Kambi ya CUF bungeni, yamuomba Jaji Mkuu kumaliza Mashauri mapema

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
MAELEZO YA WABUNGE WA CUF MBELE YA WAANDISHI WA HABARI YALIYOSOMWA NA MHE.ALLY SALEH (MBUNGE WA JIMBO LA MALINDI, MNADHIMU WA KAMBI YA CUF BUNGENI, LEO TAREHE 26 FEBRUARY, 2019 KATIKA UKUMBI WA OFISI YA WABUNGE WA CUF, MAGOMENI-DAR ES SALAAM:
IMG_20190226_110956_9.jpg

Ndugu Wanahabari,

Assalaam Aleykum.

Tokea kulipozuka mgogoro wa kupandikizwa ndani ya Chama chetu mwaka 2016, Wanachama na Wapenzi wa CUF wametiwa katika mtihani mkubwa wakiwa na wasiwasi juu ya hatma ya Chama ambacho wamekijenga kwa damu na jasho kwa pande zote mbili Zanzibar na Tanzania Bara.Kwa nia ya kuheshimu utawala wa sheria, kutetea na kukilinda Chama chetu, na kama Katiba ya CUF inavyoeleza, tumefungua kesimbalimbali Mahakama Kuu kwa madhumuni ya kupata ufumbuzi wa haki na tafsiri ya kisheria juu ya mkanganyiko uliopandikizwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kumtumia Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Nyinyi mtakuwa mashuhuda kuwa mwaka 2015 CUF ilikuwa inaelekea kufika kilele cha siasa za Tanzania ambapo tulifanya vyema kuliko wakati wote mwingine pamoja na Chama chetu kutiwa katika msukosuko na aliyekuwa Mwenyekiti na Mwanachama wetu Professa Ibrahim Haruna Lipumba kuchupa jahazi tukiwa katikati ya bahari.Prpfesa Lipumba alijiuzulu hadharani na nyote mlishuhudia kujiuzulu kwake tarehe 6/8/2015 pale Peacock Hotel –Dar es Salaam.Mwaka 2015 katika Uchaguzi Mkuu CUF,kwa kushirikiana na Vyama Rafiki katika UKAWA ilifanikiwa kushinda Majimbo 10 ya Uchaguzi kwa upande wa Tanzania Bara.

Kwa upande wa Unguja tulishinda viti 4 vya Ubunge lakini hatua kubwa tukapiga kwenye Baraza la Wawakilishi ambapokwa ujumla tulipata viti 27 sawa na CCM.Pia tulishinda viti vyote 18 vya Ubunge na Uwakilishi kisiwani Pemba na viti 9 vya Uwakilishi Kisiwani Unguja.

Kwa upande wa Urais ushindi wetu haukuwa na shaka ambapo Maalim Seif alimshinda Dk. Ali Muhammed Shein kwa tofuati ya kura 25,836 na yaliyotokea, ya kuporwa kwa ushindi wa CUF na Maalim Seif kwa njama na hila za Jecha Salum Jecha, nyote mnayajua. Aidha ushiriki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, hasa kitendo cha kumteka Jaji Abdulhakim Ameir Issa, kilifanywa dhahiri ili kumzuia asitangaze matokeo ya majimbo yaliyokuwa yamebaki na kuitaja CUF mshindi kwa mujibu wa sheria.

CUF ina madiwani zaidi ya 300 nchini na inaongoza Halmashauri 5 (Newala, Tandahimba, Mtwara, Kilwa na Liwale) na kuporwa kuongoza Manispaa ya Jiji la Tanga. Mkoani Dar-es-Salaam CUF, kwakushirikiana na Vyama Washirika katika UKAWA, ina Manaibu Meya katika Halmashauri ya Ubunge na ya Jiji na pia sehemu nyingine nchini.

Kwa matokeo hayo ni dhahiri tumepiga hatua kubwa ya mafanikio ya ushindani wa kisiasa nchini.

Ndugu Waandishi;

Madhara na athari ya mgogoro huu uliopandikizwa ni kubwa sana kwetu kama Wawakilishi wa Wananchi na kwa Chama kwa ujumla. Nikitaja machache;

