Al assad
JF-Expert Member
- Aug 14, 2017
- 1,400
- 1,501
Nakunaliana na wewe kwa hoja zako lakini bado kuna maswali ya kujiuliza..Marekani anafanya nini mashariki ya kati? Marekani alikuja kufanya nini Libya? Marekani alienda kufanya nini Congo wakati wa Patrice Lumumba? Ukijiuliza hayo maswali ndio utajua kwa nini watu wanashabikia apigwe, middle east japo kulikuwa na viongozi kama Saddam au Libya kwa Muaamar ambao marekani inadai kuwa ni Magaidi au dictators lakini beleive it or not, USA imesababisha vifo vya ma milioni ya watu ikiwemo Afrika na Mashariki ya kati, kuingilia mambo ya watu na chokochoko zake kumepelekea civil war, ni bora Saddam angebaki middle east na Muammar angebaki, Obama alishakiri kumuua Muammar Libya ilikuwa ni mistake.
Ni bora Iraq ya Saddam kuliko Iraq ya sasa.
Ni bora Libya ya Muammar kuliko ya sasa.
Tazama Syria ilivyokuwa.
Wanakuja kwako kwa kuonyesha ulimwengu wanakwenda kusahihisha jambo fulani, wanakupiga, wanachukua mali zako, wanaacha raia wanauana ovyo, wanaondoka kibabe na ulimwengu unatazama.
Acha Iran ijitetee, acha USA apate wababe wenzie, binadamu wote ni sawa, itakuwa safi sana siku 1 apigwe hata kombora 100 hapo washington ili waone uchungu wake.
*je ni kweli kila alipo Marekani kuna vurugu?
*je ni kweli kila alipo Marekani watu ni masikini? (Kama unavyosema)
*Je ni kweli kila alipo Marekani kuna Vita?
*Je Libya imeharibiwa na Marekani pekee,hakuna Mataifa mengine?
Au huoni pia Vacuum ya power na kuwepo kwa makabila mengi yenye tamaa na madaraka pia kunachangia(walibanwa kipindi cha Gaddafi.
*kusema nini Marekani anafanya Mashariki ya kati ni swali la kitoto maana hujui siasa za kimataifa! ..kwani hapo Middle East yupo Marekani pekee...Yupo Russia Syria ila husemi...yupo Russia Venezuela husemi..hayo ni mambo ya sasa za kimataifa na interest.. Hii haijalishi taifa lipo wapi..baadhi ya migogoro ya middle East inatokana na sasa za nchi husika ..ndio maana hata hapo middle East kuna nchi hazina machafuko tena ni nyingine tu mfano Jordan,Kuwait, UAE,Saudi Arabia,Qatar,Bahrain nk.
Nakushauri pitia tena hoja kwa umakini usiangalie upande mmoja wa shilingi geuza na wa pili!
Sent using Jamii Forums mobile app