalilisha mwanamke. Kumbe kasikia tu na hana ushahidi.
Askofu wangu Laizer anajishushia heshima mbele ya jamii yake.
 
"Hata kama ninayosema hamuyakubali, lakini huo ndio ukweli mtupu na anastahili hukumu, nafahamu wengi hamfurahii uamuzi wa Mahakama, lakini imetoa haki, hakuna kutupa lawama kwa Kikwete (Jakaya) wala Ridhiwani Kikwete," alisisitiza Askofu Laizer, huku watu wakiguna.
Kama hayo maneno kayasema kweli basi huko tunakoelekea hakuna matumaini...tulikuwa tunawacheka mashehe ubwabwa bure...!
 
Mkuu mimi mwenyewe Mlutheri lakini katika hili Askofu ameniumiza sana. nimeanza kupata mashaka na mahubiri yake kabisa.
Naanza kutafuta mahali kuna malisho.
 
duh hapo inakuwa ngumu maana huyu ni mtumishi wa mungu tena mwenye ngazi ya uaskofu iweje anaongea maneno ya kuiskia kwenye public? kama ilivyosemeka kuna watumishi kule arumeru walihongwa basi ni wa aina hii!
 
Kule uwanjani alijiandaa kwa ajili ya hukumu ya Lema siyo kitu kingine!
Kada wa CCM
 
duh hapo inakuwa ngumu maana huyu ni mtumishi wa mungu tena mwenye ngazi ya uaskofu iweje anaongea maneno ya kuiskia kwenye public? kama ilivyosemeka kuna watumishi kule arumeru walihongwa basi ni wa aina hii!

Amejidhihirisha ni mwanasiasa siyo mtumishi. Mungu ametuonyesha yupo Kambi ya Lowassa
 
Mimi sishangai kwani kuni baadhi ya maaskofu ni magamba kama yule aliyesema JK ni chaguo la Mungu halafu mkuu wake akamkana na kwa kumpa azabu akapelekwa mgombani akajifunze kufikili kabla ya kuropoka. Ila hawa kazi ni ndogo tuyang'oa magamba haya kuanzia huko huko kanisani.
 
Askofu yupo right, wanasiasa sio watu wazuri na ukiwachekea wanaweza kukuvua nguo. Ni wajibu wa viongozi wa dini kukemea mambo maovu!
 
Kama maaskofu nao wanaungana na wanaodhulumu haki ya watu, basi hakuna haja ya kwenda kanisani kuwasikiliza maaskofu wanafiki
 
Askofu yupo right, wanasiasa sio watu wazuri na ukiwachekea wanaweza kukuvua nguo. Ni wajibu wa viongozi wa dini kukemea mambo maovu!

Mkuu Tume,

Tunachosema ni kwamba Mahakama yenyewe ilishindwa kuthibisha kwa vielelezo kama kweli Lema aliyatamka hayo maneno.
Pia katika utetezi wake Lema alijitetea akisema maneno ya udhalilishwaji yaliyotamkwa dhidi yake siyo kweli, kwani hata katika chama chake kulikuwa na wagombea wanawake ambao yeye mwenyewe aliwaombea kura kwa wananchi.

Sasa Askofu Laizer alipata wapi uthibitisho kama kweli aliyatamka hayo maneno
 
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati,
Thomas Laizer, ameunga mkono hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ya kumpokonya
ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) na kusema ni haki na ukweli mtupu.

Alisema hayo jana katika Ibada ya Umoja wa Madhehebu ya Kikristo, iliyofanyika kwenye
uwanja wa Shekhe Amri Abeid, huku kauli yake hiyo ikipokewa kwa miguno na minong’ono kutoka kwa waumini.

Akihutubia halaiki hiyo muda mfupi baada ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu, kuonya vyombo vya Dola na Mahakama nchini, kuacha kupoka haki za watu na kunyanyasa wananchi kwa kuwapiga, Laizer alisema anaunga mkono hukumu hiyo.