1. Kupoteza Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa Mitaa hata katika maeneo ambayo kichama tuko imara.

2. Kuwepo kwa mashauri kadhaa Mahakama Kuu yanayotugharimu asilimali fedha na muda.

3. Viongozi wa Chama kuondolewa kwenye nafasi zao.

4. Wabunge Viti Maalum wanane kuondolewa Bungeni.

5. Madiwani kuvuliwa uanachama.

6. Kuibwa kwa fedha za ruzuku zaidi ya shilingi 1.5 bilioni na uharibifu wa mali za Chama zikiwemo magari, majengo nk.

7. Chama kushindwa kuendesha shughuli zake kwa utulivu na kujiandaa na chaguzi za ndani na za kiserikali kwa mwaka huu wa 2019 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Tunaipongeza Mahakama Kuu kwa kuwezesha kufikia hatma ya Shauri Namba 13/2017 ambalo lilitolewa uamuzi wake tarehe 18/2/2019 lililohusu Uhalali wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CUF lililofunguliwa na Ally Saleh dhidi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Registration, Insolvency and Trusteeship Agency - RITA) na Wadaiwa wengine 17 ambapo kimsingi imetoa Tamko la Kisheria (Declaratory Decree) kwamba RITA haikufuata taratibu katika kusajili wale waliodaiwa kuwa ni Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CUF waliosajiliwa na RITA tarehe 12 Juni, 2017 ambao waliwasilishwa na Profesa Ibrahim Haruna Lipumba na Magdalena Sakaya na kudhaminiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa. Mahakama imeeleza wazi kuwa mawasiliano ya RITA na Ofisi ya Msajili si kigezo pekee walichopaswa kuzingatia katika kuwasajili Wajumbe hao FEKI na kwamba RITA inapaswa kuwa waangalifu, makini, na kuhitaji kujiridhisha vyakutosha. Mimi (Ally Saleh-Mbunge wa Jimbo la Malindi- CUF) kama Mdai(Applicant) katika Shauri hilo nimeridhika na maamuzi ya Mahakama ya KUWAFUTA Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini waliosajiliwa na RITA na Mahakama kutoa angalizo kwa RITA na muongozo wa namna gani Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wanapaswa kupatikana kwa mujibu wa Katiba ya CUF na Sheria ya [The Trustees Incorporation Act. CAP 318 RE-2002]

Ndugu Wanahabari;

Leo tarehe 26/2/2019 tumeonelea ni vyema kuzungumza nanyi na kupitia kwenu kufikisha ujumbe wetu kwa Watanzania na mamlaka mbalimbali za kiutendaji katika nchi yetu juu ya Shauri Namba 23/2016 linalohusu Uhalali wa Uenyekiti wa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kwa Chama chetu cha CUF.

Shauri hili lililopo mbele ya Mheshimiwa Jaji Dkt Benhajj Masoud tayari limeshasikilizwa kwa pande zote mbili na lipo katika hatua ya kutolewa Hukumu.

Si lengo letu na wala hatukusudii kuingilia taratibu za Mahakama na au kutoa shinikizo la aina yoyote ile kwa Mahakama, isipokuwa tumepata mashaka makubwa namna tarehe 22/2/2019 Shauri hili lilivyoahirishwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kwa kueleza kuwa siku hiyohukumu haitasomwa kwa sababu Jaji amepangiwa majukumu mengine.Hofu zaidi ikaja kuonekana tarehe 17/3/2019 aliyoitaja pale katika ukumbi wa Mahakama ambayo ni siku ya Jumapili. Maswali yalikuwa mengi sana miongoni mwetu na kwa kwelihuwezi kuepuka hisia mbaya kwa Wanachama na Viongozi wetu kutokana na kauli alizozitoa Profesa Lipumba alipokuwa anazungumza na Waandishi wa Habari siku moja kabla ya hukumu, na hicho kilichotokea.

Kama haitoshi Shauri hili mpaka sasa limeshaahirishwa mara nne kama ifuatavyo;

1. Tarehe 12/10/2018

2. Tarehe 30/11/2018

3. Tarehe 15/1/2019 na

4. Tarehe 22/2/2019

Na sasa limepangiwa tarehe 18/3/2019.

Hili ni Shauri la mtu aliyejiuzulu nafasi yake ya kikatiba na kisha kurudi kuja kuidai nafasi hiyo baada ya mwaka mmoja kupita, ambapo pia Chama baada ya kuona mwenendo wake usiofaa na utovu wa nidhamu kilimchukulia hatua za kinidhamu kwa kumfukuza uanachama wake.

Kwa heshima na taadhima tunamuomba Mheshimiwa Jaji Mkuuna Mheshimiwa Jaji Kiongozi waliangazie suala hili kwa umuhimu na uzito maalum kwa sababu kuchelewa kwake kunakiathiri sana Chama chetu kwa kiasi kikubwa kama tulivyoeleza hapo juu. Kama tujuavyo kuna msemo“Justice delayed is justice denied”.

Waheshimiwa Wanahabari, ni ukweli kuwa; Tunashindwa kufanya maamuzi kadhaa ndani ya Chama chetu, tunashindwa kufanya siasa, tunashindwa kujipanga vyema kwa mambo mbalimbali na tumekuwa tukipoteza rasilimali zetu nyingi kushughulika kwenda na kurudi Mahakamani na mambo kadhaa nje ya uga wa kisiasa. Chama kimekosa kuwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti toka mwaka 2015, tunahitaji kufanya chaguzi za ndani kujaza nafasi hizi na nyingine.

