Kambi ya Iran yashambuliwa,18 wafariki

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,418
9,599
Kambi ya jeshi inayosadikika kua ya Iran iliyo mpakani mwa Syria na Iraq imeshambuliwa kwa makombora na kuua zaidi ya watu 18 wakiwemo wairani pamoja na wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran. Milipuko mikubwa ilisikika wakati shambulizi hilo likitekelezwa.

Mpaka sasa haijajulikana ni nani amehusika na shambulio hilo,lakini Israel imenyooshewa kidole. Taarifa zinasema kwamba Ndege zisizotambulika zilishambulia kambi hiyo,maghala ya silaha,magari pamoja na sehemu nyingine. Mpaka sasa Israel haijaongea chochote kuhusiana na shambulio hilo.

Taarifa nyingine zinadai kwamba Israel imetumia Ndege zake za F-35 ambazo ni ngumu kuonekana kwenye rada kushambulia kambi hiyo. Wengine wanadai Ndege zisizo na rubani zilitumika kutekeleza shambulio hilo.

Inaelezwa kwamba mahali palipotokea shambulio hilo ni sawa na eneo ambalo chombo Cha habari cha Fox news kilitangaza kwamba Iran imekua ikijenga kambi kubwa ya kijeshi (nchini Syria) ambayo itatumika kuweka mamia ya wanajeshi,silaha pamoja na zana zingine za kivita.

Hivi karibuni mgogoro wa Israel na majirani zake umeongezeka baada ya wiki iliyopita Israel kushambulia nchi nne (Syria,Iraq,Lebanon,Palestine) ndani ya siku mbili ikidai kwamba inatekeza kile ilichokiita uchokozi wa Iran.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliweka wazi kwamba Iran haina kinga mahali popote mashariki ya kati na kwamba itaishambulia miundombinu yake popote,Iran na washirika wake Hezbollah wameionya Israel kuhusiana na mashambulizi hayo.

https://www.google.com/amp/s/www.bbc.com/news/amp/world-middle-east-49633146
 
iran3.png

AP_19237671684567-e1567170313173-640x400.jpg

AP19227601586230-640x400.jpg
 
Ila Israel naye anazingua anatakiwa apeleke kichapo hadi Iran aingie vitani
Hapa ss walau umeongea chamaana japo Myahudi Hana Huu Uwezo Unahisi aanfika Mpaka Iraq Mpakani Na Iran Why Sasa Asishambulie Pale IRAN

Jamaa Anaelewa Sana kama Kimaliza Kushambulia Pale 2 Na akijulikana kama ni yeye basi ndio tuta andika historia mpya pale Western Asia(Mashariki Yakti)
 
Western Asia ndio Mashariki ya kati ?
 
mtabaki hivohivo,mwenzenu anawamaliza,kila siku ni maneno tu,kama wanauwezo si waifute mara moja,nchi yenyewe ni ndogo tu,,,,israel ni dunia nyingine...
Hapa ss walau umeongea chamaana japo Myahudi Hana Huu Uwezo Unahisi aanfika Mpaka Iraq Mpakani Na Iran Why Sasa Asishambulie Pale IRAN

Jamaa Anaelewa Sana kama Kimaliza Kushambulia Pale 2 Na akijulikana kama ni yeye basi ndio tuta andika historia mpya pale Western Asia(Mashariki Yakti)
 
Ila Israel naye anazingua anatakiwa apeleke kichapo hadi Iran aingie vitani
[/QUOT
Wanajua ni kipi kitakacho watokea iwapo watafanya hivyo kwa hiyo wao siyo wajinga kiasi hicho.
Ila Israel naye anazingua anatakiwa apeleke kichapo hadi Iran aingie vitani
Wana jua vizuri ni kipi kitakacho watokea iwapo watathubutu kufanya hivyo kwa hiyo wa sio wapumbavu kiasi hicho.
 
mtabaki hivohivo,mwenzenu anawamaliza,kila siku ni maneno tu,kama wanauwezo si waifute mara moja,nchi yenyewe ni ndogo tu,,,,israel ni dunia nyingine...
Dunia ipi hii inayopelekeshwa na israel wao si walisema miradi ya nyuklia ya iran itasmamishwa kwa gharama zozote zile hata kijeshi

Ss mbna wanaume wanapiga kazi 2

Iran ipo iran kijana haipo syria wala Iraq
 
Wayahudi Waache Ushamba Na Upuuzi

Wakitaka IRAN Asifanye Anayo Yafanya Kujenga Hizo Kamb hko anapojenga

Inakiwa Apasue pale Pale IRAN Kupiga Nje Ya Iran Nimatumizi mabaya yarasilimali Za WAYAHUDI Pia
Kama nawe unaona adui yenu anaingilia na kufanya uharibifu kwa ndugu yako si uingilie kumtetea? Iran naye kwa nini nduguye anapigwa na Wazayuni halafu anakaa kimya? Si aingilie?

Vv
 
nyie mnaosema Israeli ashambulie Irani kwanini isiwe kinyume chake kama kweli Irani anajiamini basi aanze yeye kushambuliwa lakini kama akili yake inamtuma kwamba ajage ashambulie kwa kutumia base atakazozijenga iraq au syria basi kila siku atakuwa anachapwa tu
 
Back
Top Bottom