ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,418
- 9,599
- Thread starter
- #81
Watu wapo mpaka Bungeni na wana wawakilishi wao unasema hawahusiani na serikali ya Lebanon?!Mkuu kuna tofauti ya institution and political millitant group.
Kuna tofauti na taasisi na kundi la wanamgambo la kisiasa.
Hizbollah wanajihusisha na siasa za pale Lebanon km ilivyo Houth tu lakini wale wanafadhiliwa na Iran.
Pesa unazoziona zinawaletea jeuri Hizbollah na silaha zinazowaletea jeuri Hizbollah ni za Iran.
Hizbollah haisimamiwi na serikali ya Lebanon bali inajihusisha na harakati za serikali ya Lebanon.
Kufadhiliwa na Iran wala haina shida maana hata vyama vyetu hapa nchini vinasaidiwa na nchi rafiki mfano Chadema inapewaga misaada na German na Ccm na CCP. Je huo msaada unatumika inavyotakiwa,lakini Hezbollah wanatumia misaada kutengeneza silaha!!
Na sasa baada ya vikwazo vya US kurudishwa ufadhili wa Iran kwa makundi yake umepungua kwa kiasi kikubwa,yeye mwenyewe tu hana fedha,shilingi yake imeshuka thamani kwa zaidi ya 60%, uchumi unaangamia.
Iran ilitumia mamilioni ya Dola kujenga mahandaki ambayo yangetumika na Hezbollah kuingia Israel wakati wa vita kumbe Israel kipindi chote walikua wanawaangalia tu wakisubiria yakamilike ili wayabomoe,na kweli mahandaki yamekamilika kabla hata hawajayatumia wayahudi wakayabomoa yote. Na hakuna kitu ilichothubutu kuwafanya Israel.