“Mimi sijawahi kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Lema, lakini niliwahi kusikia kuwa Lema alisema katika mikutano yake, kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi wa Malaigwanani, kama alisema hivyo kweli na anastahili hukumu,” alisema Askofu Laizer.

Kauli hiyo ilionesha kuchukiza waumini waliofurika katika ibada hiyo na kuguna na kutokea minong’ono mingi, kuashiria kutokubaliana naye.

“Hata kama ninayosema hamuyakubali, lakini huo ndio ukweli mtupu na anastahili hukumu, nafahamu wengi hamfurahii uamuzi wa Mahakama, lakini imetoa haki, hakuna kutupa lawama kwa Kikwete (Jakaya) wala Ridhiwani Kikwete,” alisisitiza Askofu Laizer, huku watu wakiguna.

Kauli ya Askofu Laizer ilikuja siku moja baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kumvua ubunge Lema ambaye Mahakama ilimkuta na hatia nane zikiwamo za matusi, kashfa na kejeli katika mikutano ya kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka juzi.

Askofu Lebulu, alisema hata wakati Yesu alipigwa makofi, wakati akisulubiwa na alipouliza sababu za kupigwa kwake, aliendelea kupigwa, hivyo hali hiyo inazidi kukithiri nchini kwa watu kupokwa haki zao za msingi.

“Ngoja ninukuu maneno ya Biblia, kuna sehemu inasema Yesu alipigwa makofi, akauliza sababu za kupigwa kwake, hapa nafananisha na leo watu wanapigwa makofi na mahakama zetu, Serikali na vyama vyao, jambo ambalo linapaswa kukemewa lisiendelee,” alisema.

Alimwomba Mungu kumsaidia ili asiropoke, kwa sababu katika miaka 35 ya utumishi wake, hajawahi kuropoka.

Alipomaliza hotuba hiyo kama Msemaji Mkuu wa Umoja huo, alishangiliwa na watu, huku wakipiga vigelegele na baadhi yao wakirukaruka kuashiria kuunga mkono hotuba yake.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi, alipokaribishwa kusalimia waumini, alisema lazima watu wafike mahali wajue, haki inastahili kutolewa kwa watu kuheshimu haki na kufahamu wajibu wako.

Alisema ni wajibu wa kila mtu kupata haki, ila haki hiyo itapatikana tu kwa mtu kuheshimu wajibu wake serikalini na katika familia, kisha unaweza kudai haki kwa wengine.

HabariLeo | Askofu aikubali hukumu ya Lema
:embarassed2:
 
Mkuu Kiby Askofu laizer hajajikanganya, aliyetoa mfano wa wa Yesu kupigwa ni huyo Askofu msomi Lebulu, na kama umemsoma vizuri Lebulu ameonyesha ni Askofu kwa kutoa genaral overview ambayo mwenye akili atakuwa kamwelewa vizuri kamaanisha nini, Kuwa askofu katoliki si lelemama wanakwenda shule ya ukweli achana na huo laizer hana lolote ni mjasiriamali huyo

ni kweli mkuu kumbuka hata kwenye kikombe cha babu RC walipinga mwanzo mwisho lakini KKKT waliunga mkono na huyo askofu alipiga kikombe cha babu. Na kwa lowasa wakati RC wanampinga kwa fedha zake za kifisadi KKKT wanamkumbatia na kumtetea....askofu kwani lazima umtetee lowassa mbona kkkt kuna wasomi wengi tu.
 
huyo Mzee yeye asubiri zamu yake. Anaendesha dayosisi kama taasisi yake binafsi na ukabila mwingi tuu. Hat vuguvugu la kutoa mafisadi lilipo anza huyo mzee alimsaport sana EL, yeye kila kitu ni ukabila tuu. Na lazima tumtoe uaskofu wake
 
Back
Top Bottom