Ndugu Waandishi wa Habari;

Uongozi wa Chama chetu umekwisha kusema kuwa sisi tuko tayari kupokea uamuzi wa Mahakama kama utavyotolewa na tumejipanga kwa matokeo ya aina yoyote yale. Tunaomba hukumu hiyo sasa isomwe maana muda umekuwa mkubwa ilhali Shauri lilifunguliwa kwa Hati ya Dharura toka mwaka 2016.

Tunaamini kuwa Mahakama ni chemchem ya haki, na kila raia ndio kimbilio lake na raia hao ni pamoja na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa, ambao wamechagua kujikusanya pamoja, na mkusanyiko huo unawapa haki za kisiasa na Kikatiba na haki hizo zinapotatizika basi Mahakama ndio yenye wajibu wa kuzitatua. Hukumu hii tunataraji itafanya hivyo ili tujue hatma ya Chama chetu cha CUF.

Kwa mara nyingine tena ombi letu ni kwa Mheshimiwa Jaji Mkuu na Mheshimiwa Jaji Kiongozi kuona jambo hili linafanyika kadri ya taratibu na wajibu wa ki-Mahakama unavyohitajia na kwa kutizama na ukweli kuwa uamuzi wa kesi hii utawezesha kwa njia moja au nyingine Chama cha CUF kitimize wajibu wake wa kikatiba na wajibu wake katika siasa za ushindani za Tanzania; na kwa hivyo kutimiza wajibu wake chini ya Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Jamhuri wa Muungano na Sheria zinazosimamia mambo ya siasa kote Tanzania.

Tunajua tarehe 18 Machi, 2019 sio mbali na tutasubiri. Wakati huo huo tunatoa wito kwa Wapenzi na Wanachama wetu kuwa na subira ili kulinda uhuru na taratibu za Mahakama ambazo tunaziamini.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa leo tarehe 26 Februari 2019 na Wabunge wa THE CIVIC UNITED FRONT [CUF-Chama Cha Wananchi] na kusomwa mbele ya Waandishi wa Habari.
 
HAKI SAWA KWA WOTE KUMKUMBUSHA JAJI HAKI HUINUA TAIFA SASA KAMA MTAENDELEA KUMSIKILIZA JIWE MTAACHA MAJINA MABAYA KWENYE HISTORIA YENU,NAKUMBUKA WAKATI WATU WAKIDAI UCHUNGUZI HURU KUPIGWA RISASI TUNDU LISU JAJI MKUU ANAJITOKEZA KUWA HAKUNA HAJA YA UCHUNGUZI HURU HADI LEO MNAPIGA CHENGA TU HII ILIKUA DOA KUBWA LA KWANZA KUMUAMINI JAJI
 
Maombi ya namna yeyote ya kimahakama hutakiwa kupelekwa mahakamani sio vyombo vya habari hawa CUF vipi? CUF wanachofanya ni dharau kubwa kwa mahakama
 
Kama haitoshi Shauri hili mpaka sasa limeshaahirishwa mara nne kama ifuatavyo;

1. Tarehe 12/10/2018

2. Tarehe 30/11/2018

3. Tarehe 15/1/2019 na

4. Tarehe 22/2/2019

Na sasa limepangiwa tarehe 18/3/2019.
 
Hao watu wa sefu wameshanusa kushindwa wanawekana sawa kisaikolojia tu
 
huyu jaje mkuu atauharibu huu mhimili wa mahakama kabisa....yaaani kwa sasa uonevu na matamko ya huyu jaje mkuu vinaonekana wazi kabisaaaa!!
 
Mkuu umeshawai kuwa na kesi mahakaman kwa cku za karibun tujitahidi tuwe na iman na mahakama zetu kwan hata sefu amekiri kuwa na imani nayo cjui mbowe akitoka nae atasema ako na iman nayo au hana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo mko sawa kuonesha kiu ya kuiomba Serikali ya JPM aangalie hili - CCM tutawasaidia kupata suluhu ya jambo hili

Mmesikika vizuri
 
Swala lipo mahakamani hiki kimuye muye cha nini?
Kama utasoma makala za cuf timu seif mwaka 2016,2017 na mwanzoni mwa mwaka 2018 makala zote za kulalamika kwenye mitandao mwandishi alikuwa mtatiro
Sasa hivi kazi hii ya uwandishi wa kulalamika anaifanya Mbarala
Kila ukisoma makala zao za cuf timu seif maneno ni yale yale marefu yanafanana tu hakuna kitu kipya kutoka kwao

Tuiachie mahakama itafsiri sheria
Siasa pelekeni bungeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom