ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,418
- 9,599
Kambi ya jeshi inayosadikika kua ya Iran iliyo mpakani mwa Syria na Iraq imeshambuliwa kwa makombora na kuua zaidi ya watu 18 wakiwemo wairani pamoja na wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran. Milipuko mikubwa ilisikika wakati shambulizi hilo likitekelezwa.
Mpaka sasa haijajulikana ni nani amehusika na shambulio hilo,lakini Israel imenyooshewa kidole. Taarifa zinasema kwamba Ndege zisizotambulika zilishambulia kambi hiyo,maghala ya silaha,magari pamoja na sehemu nyingine. Mpaka sasa Israel haijaongea chochote kuhusiana na shambulio hilo.
Taarifa nyingine zinadai kwamba Israel imetumia Ndege zake za F-35 ambazo ni ngumu kuonekana kwenye rada kushambulia kambi hiyo. Wengine wanadai Ndege zisizo na rubani zilitumika kutekeleza shambulio hilo.
Inaelezwa kwamba mahali palipotokea shambulio hilo ni sawa na eneo ambalo chombo Cha habari cha Fox news kilitangaza kwamba Iran imekua ikijenga kambi kubwa ya kijeshi (nchini Syria) ambayo itatumika kuweka mamia ya wanajeshi,silaha pamoja na zana zingine za kivita.
Hivi karibuni mgogoro wa Israel na majirani zake umeongezeka baada ya wiki iliyopita Israel kushambulia nchi nne (Syria,Iraq,Lebanon,Palestine) ndani ya siku mbili ikidai kwamba inatekeza kile ilichokiita uchokozi wa Iran.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliweka wazi kwamba Iran haina kinga mahali popote mashariki ya kati na kwamba itaishambulia miundombinu yake popote,Iran na washirika wake Hezbollah wameionya Israel kuhusiana na mashambulizi hayo.
https://www.google.com/amp/s/www.bbc.com/news/amp/world-middle-east-49633146